Mafundisho ya Mitume

Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.

Mafundisho ya Mitume

Mafundisho ya Mitume


Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.w).Dalili zinazodhihirisha kuwepo Allah (s.w) katika eneo hili ni pamoja na:



(a)Umoja wa ujumbe wa mitume



(b)Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao



(c)Upeo wa elimu waliyokuwa nayo mitume.

Kitu kinachodhihirisha kuwa Mitume ambao baadhi yao ulimwengu mzima una shuhudia historia yao, kama vile historia ya Nabii Ibrahim (a.s), Musa (a.s), Isa (a.s) na Muhammad (s.a.w) kuwa ni wajumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) wenye ujuzi na hekima, ni kule kufanana kwa ujumbe wao.


Kama dhana ya kutokuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) ingelikuwa kweli, ingelikuwa muhali kwa Mitume waliotokea sehemu tofauti nyakati tofauti, kutoa ujumbe unaofanana. Turejee katika Qur-an mifano michache ya mafundisho ya msingi waliyotoa Mitume kwa watu wa o:Tulipompeleka Nuhu kwa watu wake, naye akasema: 'Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu.


Nyinyi hamna Mungu ila Yeye.Hakika mimi ninakuhofieni adhabu ya siku (hiyo) iliyo kuu '. (7:59).Na kwa Adi (tulimpeleka) ndugu yao Hudi, akasema: 'Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Basi hamuogopi? (7:65).


Na kwa thamud (tulimpeleka) ndugu yao, Saleh. Akasema 'Enyi watu w angu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mola ila Yeye. Hakika umekwisha kukufikieni muujiza ulio dhahiri kutoka kwa Mola wenu. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye na ishara kwenu (ya Utume wangu).


Basi muacheni ale katika ardhi ya Mungu, wala msimtie katika dhara yoyote, isije ikakushikeni adhabu iumizayo. (7:73).


(iv) Shu'ayb (a.s)
Na kwa watu wa Madyan (tulimpeleka) ndugu yao, Shu'ayb, akasema:


'Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, hamna Mungu mwingine isipokuwa Yeye. Zimekwisha kufikieni hoja dhahiri kutoka kwa Mola wenu. Basi kamilisheni sawa sawa vipimo (vya vibaba) na mizani (pia) wala msiwapunguzie watu vitu vyao wala msifanye uharibifu katika ardhi badala ya kutengenea kwake. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi mumeamini. (7:85).


Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Mola wenu. Basi muabuduni. Hii ni njia iliyonyooka. (19:36)
(vi) Muhammad (s.a.w)



Sema (ewe Muhammad): 'Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote; (Mungu) ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi, hakuna aabudiwaye (kwa haki) ila yeye, yeye ndiye ahuishaye na ndiye afishaye.Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, aliye Nabii Ummiyyi (asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye humuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka'. (7:158)


'Na bila shaka tulimpeleka mtume katika kila umma ya kwamba, 'Muabuduni Mwenyezi Mungu na mwepukeni twaghuti. Basi wako miongoni mwao ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa na wako miongoni mwao ambao upotofu umethubutu juu yao. Basi tembeeni katika ardhi na mwangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha '. (16:36)
Ukirejea katika Qur-an utaona kuwa Mitume wote kwa ujumla wamefundisha yafuatayo:-



(i)Tawh iid
Wamewafundisha watu juu ya kuwepo Allah (s.w) na upweke wake kwa kuwaonyesha dalili zilizo waziwazi.



(ii)Lengo
Waliwafundisha watu kuwa lengo la kuumbwa kwao ni kumuabudu Allah (s.w) na kusimamisha ukhalifa wake hapaulimwenguni na kisha waliwafundisha namna ya kumuabudu Mola wao katika kila kipengele cha maisha.



(iii)Kubashiria
Waliwabashiria watu malipo mema ya kudumu ya huko Peponi kwa wale watakaoamini vilivyo na kutenda mema katika maisha yao ya hapa duniani.



(iv)Kuhofisha
Waliwahofisha watu juu adhabu kali watakayopata huko Akhera wale watakao mkufuru Allah (s.w) na kumwabudu twaghu ti.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 212

Post zifazofanana:-

kanunu na sheria za biashara katika islamu
Soma Zaidi...

Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini
hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini Soma Zaidi...

Namna ya kutoa na kuhesabu zake, masharti ya zaka na nguzo zake, nani inampasa kutoa ama kupewa zaka na sadaka
4. Soma Zaidi...

Khalifa 'Umar bin Abdul Aziz
Soma Zaidi...

Ndoa ya mke zaidi ya mmoja na taratibu zake
Soma Zaidi...

Historia ya Vijana wa Pangoni
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s. Soma Zaidi...

VYANZO VYA VYAKULA VYA VITAMINI NA FAIDA ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

JINSI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE
NJIA RAHISI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE Teknolojia ya mawasiliano ni muhimu katika kuhakikisha kuwa ulimwengu unafikika kama kijiji kimoja na hapa ndipo unapata maana halisi ya neno UTANDAWAZA yaani kwa lugha ya kimombo ni globalization. Soma Zaidi...

Sharti za kusihi kwa funga
Soma Zaidi...

TAHARUKI YA MFALME WA BAGHADANI
Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

NECTA FORM TWO CHEMISTRY PAST PAPERS
Soma Zaidi...