Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.
Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.w) kwa sauti ya kawaida pasina kumuona. Kutokana na ushahidi wa Qur-an njia hii imetumika kwa Mitume na wateule wengine wa Allah (s.w).
Nabii Mussa (a.s) ni miongoni mwa Mitume waliosemeshwa na Allah (s.w).kama tunavyofahamishwa kisa chake katika Qur-an: Basi Musa alipotimiza muda, akasafiri pamoja na ahali zake (watu wake kurejea kwao Misri). Aliona moto upande wa mlimani akawaambia ahali zake; ‘Ngojeni, hakika nimeona moto, labda nitakuleteeni habari za huko au kijinga cha moto ili muote! (28:29) 8 Basi alipoufikia aliitwa kutoka upande wa kuliani wa bonde hilo katika kiwanja kilichobarikiwa, kutoka mtini: “Ewe Mussa! Bila shaka mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu.” (28:30) Kwa njia ya nyuma ya pazia, Nabii Mussa (a.s) aliongea na Allah mara nyingi na mara zote hizo hakuweza kumuona. Alipoomba amuone alijibiwa kama inavyooneshwa katika aya zifuatazo:
Na alipofika Mussa katika miadi yetu na Mola wake akazungumza naye, (Mussa) akasema: “Mola wangu! Nionyeshe (nafsi yako) ili nikuone” Akasema (Mwenyezi Mungu): “Hutaniona, lakini tazama jabali (lililoko mbele yako) kama litakaa mahali pake utaweza kuniona”. Basi Mola wake alipojionyesha katika jabali, alilifanya liwe lenye kuvunjika vunjika na Mussa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema “Utukufu ni wako. Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa wanaoamini (haya)” (7:143).
Pia tunafahamishwa katika Qur-an kuwa Bibi Maryam, mama wa Nabii Issa (a.s) naye aliongeleshwa nyuma ya pazia wakati wa kumzaa Issa Bin Maryamu kama ilivyo katika aya zifuatazo: 9 “Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema:“Laiti ningelikufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.(19:23) Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake ikamwambia usihuzunike. Hakika Mola wako amejaalia kijito cha maji chini yako.(19:24) na litikise kwako shina la mtende, litakuangushia tende nzuri, zilizo mbivu. (19:25) Basi ule na unywe na litulie jicho (lako). Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari juu ya mtoto huyu), sema:“Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehma ya kufunga, kwa hiyo leo sitasema na mtu” (19:26).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Tendo la zinaa ni tendo chafu kimaadili na Allah (s.
Soma Zaidi...“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako?
Soma Zaidi...Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa
Soma Zaidi...Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine.
Soma Zaidi...Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s.
Soma Zaidi...Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira?
Soma Zaidi...Hili ni swali kutoka katika maarifa ya elimu ya dini ya kiislamu kidato cha kwanza (EDK FORM 1)
Soma Zaidi...