Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini.
Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini. Hii ni kwa sababu:
1.Imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha Muumini na kumshirikisha Allah (s.w) na viumbe vyake, hasa vile visivyoonekana, miongoni mwa hivyo ni Malaika na Majini.
2.Muislamu anaamini kuwa Malaika ni viumbe watukufu ambao wametakasika na dhambi na kila aina ya uchafu, lakini binaadamu amepewa daraja ya juu zaidi pindi atakapotimiza wajibu wake kama Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani. Imani hii humpelekea mtu kujitahidi upeo wa uwezo wake kuishi maisha yanayolingana na cheo hiki kikubwa, cheo ambacho Malaika walikitamani (Rejea Qur-an, 2:30)..
3.Muislam anaamini kuwa kila wakati na kila alipo yu pamoja na Malaika watukufu. Imani hii peke yake inatosha kumfanya mtu abadili tabia yake. Hii ni kwa sababu binaadamu ameumbwa na haya, kwa hiyo huhuzunika akifanya mambo maovu mbele ya watu na hasa mbele ya watu anaowaheshimu.
4.Muislamu anaamini kuwa Malaika hao sio tu kuwa wapo naye daima bali wanahudhurisha mbele ya Allah (s.w) kila anachokitenda. Imani hii ikithibiti moyoni humfanya Muislam ajitahidi kufanya mambo mema na ajitahidi kuepuka maovu.
5.Muislamu anajua kuwa Malaika sio tu hupendezwa na mema, bali pia humuombea mtu huyo anayefanya mema, maghfira kwa Allah (s.w) jambo ambalo humzidishia Muislamu hima ya kutenda mema daima na kujiepusha na maovu hata akiwa peke yake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)
Soma Zaidi...Ushahidi wa kuthibitisha kutendeka kwa kosa la uzinifu unapatikana kwa namna tatu zifuatzo: (i)Kushuhudia tendo hilo likifanyika kwa wakati mmoja watu wanne Mukalafu (Walio baleghe na wenye akili timamu), wakiwa ni Waislamu waadilifu.
Soma Zaidi...Faradhi kwa maiti ya muislamu (edk form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.
Soma Zaidi...