NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA

NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA

Darsa za Dua

Ustadh Rajabu

DARSA ZA DUA

Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Mfalme na mmiliki wa ulimwengu na siku ya mwisho. Sala na amani zimuuendee kipenzi cha Allah mtume Muhammad (s.a.w) pamoja na masahaba zake na watu wa familiya yake.


Ama baada ya utangulizi huu, hiki ni kitabu cha dua kilichoandaliwa kwa ajili ya kutoa mafunzo juu ya dua na yanayohusiana. Kitabu hiki kimeandaliwa kwa lugha ya kiswahili na iliyo nyepesi zaidi ili kuwezesha wasomaji wapate kuelewa. Maandalizi ya kitabu hiuki yametokana na mafunzo kutoka kwenye quran na sunnah.


Kitabu hiki ni waqfu kwa ajili ya Allah na hakiuzwi. Kwa yeyote atakayetaka kukiprint awasiliane nasi kwa +255675255927 au rajabumahe@gmail.com. Kitabu hiki kimeanza kusambazwa kwa njia ya kimtandao hivyo tunatoa wito kwa anayeteka kukiprint awasiliane nasi kwa haraka zaidi.


Hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo huu wa vitabu vya dua kutoka kwetu. Inshaa Allah tunatarajia kutoa mwendelezo wa kitabu hiki siku za mbeleni. Pia tunatoa wito kwa yeyote mwenye kuweza kuandika vitabu awasiliane nasi lkwa ajili ya mazungumzo zaidi.


Tumeandaa kazi hii kwa ajili ya Allah kwa kutaraji radhi zake na si vinginevyo. Pia tunatarajia dua kutoka kwenu wasomaji ili Allah atusamehe madhambi yetu pamoja na wazazi wetu na waislamu kwa ujumla.


Tunaomba kwa yeyote atakayeona kuna makosa kwenye kitabu hiki awahi haraka sana kuwasiliana nasi ili kuzuia kusambaa kwa makosa zaidi. Kitabu hiki cha kwanza nimekigawa katika sehemu kuu tano kama zitakavyoelezwa chini hapo.


Wabillah tawfiq
Al- ustadhi Rajabu Athuman
+255675255927
rajabumahe@gmail.com





KITABU CHA DUA
Hiki ni kitabu cha dua na ni waqfu kwa ajili ya Allah. Hakiuzwi na na sio ruhusa kukiuza. Kwa anayetaka kukiprint ni bure awasiliane nasi pindi akitaka kufanya hivyo.


Tumeandika kitabu hiki kwa kutarajia radhi za Allah na kutoa mafundisho kwa waislamu na si vinginevyo.


DUA
Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Na dua ni ibada kama ibada nyingine.


Dua ni jambo lenye kupendeza kama walivyosema maulamaa na masalafi wema walotangulia. Umuhimu wa dua na msisitizo wake unapatikana katika quran na sunnah.


Dua zimesisitizwa sana katika quran na sunnah hata mtume akasema ' ' ' ' ' ' ' 'na aombe mmoja wenu haya yake (dua) kwa Allah mpaka chumvi.'. Hivyo si kuomba mambo kakubwa tu na matatizo tulonayo ila mpaka chumvi.


FADHILA ZA DUA
1.Dua ni ibada. Basi utambue ewe ndugu muislamu kuwa dua ni ibada. Imepokewa hadithi kutoka kwa Nuuman Ibn Bashir ' ' kuw Mtume wa Allah ' ' ' amesema "' ' ' 'hakika dua ni ibada' (imepokewa na Tirmidh na ameisahihisha).


2.Dua ndio jambo tukufu zaidi kwa Allah kama Mtume ' ' ' aliposema katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Huraurah ' ' kuwa Mtume amesema 'hakuna kitu kitukufu mbele ya Allah kuliko dua' (imapokewa na tirmidh, imam Ahmad na Alhaakim kwa isnad sahihi) ' ' ' ' ' ' ' ' '


3.Allah anamchukia mtu ambaye hamuombi. Abuu Hurairah ' ' amesema kuwa Mtume ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' '" 'mtu yeyote ambaye hamuombi Allah, Allah humchukia mtu huyo' (amepokea hadithi tirmidh)


4.Allah anapenda kuombwa. Katika masimulizi ya Ibn Mas'ud ' ' Mtume ' ' ' ' amesema 'muombeni Allah katika fadhila zake, hakika Mwenyezimungu Mtukufu (' ') anapenda kuombwa' (amepokea Tirmidh).


5.Dua ni malango wa rehema. Katika masimulizi ya ibn 'Umar ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' 'mwenye kufunguliwa mlango wa dua, hufunguliwa mlango wa rehema.' (amepokea Tirmidh).


6.Dua huondosha mabalaa na majanga. Katika masimulizi ya Ibn 'Umar, ' ' Mtume ' ' ' ' amesema 'hakika dua hunufaisha kwa (hukinga) yale yanayoshuka (yanayotokea), na yale ambayo hayajashuaka ( hayajatokea). Basi jilazimisheni na (kuomba) dua enyi waja wa Allah.


ADABU ZA KUOMBA DUA.
1.kuelekea qibla. Amesimulia Abdallah Ibn Zayd ' ' kuwa 'alitoka Mtume ' ' ' ' kwenda kuomba dua ya mvua akaelekea kibla'. (amepokea Bukhari).


2.Kunyanyua mikono miwili juu. Amesimulia Abuu Musa ' ' kuwa 'aliomba Mtume ' ' ' ' dua akanyanyua mikono yake mpaka nikaona weupe wa kwapa lake' (amepokea Bukhari). Na amesimulia Ibn 'Abas kuwa Mtume ' ' ' ' amesema ' "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' 'muombeni Allah kwa matumbo ya viganya vyenu, wala msimuombe kwa migongo ya viganja vyenu.'. (amepokea Abuu Daud na Bayhaqiy).


3.Kuanza dua kwa kwa kumsifu Allah na kumshukuru (kama kusema alhamdu lillah '.) na kumswalia Mtume ' ' ' '. Amesimulia 'Abdullah Ibn Mas'ud ' ' kuwa nilikuwa nikiswali, wakati Mtume yupo na Abuubakar na 'Umar, basi nilipokaa nikaanza kumshukuru Allah na kumsifu na nikamswalia Mtume ' ' ' ' kisha nikajiombea dua, akasema mtume ' ' ' ' 'omba utapewa, omba utapewa'. (amepokea tirmidh kwa isnad sahih). Na katika masimulizi ya Fudailah Ibn 'Ubayd ' ' amesema 'hakika amefundisha mtume ' ' ' ' uma wake jinsi ya kuomba dua akasema 'pindi anapoomba dua mmoja wenu basi aanze na tahmid (kumshukuru Allah) na thanaai (kumsifu Allah) kisha amswalie Mtume ' ' ' ' kisha aombe chochote anachotaka' '"' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' (amepokea Abuu Daud, tirmidh, Ibn Hiban na baihaqy).


4.Kuanza kuomba dua kwa kujiombea mwenyewe. Kwa anayetaka kumuombea mtu mwingine dua anatakiwa aanze na kujiombea mwenyewe. Amesimulia Ubaiya Ibn K'ab ' ' kuwa ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' 'alikuwa mtume ' ' ' ' anapomkumbuka mtu na akataka kumuombea dua huanza kwa kujiombea mwenyewe kwanza.' (amepokea tirmidh kwa isnad sahih).


5.Kurudia rudia katika kuomba na kusisitiza maombi yako. Ila usiharakishe majibu kutaka kujibiwa haraka hata ukawa unamlaumu Allah. Amesimulia Abdallah ibn Ms'ud ' ' kuwa alikuwa Mtume ' ' ' ' anapenda kuomba mara tatutatu na (akawa) anaomba istighfar (msamaha) mara tatutatu. (amepokea Abu Daud kwa isnad salih).


6.Kuwa na yaqini juu ya kujibiwa na kujiepusha na yaliyo haramu. Mtu anatakiwa asiwe na shaka juu ya kujibiwa dua yake. Amesimulia Abuu Hurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' 'muombeni Allah mkiwa na yakini juu ya kujibiwa na jueni kuwa Allah hakubali dua ya mtu ambaye moyo wake umeghafilika naye. (amepokea Tirmidh na Alhaakim).


7.Usiharakishe kujibiwa. Isitokee mtu akawa na haraka ya kutaka maombi yake yajibiwe kama anavyotaka yeye kwa haraka hata akawa analaumu. Amesemulia Abuuhurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '" 'atajibiwa (dua yake ) mmoja wenu maadam hajaharakisha (kujibiwa) akawa anasema nimeomba na wala sijajibiwa'. (amepokea Bukhari na Muslim). Na katika masimulizi mengine ya Abuuhrairah kuwa mtume amesema 'hataacha mja kujibiwa dua yake maadam hajaomba madhamdhi au kukata udugu'. (amepokea Muslim na Abuu Daud). Hii ina maana dua itajibiwa tu ila isiwe ya kuomba madhambi au kukata udugu.


8.Kuitikia 'aamiin'. Mwenye kuomba dua basi aitikie 'aamiin' eidha awe mwenyewe pekee au yupo na kundi la watu. Amesimulia Abuuhurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' 'atakapoomba dua mmoja wenu basi na aitikie 'aamiin' mwenyewe'. (amepokea Ibn 'Adiy).


MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.
1.kuchunga adabu za dua kama zilivyotajwa hapo juu.


2.Kuwa twahara nje na ndani. Yaani kujiepusha na mambo maovu na machafu ya siri na yasiyo ya siri. Amesema Mtume ' ' ' ' 'hakika Allah ni mzuri na anapenda (vitu) vizuri.'. (amepekea Bukhari na Muslim) Hivyo mtu anatakiwa ahakikishe ni mzuri ndani na nje.


3.kujiweka mbali na yaliyo haramu yote, na kujiepusha kula na kunywa bya haramu au kuvaa vilivyo haramu. Amesema Mtume ' ' ' ' 'ukitaka dua maombi yako basi kifanye kizuri chakula chako (kisiwe cha haramu) ' (amepekea Bukhari na Muslim). Na pia katika hadithi ndefu iliyo sahihi katika kuwa mtume anashangaa mtu ambaye chakula chake haramu, kinywaji chake haramu, a mavazi yake haramu. Isitoshe mtu huyu amechafuka na manywele yapo timtim. Vipi atajibiwa dua yake mtu huyu. (amepekea Bukhari na Muslim).


4.Kuzingatia nyakati ambazo dua hujibiwa. Tutaziona hapo mbele.


5.Sifa ya dua yenyewe. Tutaona dua zenye sifa ya kujibiwa.


6.Hali inayozunguruka dua. Tutaona hali ambazo dua hujibiwa.


NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '" 'anashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema 'nani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsamehe'. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).


2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' ' ' ' ' ' ' '"' Amesimulia Abuu Umama ' ' kuwa aliulizwa Mtume ' ' ' ' 'dua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema:) usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhi'. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).


3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema 'hairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqama'. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).


4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema 'muda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).


5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema: 'hufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkaba'. (amepokea Tabrany).


6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-'asr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ungeupata.


HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
1.Dua ya kumuombea aliye mbali. Chukulia mfano una ndugu yako yupo nchi nyingine ama mji mwingine kisha ukamkumbuka na ukataka kumuombea dua, basi dua hii itajibiwa tu. Mtume ' ' ' ' amesema 'hakika dua iliyo nyepesi (na haraka ) kujibiwa ni dua ya mtu kumuombea aliye mbali' (amepokea Abuu Daud na Tirmidh kwa isnad sahihi). Pia amesimulia Abuu Dardaa ' ' kuwa mtume ' ' ' ' amesema 'dua ya mtu muislamu ni yenye kujibiwa anapomuombea ndugu yake aliye mbali. Juu ya kichwa chake kuna Malaika anaitikia 'aamiin' na wewe upate mfano wa wake'. (amepokea Ahmd na Muslim).


2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa. Hali za watu watatu hawa wakiomba dua Allah atajibu dua zao bila ya shaka. Mtume ' ' ' ' amesema ' "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '


3.'dua za watu watatu (hawa) ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa'. (amepokea Abuu Daud, Ahmad na Tirmidh kwa sanad sahihi).


4.Dua ya mwenye swaum (funga), imamu muadilifu, na mwenye kudhulumiwa. Watu hawa dua zao zitajibiwa tu, kingozi muadilifu, mtu aliyekuwa kwenye funga na kabla hajafuturu na mtu aliyedhulumiwa. Amesema Mtume ' ' ' ' watu watatu dua zao hazirudi: mwenye funga mpaka afutauru, imamu muadilifu (kiongozi muadilifu), na mwenye kudhulumiwa.'.' (amepokea tirmidh kwa isnad sahihi).


SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.
Hapa tutaona dua iliyo katika sura ambayo Allah ataijibu. Dua zenye kujibia wakati mwingine zina sura yake na sifa zake katika maneno na matamshi. Hebu tuone sifa hizo.


1.Dua ya nabii Yunusi. Mwenye kuomba dua na akatumia maneno aliyoyasema nabii Yunusi (amani ishuke juu yake) dua hii ni yenye kujibiwa. Amesema mtume ' ' ' ' 'dua ya nabii Yunus pindi alipokuwa kwenye tumbo la samaki (aliseme) 'LAA LILAAHA ILLAA ANTA, SUBHAANAKA INII KUNTU MINADHWALIMIINA' hakika hataomba mtu muislamu dua kwa kutumia maneno haya kitu chochote isipokuwa atajibiwa na Allah'. (amepokea tirmidh).


2.Kuomba dua kwa kutumia jina la Allah lililo kubwa. Allah ana majina mengi na mazuri. Lakini katika majina hayo lipo ambalo ni kubwa na ukiomba dua kwalo lakina utajibiwa. Kwa ufupi ni kuwa jina hili limefichwa na hakina yeyote anayelijuwa. Ila mtume ametowa ishara ya kuonesha wapi linapatikana na maneno gani mtu atumie kulipata jina hilo.


Amesema mtume ' ' ' ' 'jina kubwa la Allah lipo kwenye aya sita za mwisho za surat hashri. (amepokea Dilamy kutoka kwa Ibn 'Abas). Pia katika mapokezi mengine ya Tabrany kutoka kwa Ibn 'Abas kuwa mtume amesema jina kubwa lipo kwenye aya ya 20 ya surat al-imran. Na pia zipo hadithi nyingi sana zinazoashiri wapi jina hilo lipo. Nitaleta chache tuu.


i) Aisha ' ' aliomba dua hii ' ALLAHUMMA INII AD'UKA LLAHA WA-AD'UKAR-RAHMANA, WA-AD'UKAL-BARRAR-RAHIIMA, WA-AD'UKA BIASMAAIKAL-HUSNAA KULLIHAA MAA 'ALIMTU WAMAA LAM A'ALAM AN TAGHFIRA LII WATARHAMNII' Mtume akacheka kisha akasema 'hakika jina kubwa lipo ndani ya dua hii. (amepokea Ibn Maajah kutoka kwa 'Aisha) hadithi hii ni ndefu nimeikatisha na kuchukua hiyo dyua tu. ii)hadithi ya Anas' 'kuwa' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '.' ' ' ' ' ' ' ' "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"amesimulia Anas ' ' kuwa alikuwa amekaa na mtume ' ' ' ' wamekaa msikitini na kulikuwa na mtu mmoja anaswali kisha akaomba dua kwa kusema ' ALLAHUMMA ANNII AS-ALUKA BIANNALAKAL-HAMDA, LAA ILAAHA ILLA ANTAL-MANNAANU BADI'US-SAMAAWATI WAL-ARDH YAA DHALJALALI WAL-IKRAM YAA HAYYU YAA QAYYUUM' akasema Mtume ' ' ' ' umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo anapoombwa kwalo atajibu'. (amepokea tirmidh kwa isnad gharib).


iii)amesimulia Abdillah Ibn Buraydah ' ' kutoka kwa baba yake kuwa Mtume ' ' ' ' alimsikia mtu mmoja akisema 'ALLAHUMMA INNIASALUKA BIAN-ASHHADU ANNAKA ANTALLAHU LAA ILAAHA ILLA ANTA. AL-AHADUS-SWAMADUL-LADHII LAMYALID WALAM YUULAD, WALAM YAKUN LAHU KUFWAN AHAD' akasema Mtume ' ' ' ' hakika umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo akiombwa hutoa na akiombwa dua hujibu. (amesimulia Abuu Daud,tirmidh,Ibn Maajah na Ibn Hiban).


Iv). Mtume amesema ' ' ' ' ' ' '{' ' ' ' ' ' ' ' '}' ' ' ' ' '"'Jina kubwa la Allah linapatikana kwenye aya hizi' waillahukum ilahu wahidu laa ilaaha illa huwar-rahmanir-rahiim' na mwanzoni mwa surat al 'Imran


3.dua ya Mtume ' ' ' ' ni yenye kujibiwa. "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' Katika hadithisahihi mtume amesema Nabii yeyote ameomba dua yake na akajibiwa. Na nikaifanya dua yangu mimi ni shifaa kwa umati wangu sikku ya qiama. (amepokea Bukhari, Muslim na tirmidh kutoka kwa Anas).


4.Dua wakati wa raha hujibiwa wakati wa shida. Hii ni sifa ya dua yenye kujibiwa mbayo watu wengi hatujui. Nikuwa pindi unapopata neema na raha hapo ndipo pa kumuomba Allah na Allah atakujibu wakati unapopata matatizo kwa kukufariji na kukuondlea matatizo. Amesimulia Abuuhurairah ' ' kuwa mtume ' ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '" ' 'mwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa raha'. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib).


Na katika mapokezi mengine amesema Mtume ' ' ' ' "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '" 'Mwenye kupenda kujibiwa dua zake wakati wa shida na taabu basi na azidishe dua wakati wa raha' (amepokea tirmidh)


KUKUSANYIKA KATIKA DUA.
Ni jambo la kupendeza kuomba dua mkiwa kwenye kundi. Zipo dua ambazo siku zote zinaombwa watu wakikusanyika kama dua ya kuomba mvua. Kukusanyika kwenye dua ni sunnah katika sunnah zingine.


Ijulikane kuwa pindi mtu akiomba dua kisha wengine wakaitikia aamiin huenda katika waloitikia akawepo walii wa Allah ambae ikawa sababu ya dua kujibiwa. Pia watu waliokuwepo kwenye kundi aombe mmoja na wengine waitikie aamiin na wanyanyue mikono yao.


Maswahaba Allah awaridhie walikiwa wakiombeana dua na walikuwa pia wakikusanyika kayika kuomba dua. Mtume ' ' ' ' alikuwa pia akiwahimiza maswahaba wake kuwa katika kundi wanapoomba dua na wengine waitikie aamiin. Amesimulia Habiib Ibn Salamah ' ' kuwa mtume ' ' ' ' amesema 'halikusanyiki kundi la watu na wakaomba dua wengine na wengine wakaitikia 'aamiin' isipokuwa Allah ataijibu dua hiyo'. (amepokea tbrany, Bayhaqy na Alhaakim).


NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA.
Itambulike kuwa dua ambayo imefata vigezo na masharti ya dua itajibiwa tu. Ila pia itambulike kuwa dua hujibiwa katika njia kuu tatu ambazo ni kupewa alichoomba, kufutiwa madhambi au kulipwa siku ya qiama kwa kuingizwa peponi. Hivyo itambuluke kuwa mtu anaweza kuomba dua kisha asijibiwe huenda Allah anataka kumpa kheri zaidi au huenda ameshamjibu kwa kumfutia madhambi yake. Allah ndiye anaejua lile ambalo ni bora kwa wajawake katika wakati wowote ule.


Amesimulia Abuuhurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' ' 'mtu yeyote anaeomba dua ila atajibiwa ima awahishiwe kujibiwa haphapa duniani, au acheleweshewe (kujibiwa hapa duniani na badala yake ) ajibiwe akhera au asamehewe madhambi yake kwa kiasi kile alichoomba, maadam hajaomba (jambo la) madhambi au kukata udugu aua hajafanya haraka ya kutaka kujibiwa hata akawa anasema 'nimemuomba Mola wangu na hakunijibu'. (amepokea tirmidh).
Pata kitabu Chetu Bofya hapa

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 816

Post zifazofanana:-

Kuwashwa pumbu ni dalili ya fangasi?
Habari. Soma Zaidi...

binadam akiwa mweupe mikononi atakuwa na upungufu wa vitamin gani?
Natak kufaham kuwa binadam akiwa mweupe mikononi atakuwa na upungufu wa vitamin gani? Soma Zaidi...

HADITHI YA KILEWA WA VIUNGO
HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Soma Zaidi...

MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)
Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Soma Zaidi...

Si Yesu Aliyesulubiwa (yesu hakufa msalabani wala hakusulubiwa
Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

lengo la kuswali za faradhi na suna
Soma Zaidi...

SCIENTIFIC PROCESSES IN BIOLOGY
SCIENTIFIC PROCESSES IN BIOLOGYY THE USE OF SENSE ORGANS TO MAKE CORRECT OBSERVATION Sense organ this is an organ of the body that responds to external stimuli by conveying impulses to the sensory nervous system. Soma Zaidi...

JARIBU LA PILI LA ALADINI
Soma Zaidi...

Dawa ya kiungulia na njia za kuzuia kiungulia
utajifunza njia za kuzuia kiungulia, dalili za kiungulia na dawa ya kutibu kiungulia. Soma Zaidi...

Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo kitomvuni, sababu zake na dalili zake
Hapa utajifunza sababu za kuwepo na maumovu ya tumbe kitomvuni. Soma Zaidi...

Subscribe
Ingiza taarifa zako hapo chini uweze kupata Update zetu. Soma Zaidi...