Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)


Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)


imageKatika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume

Imepokelewa toka kwa Humraan mwachwa huru wa ‘Uthmaan kwamba alimwona ‘Uthmaan bin ‘Affaan akiagiza chombo, kisha akamimina (maji) juu ya viganja vyake mara tatu na kuviosha.

 

Kisha akauingiza mkono wake wa kuume kwenye chombo, akasukutua na kupaliza  maji puani. Kisha akaosha uso wake mara tatu, na mikono yake hadi kwenye viwiko mara tatu.

 

Halafu akapukusa (akapangusa/ akafuta) kichwa chake, kisha akaosha miguu yake mara tatu hadi kwenye vifundo, kisha akasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

(( ?? ???? ??? ????? ???? ?? ??? ?????? ?? ???? ????? ????? ??? ?? ?? ???? ?? ????))

((Mwenye kutawadha mfano wa wudhuu wangu huu, kisha akaswali rakaa mbili, haizungumzishi nafsi yake ndani yake, hughufiriwa (atafutiwa) madhambi yake yaliyopita)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (158) na Muslim (226)].

 

 

Na kutokana na Hadiyth hii na nyinginezo zitakazokuja kuzungumziwa kwa ufafanuzi, tunaweza kuiweka sifa ya wudhuu katika haya yafuatayo:

 

 

1-Atanuwia wudhuu kwa ajili ya kuondosha hadathi.

 

2-Atalidhukuru Jina la Allaah Mtukufu (yaani kusema Bismillah).

 

3-Ataviosha viganja vyake mara tatu.

 

4-Atateka maji kwa mkono wake wa kuume, kisha atayaweka mdomoni na puani kwa teko moja, atasukutua na kupaliza.

 

5-Atapenga kwa kutumia mkono wake wa kushoto. Atafanya hivi mara tatu.

 

6-Ataosha uso wake wote mara tatu pamoja na kupachanyisha ndevu.

 

7-Ataiosha mikono yake miwili – wa kulia kisha wa kushoto – mpaka juu ya viwiko viwili pamoja na kupachanyisha vidole vya mikono miwili.

 

8-Atapukusa (pangusa/futa) kichwa chake chote kwenda nyuma na mbele mara moja.

 

9-Atapukusa (pangusa/futa) masikio yake mawili nje na ndani.

 

10-Ataosha miguu yake miwili pamoja na vifundo vyake viwili - wa kulia kisha wa kushoto - pamoja na kupachanyisha vidole vya miguu miwili.Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-06

RELATED POSTS

picha
JE MANII NI TWAHARA AU NAJISI?


Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara
picha
MAMBO YANAYOWEZA KUTOA UDHU WAKO


Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu.
picha
TWAHARA NA UMUHIMU WAKE KATIKA UISLAMU


Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria.
picha
MAMBO YALIYO HARAMU KWA MWENYE HEDHI NA NIFASI


Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa
picha
ZIJUWE NGUZO TANO ZA UISLAMU NA MAANA ZAKE KATIKA SHERIA YA UISLAMU


Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa
picha
FADHILA ZA UDHU YAANI FAIDA ZA UDHU


Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu
picha
JINSI YA KUTWAHARISHA AINA MBALIMBALI ZA NAJISI


Kila najisi ina namna yake ya kutwaharisha, hata hivyo namna
picha
AINA ZA NAJISI NA TWAHARA KATIKA UISLAMU


Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina