Huduma ya Kwanza kwa aliyeng'atwa na nyuki

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko

3.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYUKI

Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Utamjuaje kama ana aleji na nyuki?. ni pale utakapomuona aliyeng’atwa na nyuki akivimba mwili, na anaweza pia kupoteza fahamu. Pia hali hizi zinategemea ni kiasi gani cha nyuki wamemg’ata mtu.

 

Utakapomuona mtu ameng’atwa na nyuki usimkimbie, kwanza msaidie, kuhakikisha kuwa nyuki hawamng’ati tena. Unaweza kuchukuwa blanketi ama shuka uakmfunika vyema. Hakikisha na wewe umefunika pua, mgomo na masikio. Kama nyuki wanaendelea kuja mmwagie maji mgonjwa ili kupoteza harufu ya nyuki.

 

Hakikisha kabla hujaanza kutoa huduma ya kwanza, kwanza unaangalia hali ya aliyeng’atwa, kama hali ni ya kawaida na hahitaji kwenda hospitali. Kama anahitaji kwenda hospitali haraka wasiliana na kituo kilicho jirani ama tafuta msaada, kwa watu walio karibu. Hakikisha maamuzi haya hayaathiri hali ya mgonjwa. Ili kumpa huduma ya kwanza aliyeng’atwa na nyuki:-

1.kwa upole tumia kitu chenye wembamba kisha toa miiba ya nyuki kwenye ngozi ya mgonjwa. Katu usitukie kucha zako, maana zitaipasua miipa na sumu itaingia ndani na katu hutaweza kuitoa tena.

2.Unaweza kutuia kisu, ama kituchenye ncha, ila hakikisha kuwa miiba ya nyuki haikatiki kwa ndani. Kwa mfano unapotumia kiwembe kuna uwezekano mkubwa ukaikata miib kwa ndani.

3.Muweke mgonjwa mahali pa ubaridi kama inawezekana

4.Osha maeneo aliyong’atwa kwa sabuni na maji

5.Unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu.

6.Zipo dawa kama losheni (calamine lotion) ila ni maalumu kwa aliyeng’atwa na nyuki, kama zipo mgonjwa apakwe.

7.Hakikisha unamtuliza moyo mgonjwa.

8.Kama hali ni mbaya bado mgonjwa apelekwe kituo cha afya



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-10-29     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 864


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Kazi za wahudumu wa afya wakati wa kutoa dawa kwa wagojwa
Hii post inahusu zaidi kazi za wahudumu wa afya wakati wa kutoa dawa, ni kanuni zinazopaswa kufuata wakati wa kutoa dawa kwa wagojwa. Soma Zaidi...

Zijue kazi za uke (vagina)
Uke ni sehemu ambayo imo ndani ya mwili wa mwanamke, sehemu hii ufanya kazi mbalimbali hasa wakati wa kujamiiana, kubarehe na kujifungua kwa mama. Soma Zaidi...

Zijuwe athari za vidonda mwilini
Posti hii inahusu zaidi athari za kutotibu vidonda, hizi ni athari mbalimbali ambazo zinaweza kutokea ingawa kama vidonge haujatibiwa au vimetibiwa kwa kuchelewa. Soma Zaidi...

Njia za kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya njia za kuongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...

Fahamu kuhsu vitamini E na kazi zake mwilini
Je unazijuwa faida za kuwa na vitamini E mwilini mwako.Unahani utapata matatizo yapi ya kiafya endapo utakuwa na upungufu wa vitamini E mwilini? Makala hii ni kwa ajili yako. Soma Zaidi...

Zijue kazi za ini
Post hii inahusu zaidi kazi za ini, ni kiungo muhimu kwenye mwili ambacho Kina umuhimu sana, bila ini maisha ya mwanadamu yanaweza kuishia pabaya Soma Zaidi...

Njia juu zinazosababisha kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi
Post hii inahusu zaidi njia za kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini. Soma Zaidi...

Mbinu za kupunguza magonjwa yanayohusiana na figo
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa figo. Ni ugonjwa unaotokana pale figo linaposhindwa kufanya kazi, tuone mbinu za kufanya Ili kuepuka na tatizo hilo. Soma Zaidi...

Huduma kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo
Post hii inahusu zaidi huduma Kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo,ni huduma maalumu ya kumsaidia mgonjwa aliyepata maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo. Soma Zaidi...

Mzunguko wa mwezi kwa mwanamke
Posti hii inahusu zaidi mzunguko wa mwezi kwa mwanamke, ni mzunguko ambao huchukua siku ishilini na nane kwa kawaida Ila lla ubadilika kulingana na mtu, Ila ngoja tuangalie siku ishilini na nane tu. Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa Soma Zaidi...

Namna ya kutunza nywele za mgonjwa
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi. Soma Zaidi...