image

Mafunzo ya php level 1 somo la kwanza (1)

Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi

MAFUNZO YA PHP SOMO LA KWANZA

 

Mahitaji ya course:

  1. Uwe na kompyuta ama smartphone
  2. Uwe na uelewa wa html
  3. Uwe mjanga, wa kuweza kutumia simu ama kompyuta yako vyema
  4. Ujuwe kusoma na kuandika
  5. Kuwa na hamu ya kutaka kujuwa.

 

 

Utangulizi:

PHP ni katika lugha za kikompyuta inayotumika kwenye server. Php hutumika katika kutengeneza kurasa za wavuti kama ilivyo html. Php pia inaweza kutumika katika kutengeneza software. Php ni moja katika lugha zinazotumika sana katika blog kama wordpress na katika social media kama facebook. Php ni free kibiashara na hata binafsi.

 

Php ilianzishwa mwaka 1994 na mmarekani aliyejulikana kwa jina la Rasmus Lerdorf, ikiwa kama home project. Nika katika luga za kikompuata zilizo rahisi kujifunza, hata hivyo syntax yake inaweza kuwa ngumu kuliko javascript na lugha nyingine.

 

PHP ni nini?

Php ni kifupisho cha maneno Hypertext Preprocessor. Php hutengeneza kurasa za wavuti kama html, pia huweza kutumiwa ndani ya html ama html ikatumiwa ndani ya php. Kwa pamoja tukaweza kuhama kutokakurasa kwenda kurasa ndio maana php ikawa nayo ipo katika hypertext kama ilivyo html. Tofauti ni kuwa php kwanza code hufanyiwa processing kwenye server, kisha ndipo server hutuma matokeo kwenye browser kama html code ama plain text kwa maana hii ndipo tunapata preprocessor kwa maana kwana code zinachakatwa kwenye server kisha matokeo ndipo hutolewa kama html ama plain text kwenye browser.

 

NINI PHP HUFANYA:

  1. Hutengeneza dynamic web page
  2. Hutengeneza static webpage
  3. Huwengeneza web App

 

Kwa ufupi php ina uweza kufanya mambo haya:-

  1. Inaweza kuedit data kwenye database
  2. Kuongeza na kupunguza data kwenye database
  3. Kujaza fomu za madodoso
  4. Kupokea taarifa kutoka katika madodoso (form)
  5. Kufunga na kufunguwa database
  6. Kufunguwa na kufunga mafaili
  7. Kutengeneza dynamic na static web page
  8. Kutengeneza system za web App

 

PHP inafanyaje kazi?

Kwanza browser inapokutana na code za php, code hizi hutumwa kwenda kwenye server. Server inachakata code za php na kurudisha matokeo kwenye browser kama plain text, na hapo html huchukuwa nafasi yake, hatimaye maudhui yanaonekana kwenye browser kama html.

 

Server ni nini?

Server ni kompyuta inayohudumia kompyuta nyingine. Zipo kompyuta maalumu zinafanya kazi ya kuhudumia kompyuta nyingine, lakini kompyuta yako mwenyewe pia unaweza kuifanya iwe server na kuhudumia kompyuta nyingine. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia sikuhisi hata simu inaweza kuwa server na kuhudumia kompyuta.

 

Browseer yako kama chrome, firefox na opera zinaelewa html, javascript, xml, css lakini haziwezi kuelewa php. Hivyo ili code za php uweze kuzirun kwenye browser ni lazima uwe na server ambayo inachakata php na kurudisha majibu kama plain text.

 

KUIANDAA SIMU NA KOMPYUTA YAKO KUTUMIA  PHP

Kama nilivyokueleza kuwa php inahitaji server. Hivyo unatakiwa uwe na App ambazo zitaweza kufanya simu yako iwe localhost server. Fuata hatuwa zifuatazo:-

  1. Katika simu yako tengeneza folder liite website
  2. Download App hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sylkat.apache kama unatumia simu ama download xamp au wampserver kama unatumia kompyuta.
  3. Download App hii kama unatumia simu https://play.google.com/store/apps/details?id=com.rhmsoft.code ama kama unatumia kompyuta unaweza kutumia notepad, ama sublime text, au notepadplus.
  4. Funguwa App hiyo hapo juu kama unatumia simu, kisha pest code hizo hapo chini.

 

<?php

print “hello my php”;

?>

  1. Kishha sevu, utaona kialama cha kusevu chini. Utaletewa kuchakuwa folda la kusevu. Hapo chaguwa lile folda uliolitengeneza. Wekajina kisha weka .kisha wepa php. Mfano index.php.

 

  1. Baada ya kusevu chini utaona kibatani cha kuplay. Bofya hicho kurun code zako hapo maneno haya yatatokea “hello my php”

 

  1. Hapo utakuwa tayari kwa somo.

 

KWA WATUMIAJI WA KOMPYUTA:

  1. Kama umedownload xamp ingia kwenye folda lililoandika htdocs, hapo tengeneza folda lingine liite website.
  2. Kwa waliodownload wampserver tafuta folda lililoandikwa www ingia hapo kisha tengeneza folda lingine liite website
  3. Funguwa notepad kisha pesti code hizi

<?php

print “hello my php”;

?>

 

  1. Sevu kwenye folda la website ulilotengeneza hapo juu. Weka jina kisha weka doti kisha weka php. Mfano index.php
  2. Funguwa browser yako kisha andika localhost kwenye upau wa link.
  3. Utakapofunguka ingia kwenye folder la website kisha bofya faili lako ulilotengeneza kwa code hizo hapo juu. Browser italete matoke kwa text hizi “hello my php
  4. Kama umefika hatuwa hii basi upo tayari kuendelea na somo.

 

Usikose somo lijalo litakalokuja kuangalua zaidi kuhusu php na kanuni zake za kuandika project.

 

Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email:mafunzo@bongoclass.com

Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 994


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Mafunzo ya database MySQL database somo la 9
haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 3 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 3)
Hili n somo la tatu katka muendelezo wa mafunzo ya HTML LEVEL 2 kwa lugha ya kiswahili. Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya bongoclass Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 8
Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

Mafunzo ya html level 2 (html full course for beginners)
haya ni mafunzo ya HTML level 2 kwa wenye kuanza. Mafunzo haya ni muendelezo wa level 1 html. Katika course hii utajifunza mengi zaidi lu;iko level1 pia tutazidi kuboresha project yetu. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 4 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia. Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE MYSQL na SQL somo la 1
Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

Mafunzo ya Database MySQL DATABASE somo la 2
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 1 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 6 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 6)
Katika somo hili la 6 mafunzo ya HTML level 2, tutajfunza namna ya kugawa ukurasa wa wavuti wa html. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database mySQl database somo la 11
huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database. Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la pili (2)
hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php. Soma Zaidi...