Karanga (groundnuts)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga

. Karanga (ground nuts)

Karanga ni katika vyakula vya asili na ni kiungio cha mboga kwa jamii nyingi sana Tanzania na dunia kwa ujumla. Kama vilivyo vyakula vingine karanga ni katika vyakula vyenye virutubisho vingi. Ndani ya karanga kuna fotale, vitamin E, madini ya copper na arginine. Pia karanga ni chanzo kizuri cha omega-3 fatty acid, vitamin E na ijulikane kuwa fatty acid ni muhimu sana kwa afya ya moyo.

 

Ndani ya kjaranga kuna antioxidant iitwayo phenolic, polyphenol na resveratrol hizi husaidia katika kulinda mwili dhidi ya stress yaani misongo ya mawazo, na husaidia pia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya saratani. Pia husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini yaani mfumo wa kupambamba na maradhi na mashambulizi ya magonjwa.

 

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa aina ya mafuta (fat) yaliyomo kwenye karanga ni mafuta ambayo ni salama kwa afya ya moyo. Kitaalamu aina ya fat iliyomo kwenye karanga ni monosaturated fat na polyunsaturated fat kwa ufupi fat hizi ni salama kwa afya ya moyo na mfumo mzima wa usukiumwaji wa damu. Kwani fat hizi husaidia katika kupunguza cholesterol kwenye damu hivyo hupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo.

 

Karanga pia ni chanzo kizuri cha protini. Itambulike kuwa protini ni katika virutubisho muhimu na vinavyotakiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya miili yetu. Seli za mwili zinahitaji protini kuweza kukuwa na kutengenezwa upya. Ukuaji wa mwili na uponaji wa vidonda na majeraha unahitaji protini.. watoto wanatakiwa wapewe vyakula vya protini kwa kiasi kikubwa zaidi ili kuwezesha maendeleo ya ukuaji wao.

 

Tofauti na protini mwili unahitaji madini kwa kiwango kinachohitajika. Katika karanga kuna aina mbalimbali za madini kama vile magnesium, phosphorus, potassium, zinc, calcium na sodium. Madini yote haya husaidia katika ukuaji wa mwili na mwili kufanya kazi vyema.

 

Mafuta ya karanga yana fatty acid ambayo hutambulika kuwa inaongeza lipoprotein ndani ya mwili inayojulikana kama “good cholesterol” yaani cholesterol iloyo safi. Hii ni muhimu katika kuimarisha afya ya moyo na ubongo. Pia madini ya copper yaliyomo kwenye karanga husaidia katika kuzuia maradhi ya moyo yaani “coronary heart diseases”. pia vitamin B1 (thiamine) ni virutubisho muhimu katika kulinda mwili dhidi ya ufanyaji dhaifu wa kazi wa moyo. Yaani “cardiac failure”. na pia husaidia katika kuimarisha afya ya moyo.

 

Karanga husaidia katika kuboresha ngozi. Virutubisho vilivyomo kwenye karanga pamoja na vitamin C husaidia katika kuilinda ngozi dhili ya mikunjo mikunjo, madowa madowa na kuifanya ngozi iwe ang’avu, yenye majimaji na iyoyokuwa na ukavu au mikunjomikunjo. Uwepo wa anti-ageing phytohemical inayotambulika kama reseveratrol husaidia katika kumfanya mtu asizeheke kwa haraka.

 

Karanga husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa, kutokana na uwepo wa madini kama potassium, calcium, sodium, magnesium na phosphorus. Pia kwa wajawazito nivyema wakatumia chakula hiki kwani kuna protini na madini kwa ajili ya afya ya mama na mtoto



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-10-30     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1419


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Faida za muarobaini
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za muarobaini Soma Zaidi...

Limao (lemon)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula limao Soma Zaidi...

Faida za kitunguu maji/ onion
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu umuhimu wa kitunguu maji mwilini Soma Zaidi...

Faida za kula tango
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula korosho
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula korosho Soma Zaidi...

Je ni kweli vitunguu saumu vinashusha presure
Kitunguu saumu ni tiba mbadala ya presha yabkushuja. Hakitatui tatizo yaani hakiponyeshi, ila husaidia katika kushusha presha iliyo panda. Soma Zaidi...

Faida za mchaichai/ lemongrass
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mchaichai Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula spinach
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kunazi/ lote tree
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kunazi/ lotetree Soma Zaidi...

Dalili za ukosefu wa madini ya iodini (goiter)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za upungufu wa iodini ambapo kitaalamu hujulikana Kama goiter. Goiter Ni Sababu ya kawaida ya goiter duniani kote ni ukosefu wa iodini katika chakula. Nchini Marekani, ambako utumiaji wa chumvi yenye iodini ni j Soma Zaidi...

Mafidodo (mafindofindo) au tonsils kweye koo je inaweza ikawa Ni moja kati ya dalil za ukimwi
Tezi za lymph huanza kuonyesha dalili za kuwa mwili upo katika mapambano dhidi ya vijidudu vya maradhi. Ishara ni pale utakapoona tezi za lymph zina maumivu. Tezi hizi hupatikana kwenye mapaja, kwapa nashingo. Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo baada ya kula
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula Soma Zaidi...