HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATA JOTO LA JUU ZAIDI (HEAT STROKE)
Hii ni hali inayotokea ambapo wili unakuwa na joto la juu sana tofauti na kawaida.
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATA JOTO LA JUU ZAIDI (HEAT STROKE)
Hii ni hali inayotokea ambapo wili unakuwa na joto la juu sana tofauti na kawaida. Joto linaweza kufika nyuzi 40 za sentigredi. Hali hii inaweza kupelekea kufa kwa viungo vya ndani kama ini, figo moyo na ubongo. Ukikutana na mgonjwa wa hali hii kwa hakika anahitaji huduma ya kwanza haraka iwezekanavyo.
Endapo mgonjwa huyu hduma ya kwanza ikichelewa inaweza kuhatarisha maisha yake ama uharibifu wa afya yake kwa ujumla. Endapo hali hii itaambatana na homa kali, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutokwa n adamu za pua, ama kuchanganyikiwa mpeleke mgonjwa kituo cha afya. Huduma ya kwanza kwa mgonjwa huyu ni kama ifuatavyo:
1.mpunguzie mgonjwa nguo, abakiwe na nguo laini na chache
2.Mpeleke sehemu iliyopoa nabyenye baridi
3.Mpe maji yaliyopoa anywe
4.Tumia nguo mbichi na iliyopowa, ama sponji lenge maji yaliyopoa, fanya kama una mfuta mgonjwa.
5.Kama kuna feni karibu unaweza utumia ama muweke kwenye IC.
6.kama hali inaendelea basi awahishwe kituo cha afya mara moja.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 web hosting 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Aina za kuungua
Post hii inahusu Aina za kuungua, kuungua ni Hali ya kubabuka kwa ngozi ya mwili na kusababisha madhara mbalimbali
Soma Zaidi...Kazi za mifupa mwilinj
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa mifupa mwilini, mifupa ni mojawapo ya tushy zilizounganika na ufanya kazi kubwa kwenye mwili.
Soma Zaidi...Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa walio na majeraha ya macho.
Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa walio na majeraha ya macho kutokana na aina mbalimbali ya jeraha
Soma Zaidi...Madhara ya kuchelewa kutibu tatizo la kiafya
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea endapo tatizo halijatibiwa.
Soma Zaidi...Namna ya kusaidia vijana wakati wa kubarehe
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia vijana wakati wa kubarehe, ni njia za kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na mwelekeo ,
Soma Zaidi...Vyakula vya fati na mafuta
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya fati na mafuta
Soma Zaidi...