Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama

Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama

Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama




Mtume (s.a.w) pia ametutajia dalili kubwa za kukaribia kwa siku ya Mwisho. Dalili hizo zinapatikana katika Qur'an na Hadith kama inavyobainishwa hapa chini:'Na kitakapokaribia Kiyama, tutawatolea mnyama kutoka ardhini atawaeleza (watu) kwa kuwa watu walikuwa hawaziamini aya zetu' (27:82)'Mpaka watakapofunguliwa Ya'juj na Ma'juj nao wataporomoka kwa kasi, na ikakaribia ahadi ya kweli kufunguliwa, hesabu na malipo, basi wakati huo macho ya makafiriyatatokeza mno juu ' (21:96 ' 97)
Katika hadith aliyoipokea Imam Ahmad, na kusimuliwa na Khudhaifa Ibn Usaid Al ' Ghifaar (r.a) amesema; Alitutokea Mtume (s.aw) kutoka chumbani kwake na sisi tukikumbushana jambo la kiyama, Mtume (s.a.w) akasema: Hakitosimama Kiyama mpaka muone alama kumi,



1. Kuchomoza jua Magharibi



2. Kutokea moshi mkubwa utakaochafua mazingira (pollution)



3. Mnyama atatokeza na kuwasemesha watu (27:82)



4. Kufunguliwa Ya'juj na Ma'juj (21:96 97)



5. Kurudi kwa Issa mwana wa Maryam



6.Kuja kwa Masih Dajal (False Messayah)



7.Kutoka Moto (Volcano) katika pango la Aden ukiwaendesha watu



8.Dunia kugawika mapande matatu (Three Blocks); Pande la Mashariki (Eastern Block)



9.Pande la Magharibi na (western block)



10.Bara Arab (Mashariki ya kati - Middle East)
Kwa hakika Qur'an imetaja dalili nyingi mno, Rejea Suratul qiyaamah (75:6 ' 9) na nyinginezo nyingi zilizotajwa katika hadith mbali mbali.
Kuamini siku ya mwisho ni kuamini kuwa kuna maisha ya milele baada ya maisha haya ya hapa duniani. Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur-an, maisha hayo yatakuwa na hatua kuu nne zifu atazo:



(i)kutokwa na roho



(ii)Maisha ya kaburini - Barzakh.



(iii)Kufufuka na kuhudhurishwa mbele ya Allah (s.w) na kuhesabiwa.



(iv)Maisha ya kukaa Peponi milele kwa watu wema au kukaa motoni kwa watu waovu.Aidha kwa kuzingatia matukio yatakayotokea katika hatua nne za maisha yajayo,





                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 985


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?
Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu? Soma Zaidi...

DUA 11 - 20
11. Soma Zaidi...

SIRI YA KIFO INAFICHUKA
Soma Zaidi...

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu
1. Soma Zaidi...

Ndoa ya kwanza ya kamaralzamani
NDOA YA HAMU Basi hali ikawa kama hivyo wawili hawa binamu na Kamaralzamani wakaanza kupanga njama ya kuweza kuondoka eneo lile kuelekea nchi za mbali kwa ajili ya kukutana na binti mfalme. Soma Zaidi...

DUA BAADA YA TAHIYATU, NA KUTOA SALAMU KWENYE SWALA
13. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA QALQALA
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Muhtasari wa madili malezi ya jamii kama ilivyobainishwa katika Qur-an
(v)Kuwaombea dua wazazi. Soma Zaidi...

Masiku ya Tashiq, kuchinja na kufanya tawafu ya kuaga
8. Soma Zaidi...

Kuamini siku ya mwiho: Pia utajifunza kuhusu maisha ya barzakh (kaburini), siku ya qiyama
Soma Zaidi...

NINI MAANA YA KUSIMAMISHA SWALA, KATIKA UISLAMU (NI YUPI TARQU SWALA) yaani mwenye kuacha swala)
Kusimamisha Swala. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 37: Allaah Kaviandika Vitendo Vyema Na Vibaya
Soma Zaidi...