SWALI
Ilkuw nina xhid na ninaomb nipat jib la hili Qn ambalo ni ..kwa kutuamia ushahid 4 ya kihistoria thibitish kuw ufufuo ni jamb jepesi
Swali No. 209
JIBU
Ushahidi wa ufufuo kutokana na historia
Miongoni mwa matukio ya kihistoria yanayothibitisha kuwepo uhai baada ya kufa ni;
i. Mtu (msafiri) na punda wake waliokufa walifufuka baada ya miaka mia (100).
Rejea Qur’an (2:259)
ii. Kufufuka ndege wanne (4) wa Nabii Ibrarahim (a.s) kama mujiza wa kuonesha uwezekano wa kufufuliwa viumbe.
Rejea Qur’an (2:260)
iii. Kuamka vijana wa pangoni baada ya kulala kipindi cha muda wa miaka 309 ili kuwa ushahidi wa kufufuka viumbe baada ya kufa.
Rejea Qur’an (18:25)
iv. Kufufuka kwa watu wa Nabii Musa (a.s) waliokufa walipotaka kumuona Allah
(s.w) kwa dhahiri (jahara).
Rejea Qur’an (2:55-56)
v. Kufufuka kwa mtu (Myahudi) aliyeuliwa kwa dhuluma zama za Nabii Musa (a.s) ili
amtaje aliyemuua baada ya kupigwa na sehemu ya nyama ya ng’ombe. Rejea Qur’an (2:72-73)
vi. Nabii Isa (a.s) kufufua wafu (watu waliokufa) kwa idhini ya Allah (s.w) kama sehemu ya muujiza wake.
Rejea Qur’an (3:49), (5:111)
Kumbukumbu
Swali hili limeulizwa na Muulizaji Kutoka WhatsApp Chat yetu tarehe 06-02-2023-18:33:58 . Jina la muulizaji limehifadhiwa.
Nicheki Nicheki WhatsApp