IJUWE SWALA YA MTUME NA FADHILA ZAKE NA JINSI YA KUMSWALIA MTUME.


image


Post hii itakufundisha jinsi ya kumswalia mtume, pamoja na kuzijuwa fadhila unazopata kwa kumswalia Mtume



SWALA YA MTUME
Kumswalia Mtume (s.a.w) ni nguzo ya swala inayofuatia baada ya kusoma Tahiyyatu. Kumswalia Mtume si faradhi katika swala tu bali pia ni faradhi kumswalia kila anapotajwa kwa jina lake. Msisitizo wa amri ya kumswalia Mtume unaonekana katika aya ifuatayo:

“Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume; na Malaika wake (wanamuombea dua). Basi; enyi Mlioamini msalieni (Mtume, muombeeni Rehema) na amani”. (33:56)

Pia katika maana ya hadithi nyingine Mtume (s.a.w) amesema kuwa bahili ni mtu ambaye atatajwa Mtume (s.a.w) kisha asimswalie.

Pia hadithi zifuatazo zinasisitiza umuhimu wa kumswalia Mtume (s.a.w) kila atajwapo na kila mtu apatapo wasaa. Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Bakhili ni yule anayesikia nikitajwa, lakini haniswalii. (hanitakii rehma). (Tirmidh).

Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Anayenitakia Rehma (anayeniswalia) mara moja, Allah humrehemu mara kumi”. (Muslim).

“Ibn Mas’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayekuwa kipenzi changu katika watu, katika siku ya Kiama atakuwa ni yule aliye mbele kuliko wote katika kunitakia Rehma (kuniswalia). (Tirmidh).

Namna ya kumswalia Mtume (s.a.w) imeelezwa katika Hadithi nyingi lakini iliyomashuhuri katika hizo ni ile iliyosimuliwa na Abdur- Rahman bin Ubaidillah(r.a) na kupokelewa na Maimamu wote wa Hadithi kuwa Mtume (s,.a.w) ametufundisha tumswalie (tumtakie Rehma) kama ifuatavyo;

“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka hamiidum-majid”

Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Dua za kuomba wakati unapokuwa na maumivu kwenye mwili
Posti hii inakwenda kukufundisha dua za kuomba wakati wa kuwa na maumivu kwenye mwili wako. Soma Zaidi...

image Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hujibiwa kwa urahisi
Post hii inakwenda kukugundisha ni nyakati zipi ambazo Allah hukubali dua kwa urahisi. Soma Zaidi...

image Utofauti wa dua ya kafiri na dua ya muislamu katika kujibiwa
Posti hii inakwenda kukufundisha ni kwa nini dua ya kafiri inawwza kujibiwa wakati ya muumini haijibiwi. Soma Zaidi...

image Masharti ya kukubaliwa kwa dua
Post hii itakwenda kukugundisha masharti yanayofungamana na kukubaliwa kwa dua. Soma Zaidi...

image Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua. Soma Zaidi...

image JINSI YA KUOMBA DUA ILI IKUBALIWE NA ALLAH
Kukubaliwa kwa dua kunategemea mahusiano yako na Allah. hata hivyo kuna baadhi ya mabo ukiyafanya dua yako inaweza kukubaliwa kwa haraka zaidi. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kuomba dua ikubaliwe. Soma Zaidi...

image Dua za kuomba wakati unapokuwa na hasira ama ukiwa umekasirika
Post hii itakueleza ni dua gani unatakiwa uzisome wakati unapokiwa na hasira ama pale unapokasirika. Soma Zaidi...

image Dua 10 ambazo ni muhimu kuziomba kwa kila siku.
Posti hii inakwenda kukupa orodha ya dua 10 ambazo unaweza kuziomba kila siku. Soma Zaidi...

image Matamshi ambayo ukimwambia Allah kwenye dua yako basi hujibiwa kwa haraka dua hiyo
Post hii inakwenda kukufundisha matamshi ambayo mtu akiyatamka Allah hujibu dua hiyo kwa urahisi. Soma Zaidi...

image Maana ya dua na fadhila zake
Dua ni moja ya Ibada ambazo tunatakiwa kuziganya kila siku. Kuna fadhila nyingi sana za kuomba dua. Post hiibitakwenda kukujuza fadhila za kuomba dua. Soma Zaidi...