image

Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 8

Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.

SOMO LA NANE

Katika somo lililotangulia tumejifunz namna ya kubadili jina kwenye table pia tukaona kuongeza column. Sasa katika somo hili hasa ndipo tunakwenda kuweka data kwenye table yetu, yaani kuweka data kwenye database. Katika somo hili tunakwenda kutumia ile table tulioiita post.

 

1. Kuweka data kwenye table kwa kutumia MySQL

Kama tulivyofanya kwenye masomo yaliyotangulia kuwa tunatumia MySQl kisha tunatumia SQL statement hivyohivyo ndivyo tutakavyofanya kwenye somo hili.Ili kuweka taarifa kwenye database yako fuata hatuwa zifuata:-

 

  1. Fifya hiyo table yenye jina post
  2. Kwenye menu juu bofya neno insert
  3. Ukurasa wenye vijumba vingi utafunguka
  4. utaona kuna column zile ambazo tumetengeneza aina zake za data na character leght. Sasa wewe unachotakiwa ni kutafuta palipoandikwa value chini yake kuna hivyo vijumba.
  5. Angalia mpangilio wa hiyo menu. Imeanza column, kisha type kisha Function kisha Null kisha Value.
  6. Hivyo utaangalia kwenye column kama ni Id utaweka value yake kwenye kijumba cha value. Weka namba moja kwenye id
  7. Angalia kwenye column baada ya id inafata title nenda upande wa kulia kwenye value weka jina la kichwa cha habari cha post yako mfanp “mafunzo ya html”
  8. Angalia column nyngine ambayo ni summaery kwenye value weka mhutasari wa ppost yako mafano “post hii itakwenda kukujuwa maana ya HTML”
  9. Cheki tene kenye column inafata content hapo weka maudhui ya post yako mfano “HTML ni kifupisho cha Hypertext Markup Language”
  10. Kisha kwenye image weka link ya picha yako mfano  unaweza kutumia link hii “https://bongomakataba.web.app/images/sampo.png”
  11. Kwenye publisher weka jina lako mfano “Bongoclass”
  12. Kwenye date angalia kwenye value utaona kajialama ka kalenda kadogo bofya hako kisha bofya tarehe ya leo utaona imekaa.
  13. Kisha bofya GO.
  14. Mpaka kufika hapo utakuwa umeongeza data. Kwenye menu juu bofya browser utaona post yako.
  15. Baada ya hapo ingia kwenye structure
  16. Kwenye column ya id kulia bofya change kama vile unataka kuiedit
  17. Angalia kwenye A_I au autoincement kama pana tiki, kama hapana weka tiki kisha save, kama ipo rudi nyuma.
  18. Angalia kwenye column ya edit kuliani mwa neno change kuna neno linasomeka more bofya hapo kisha kwenye menu itakayokuja bofya unique, kuna kaujumbe katakuja weka ok
  19. Kuipa column unique maana yake tunataka isifanane datazake. Kwa mfano kama post ina id 1 isitokee nyingine ikawa na namba hiyohiyo.
  20. Rudi kwenye browser.
  21. Utaona post yako uliyoweka pamoja na menu nyingine kama edit na nyinginezo.

Fanya hivi kuweka posta zaidi na kwenye menu weka menu inayoitwa afya.

 

2. Kuweka data kwenye table kwa kutumia SQL

Sasa tunakwenda kuongeza data kwenye table yetu menu. Tujaalie tunataka kuweka menu ya afya kwenye blog yetu sasa tunakwenda kuongeza menu ya afya.

 

Kwanza tuedit table ya menu nayo iwena unique kama tulivyofanya kwenye post. Hivyo ingia kwenye structure, kwenye id bofya change, angalia kwenye Null kama kuna tiki ondoa, angalia kwenye A_I  kama hakuna tiki weka, kisha save.

 

Kwenye id nenda pembeni ya change bofya more, kisha unique kisha kwenye kaujumbe utakaokuja bofya OK.

 

Kisha edit na hiyo title ingia change kwenye null ondoa tiki kisha save. Baada ya hapo table yetu tutakuwa tumeiandaa vyema kwa ajili ya kutumia SQL kwa urahisi kabisa. Sasa ili uweze kuweka data kwa kutumia SQl fuata hatuwa hizi:-

 

  1. Ingia kwenye uwanja wa SQl
  2. Ili kuweka data kwa kutumia SQl huwa tunatumia INSERT INTO kisha jina la table kisha weka mabano na ndani yake utaandika majina ya column mfano id na title utatenganisha kwa kutumia alama ya koma (,) ila neno la mwisho halina koma kisha utafunga mabano. Baada ya hapo ni kuweka value, value maana ya ke ni thamani, aua hicho unachotaka kukiweka kwenye hiyo column. Value nayo itakuwa ndani ya mabano kwa kulingana na mabano ya mwanzo.
  3. Yaani thamani ya id itaana kisha itafata thamani ya title. Hivyo itasome ka kama:-
  4. INSERT INTO `menu` (`id`, `title`) VALUES (NULL, 'afya'); hapo kwenye null kule itaweka namba yenye kwa kuwa umeiambia kwenye A_I. ila ukitaka unaweza kuweka namba wewe mfano
  5. INSERT INTO `menu` (`id`, `title`) VALUES (4, 'afya');
  6. Mpaka kufikia hapo utakuwa umeongeza menu ya afya kwenye table yako.
  7. Fanya hivi kuongeza menu zaidi.

 

3. Kuedit na kufuta data kwenye table

Kuedit data kwenye MySQl rahisi sana. Kwanza bofya hiyo table mfano post. Kisha bofya browser utaona data zako.utaone katika kila row yako ya data kuna neno edit na delete. Unachotakiwa kufanya ni kubofya edit ama delete. Ukibofya delete maana yake unafuta. Na ukibofya edit maana yake utaedit.ukimaliza kuedit bofya neno GO na hapo data yako itakuwa imebadilika.

 

Pia MySQL inakupa fursa ya kuedit humohumo huku tunaita inline edit. Unachotakiwa kufanya kama unataka kuedit column ya conten bofya hapo, kwenye data yenyewe ya kontente yaani maandishi ambayo umesha andika. Baada ya hapo utaona kamsitari ka kuonesha sasa unaweza kuedit. Hakuna haja ya kusave ukiodoka tu hapo itasave automatik. Ama unaweza pia kubofya pembeni ambapo hapana maandishi itasave yenyewe automatiki.

 

4. Kufuta ama kuedit kwa kutumia SQL

Kwa kutumia SQL pia unaweza kufuta data kwenye database ama kuedit. Ila jambo hili tutajifunza katika masomo yanayofuata kwa sasa tuendelee kutumia MySQL interface kufanya haya.

 

Somo linalofuata tutajifunza namna ya kusoma data kwenye database. Kazi yako kwa sasa kablya ya kuingia somo lijalo ni kuhakikisha kuwa umeweka data nyingi zaidi kwenye table zako. Unaweza kupost posta 5 kwenye dabke ya post na menu hivyo hivyoo ama zaidi ya hapo.

 

 

Mafunzo haya yamekujia kwa Ihsani ya bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: mafunzo@bongoclass.com

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tehama Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 954


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 5 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 5)
Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file. Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE MYSQL na SQL somo la 1
Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

PHP level 11 somo la kumi na moja (11)
Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database MySQL database somo la 9
haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 8 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Katika somo hili la 8 mafunzo ya html level 8 utajifunza jinsi ya kuhost project ya html na kuwa live, watu wakaipitia na kusoma maudhui yake. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 1 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 3 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi. Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la nne (4)
somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza (basic level)
Huu ni utangalizi wa mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza level ya kwanza kwa lugha ya kiswahili. Haapa utapata msingi wa kuweza kutengeneza tovuti na blog. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database MySQL - DATABASE somo la 6
Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database mySQl database somo la 11
huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database. Soma Zaidi...