image

FANGASI NA MADHARA YAO KIAFYA: FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI NA NYAYONI

FANGASI NA MADHARA YAO KIAFYA: FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI NA NYAYONI

Maradhi 7 ya Mbu

by Rajabu Athuman

MAGONJWA 13 YAENEZWAYO NA MBU

FANGASI
Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi ni hatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakili kama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathiri mwili wa binadamu.


Wapo fangasi ambao wanaonekana kwa macho na wengine hawawezi kuonekana. Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina za fangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Miongoni mwa maradhi yanayoweza kusababishwa na fangasi ni pamoja nna:
1.Aleji
2.Mapele na maruturutu kwenye ngozi na vidole
3.Maambukizi ya mapafu kama pneumonia ambayo hufanana na mafua au kifua kikuu
4.Maambukizi kwenye mfumo wa damu
5.Kupata ugonjwa wa meningitis huu ni ugonjwa unaoathiri ubongo pamoja na ugwe mgongo.


MAENEO AMBAYO FANGASI WANAISHI
Fangasi huweza kuishi kwenye maeneo mengi kama
1.Kwenye udongo
2.Hewa
3.Kwenye mimea
4.Kwenye ngozi za watu
5.Na ndani ya miili ya watu


AINA ZA FANGASI
Fangasi wamegawanyika katika makundi mengi. Na wamekuwa wakisababisha maradhi mblimbali na katika sehemu mbalimbali za miili yetu. Hapa nitakutajia aina za fangasi hawa kama ifuatavyo:-


1.Fangasi wa kwenye kucha.
Hawa ni fangasi ambao wanashambulia sana kwenye kucha za vidole vya mikonobna miguu. Jina la kitaalamu la fangasi hawa ni onychomycosis. Wanakifanya kidole kivimbe, na kupoteza rangi yake ya asili. Kidole kinaweza kuwa na mipasuko. Fangasi hawa wanaathiri zaidi kwenye vidole vya miguu kuliko vya mikono. Fangasi hawa hawana maumivu lamda kama wataathiri zaidi.



Dalili za fangasi hawa:-
?Kucha kuwa na utandu mweupe au njano
?Kidole kuwa kigumu na kuvimba
?Kupasuka kwa vidole


Fangasi hawa tunaweza kuwapata kwenye mazingira yetu, wanaingia kupitia mipasuko kwenye miguu ama kwa namna nyingine. Kila mtu anaweza kupata fangasi hawa ila kuna watu wapo hatarini sana yaani ni rahisi kupata fangasi hawa.


Watu walio hatari kupata fangasi hawa
Watu hawa ni kama:-
?Mtu mwenye majeraha kwenye kucha ama aliyefanyiwa upasuaji
?Watu wenye kisukari
?Watu wenye mfumo wa kinga ulio dhaifu
?Watu wenye matatizo katika mfumo wa damu
?Watu wenye minyoo kwenye miguu.


Njia za kuepuka fangasi hawa:
1.Weka vidole vyako safi na vikavu muda wote
2.Kata kucha zako ziwe fupi na usiweke safi muda wote
3.Usitembee bila ya viatu kwenye maeneo yasiyo salama.
4.Usishiriki kifaa cha kukatia kucha na watu wengine


2.Fangasi wa mapunye;
Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni. Kitaalamu fangasi hawa hujulikana kama tinea” au “dermatophytosis. Na kwa maarufu sana wanafahamika kama ringworm kwa kuwa wanatoa mabako ya mduara kwenye ngozi.


Fangasi hawa wanaweza kukaa kwenye ngozi, kuta, nguo, taulo na maeneo mengine. Miongoni mwa dalili zao ni kuona maduara kwenye ngozi, mara nyingi dalili za fangasi hawa huweza kuonekana kuanzia siku 4 mpaka 14 baada ya ngozi kupata maambukizi ya fangasi hawa. zifuatazo ni katika dalili za fangasi hawa:-
?Kuwasha kwa ngozi na maumivu wakati mwingine
?Kuwepo kwa mapele ama ukurutu uliotengeneza umbo la duara
?Ngoz kuwa nyekundu, kupasuka ama kuwa kavu
?Kukatika ama kunyonyoka kwa nywele kwenye sehemu iliyo athirika


Fangasi hawa wanaweza kukaa katika maeneo mbalimbali ya mwili na kusababisha dalili tofautitofauti kulingana na eneo lililo athirika. Kwa mfano;-


Fangasi hawa wakiwa kwenye nyayo (sthlete’s foot) huweza kuonesha dalili kama nyayo kuwa nyekundu, kuvimba ama kujaa maji, ngoxi kutoka ama kubabuka, kuwasha kwa ngozi katikati ya vidole na kidole na mara nyingi kati ya kidole kidogo na kinachomfatilia. Wakati mwingine kisigino na nyayo huweza kuathirika na kuweka mabumbuza.


Kwenye kichwa, fangasi hawa huweka maduara yaliyo nyonyoka ngozi, yakiwa na ukurutu, ngozi kavu, na kuwasha. Maduara haya maarufu tunayaita mapunye, yanaweza kuwa mengi na kuungana kufanya duara moja kubwa. Mara nyingi sana fangasi wa kichwani huwapata sana watoto kuliko watu wazima.


Kwenye pachipachi za mapaja (jock itch). Fangasi hawa hukaa sehemu ya ndani ya mapaja karibu na sehemu za siri ama kuzungukia eneo hilo, lakini wanashambulia mapaja. Miongoni mwa dalili zao ni mapaja kufanya wekundu, kuwasha na hali inaweza kuwa mbaya mpaka ngozi ikababuka na hatimaye kufanya vidonda kwa kujikuna. Wanaweza kushambulia pia korodani na kufanya ibabuke, iwe nyekundu na kuweka vidonda.


Fangasi wa kwenye ndevu (tinea barbae). fangasi hawa wanashambulia maeneo ambayo ndevu zinapatikana kama kwenye kidevu na shavu. Dalili zao ni kuwasha kwa kidevu, shavu, na sehemu ya juu ya shingo. Fangasi hawa wanaweza kuwa hatari zaidi na kusababisha mapele yenye usaha kwenye eneo hili.


Huweza kuwapata wenye ndevu ama ambao wananyoa ndevu. Dalilizao ni kama za fangasi wa maeneo mengine, kama eneo kuwa jekundu, kuwasha kuwa na madoamadoa na kunyonyoka kwa ndevu katika eneo lililo athirika.


Walio hatarini zaidi kupata fangasi hawa
Watu wote wanaweza kupata fangasi hawa wa mapunye. Lakini kuna watu wengine wapo hatarini zaidi. Na hii ni kutokana na shughuli zao wanazofanya, mazingira wanayoishi ama staili za maisha yao.
?Watu wenye mfumo wa kinga dhaifu
?Watu wanotumia changia sehemu moja ya kuwekea nguo
?Watu wanaofanya shughuli ambazo hugusana gusana kwa mfano wanaofanya miereka.
?Watu wanaovaa nguo za kubana sana
?Watu wanaogusana gusana na wanyama wenye mapunye.


Namna ya kujilinda na mapunye
1.Weka ngozi yako katika hali ya usafi
2.Vaa viatu ambavyo vinaruhusu hewa kupita kwenye nyayo zako
3.Usitembee miguu peku hasa kwenye maeneo yenye watu wengi
4.Kata kucha zako ziwe fupi na ziweke katika hali ya usafi
5.Badilisha soksi zako na nguo za ndani (chipi, boksa n.k) japo mara moja kwa siku
6.Usichangie nguo zako na mtu mwingine
7.Kama uanfanya kazi inayohitaji kugusana gusana kwa ngozi hakikisha unaoga mara kwa mara kwa siku.


3.Fangasi aina ya Candidiasis
Huu ni ugonjwa wa fangasi wanaosababishwa na mashambulizi ya fangani aia ya yeast waitwao candida. Miongoni mwa fangasi maarufu sana katika kudi hili ni wale wanaoitwa candida albican. Fangasi hawa wanaishi juu ya ngozi, na ndani ya mwili katika maeneo kama mdomo, koo, tumbo, na katika uke. Wanaeza kuishi maeneo haya bila ya kusababisha madhara yeyote.


Candida wanaweza kusababisha madhara endapo tu watakuwa wengi sana tofauti na kawaida, ama kama wakiingia ndani zaidi kama kweny mfumo wa damu, ama kwenye organ za ndani kama figo, moyo ama ubongo. Na wapo baadhi ya fangasi hawa ni sugu sana kwa madawa.


Fangasi hawa ambao hupatikana kwenye mdomo kitaalamu hufahamika kama thrush au oropharyngeal candidiasis. Na wale ambao hukaa ukeni hutambulika kama yeast infection. Pindi wakiingia kwenye mfumo wa damu ama wakiathiri organ za ndani kama figo, koyo na ubongo hutambulika kama invasive candidiasis.


1.Fangasi hawa wa kwenye mdomo watambulikao kama thrush ama oropharyngeal candidiasis wanaweza kuishi kwenye koo na tundu zima la koo kuelekea kwenye tumbo na hawa wanajulikana kama esophageal candidiasis ama candida esophagitis. Fangasi hawa ni maarufu sana kwa watu wanaoishi na HIV ana UKIMWI.


Dalili za fangasi hawa
?Kuwa na madoa meupe kwenye sehemu ya ndani ya shavu, ulimi, sehemu ya juu ya mdomo, na koo.
?Unahisi kama kuna pambai kwenye mdomo
?Kupetea kwa ladha ya unachokila
?Maumivu wakati wa kula ama kumeza
?Kupasuka na kuwa wekundu kwenye kona za mdomo


Walio hatarini kupata fangasi hawa:
Fangasi hawa si kawaida sana kuwapata watu wenye afya madhubuti. Ijapokuwa wapo watu ambao wapo hatarini sana kupata fangasi hawa kama watoto chini ya umri wa mwaka mmoja, na watu wenye matatizo ya kiafya kam wenye:-
?Watu wanaotumia meno bandia
?Watu wenye kisukari
?Watu wenye saratani
?Watu wenye HIV ama UKIMWI
?Watu wanaotumia dawa amazo zinakausha mdomo
?Watu wanaovuta sigara.
?Watu wanaotumia dawa za kupulizia za pumu


Njia ya kupambana na fangasi hawa:
Wengi wanaopata fangasi hawa ni wale ambao mfumo wao wa kinga umeathirika hivyo miili yao haiwezi kupambana vyema na mashambulizi. Hivyo kupambana na fangasi hawa hakikisha unaweka mwili wako katika hali njema ya kiafya. Muone daktari akuelekeze namna ya kuboresha afya yako. Pia piga mswaki kila unapotumia dawa ya kupulizia ya pumu. Wacha kuvuta sigara.


2.Fangasi wa kwenye uke.
Fangasi hawa kitaalamu wanafahamika kama vagina yeast infection na majina mengine ya kitaalamu ni kama vagina candidiasis, u vulvovaginal candidiasis au candidal vaginitis. Majina yete haya yanalenga vagina yaani uke.


Dalili za fangasi hawa wa ukeni
?Uke kuwasha na kuweka kama makovu
?Maumivu wakati wa tendo la ndoa
?Paumivu wakati wa kukojoa
?Kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida kwenye uke.


Wakati mwingine fangasi hawa wa kwenye uke wanakuwa hatari sana na kusababisha mipasuko kwenye ukuta wa uke, kuvimba na kuwa kwekundu. Hali hizi humfanya mwanamke kukosa hali ya kujiamini.





Walio hatarini zaidi
Fangasi hawa ni kawaida lakini kuna watu ambao wapo hatarini zaidi kupata fangasi hawa. Tafiti nyingi bado zinafanyika kuweza kugundua kwa nini watu flani wapo hatarini zaidi kuapa fangasi hawa. Watu hawa ni:-
?Wajawazito
?Wanaotumia njia za uzazi wa mpango za homoni
?Watu wenye kisukari
?Watu wenye mfumo dhaifu wa kinga kama wenye HIV
?Wtu wanaotumia antibiotics


Kupambana na fangasi hawa
1.Vaa nguo za ndani zinazotokana na pamba
2.Usivae nguo za kubana
3.Vaa nguo zilizo kavu
4.Zungumza na daktari kuhusu matumizi ya antibiotics kama zinakuletea madhara


3.Fangasi watambulikao kama invasive candidiasis.
Hawa huweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kuenda maeneo mengine nyeti sana ya mwili. Kwa mfano kwenye figo, moyo na ubongo machi, mifupa na viungia. Fangasi hawa wakiingia maeneo haya wanakuwa ni hatari sana kwa afya ha mtu.


Dalili za invasive candidiasis
Watu wenye fangasi hawa wanaonesha dalili ambao ni za maradhi mengine, hivyo kufanya vigumu kugundulika. Ijapokuwa kuna dalili ambazo ni za kawaida kama vile, kuhisi baridi, homa ambapo mgonjwa hawezi pata nafuu hata akitumia dawa.


Watu walio hatarini
?Watu ambao wapo ICU kwa muda mrefu
?Watu wenye mfumo dhaifu wa kinga
?Watu waliofanyiwa upasuaji haswa haswa uliohusisha tumbo
?Watu ambao wametumia antibiotics kwa wingi hivi karibuni
?Watu waliotumia chakula kwa kutumia mirija
?Watu wenye matatizo kwenye figo au hemodialysis
?Watu wenye kisukari


5.Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis. Fangasi hawa wanaishi kwenye mazingira yenye majimaji haswahaswa kwenye udongo ama kwenye maozea kama ya miti au majani. Fangasi hawa tunaweza kuwapata kwa kuvuta hewa ambayo imekusanya fangasi hawa.


Dalili za fangasibhawa:-
1.Homa na maumivu vya kichwa
2.Kukohoa
3.Kutokwa na jasho usiku
4.Maumivu ya mivuli na viungio
5.Kupoteza uzito
6.Maumivu ya kifua
7.Uchovu wa hali ya juu sana


Kwa ufupi zipo aina nyingi sana za fangasi, na yapo maradhi mengi sana yasababishwayo na fangasi. Nadhani hapo juu nimekutajia aina maarufu za mangasi ana mago njwa yako. Pia nimekutajia baadhi ya njia za kutumia ili kupambana na fangasi hoa. Sasa nakwenda kukuorodheshea maradhi 7 yatokanayo na fangasi:-


MARADHI YATOKANAYO NA FANGASI
1.Ugonjwa uitwa Mycoses:
2.Ugonjwa uitwa Mycotoxicoses
3.Ugonjwa uitwa Candidiasis: ugonjwa huu umegawanyika kama:-
?Candidiasis ya mdomoni Ooral Candidiasis)
?Candidiadis ya kwenye tundu la hewa kuelekea kwenye mapafy (Bronchocandidiasis au Bronchomoniasis)
?Candidiasis ya kwenye mapafu (pulmonary Candidiasis)
?Endocarditis
?Meningitis
4.Ugonjwa wa actinomycosis
5.Ugonjwa wa Aspergillosis
6.Ugonjwa uitwa Otomycosis (fangasi wa kwenye sikio)
7.Ugonjwa uitwa peniciliinosis


MATIBABU YA FANGASI
Karibia fangasi wote hawa wanatibika bila ya ugumu wowote maka mgonjwa atakamilisha dozi. Zipo dawa za kupaka kama losheni, dawa za kunywa za vidonge. Pia zipo dawa za kupewa kwa njia ya sindano. Muone sasa daktari kama una tatizo, kwa hakika utapona kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.


Dozi hizi pia zinaweza kuchukuwa muda mpaka miezi mitatu kulingana na ukubwa wa tatizo. Hata ukijihisi umepona hakikisha unamaliza dozi. Hakikisha pia unajiweka katika afya njema muda wowote na usafi wamavazi, malazi na mwili.


FANGASI SEHEMU ZA SIRI
Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi ni hatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakili kama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathiri mwili wa binadamu.


Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina za fangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Fangasi wanaweza kuathiri makwapa, vidole, sehemu za siri kwenye tumbo na maeneo mengine.


Fangasi wa sehemu za siri husababishwa na fangasi waitwao candida. Hawa wanaweza kuathiri sehemu za siri kuzungukia uume ama uke. Kunatafiti zinaonesha kuwa fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi. Japo tafiti zaidi zinahitajika ili kuthibitisha hili.


FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI DALILI ZAO KWA WANAUME
1.Kuvimba kwa kichwa cha uume
2.Kuwasha kwa sehemu za siri, hususan kichwa cha uume
3.Uume kuwa mwekundu kwa kuchubuka ama kuvumba ama kwa mashambulizi ya fangasi hawa.
4.Kuota kwa mapele na maruturutu kwenye uume
5.Kuwasha uume ama kuungua moto kwa uume.
6.Kutokwa na majimaji meupe kwenye uume, majimaji haya huwa na harufu mbaya.
7.Maumivu wakati wa kukojoa na kufanya tendo la ndoa.


DALILI ZA FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE
1.Maumivu na miwasho kwenye mashavu ya uke na sehemu ya juu ya uke
2.Maumivu wakati wa kukojoa ama kufanya tendo la ndoa
3.Uuke kuwaka moto kwa ndani
4.Kuvimba kwa mashavu ya uke na kuwa mekundu
5.Kuot mapele na maruturutu kwenye uke
6.Kutokwa na majimaji kwenye uke
7.Kutokwa na majimaji mazito meupe na yenye harufu mbaya kwenye uke.


WATU WALIO HATARINI KUPATA FANGASI HAWA
1.Wachafu
2.Kuwa na mikunjomikunjo kwenye ngozi kama kitambi
3.Wenye kisukari
4.Wenye HIV
5.Wenye saratani
6.Wenye kutumia baadhi ya madawa ya kuzuia mimba
7.Wajawazito


NJIA ZA KUPAMBANA NA FANGASI HAWA
1.Kuwacha kutumia madawa ya kusafishia ama kuunga uke
2.Kutokuvaa nguo mbichi
3.Kutokuvaa nguo za kubana hususani za mpira
4.Kuwa msafi muda wowote
5.Kuosha kichwa cha uume na ngozi ya govi mara kwa mara
6.Kuosha uke mara kwa mara
7.Kutumia pedi zilizo kavua na safi na kubadilisha mara kwa mara



Download kitabu hiki hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1866


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Bawasili usababishwa na nini?
Posti hii inahusu zaidi visababishi vya ugonjwa wa Bawasili,kuna watu wengi wanapenda kujua kabisa chanzo cha kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii na kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu visababishi vya Bawasili. Soma Zaidi...

tatizo la kushindwa kujaza misuli ya mwilini na kusinyaa kwa misuli mwilini
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa kusinyaa kwa Misuli. Ni maradhi yanayopelekea uzalishwaji hafifu wa misuli, hivyo kupelekea misuli kukosa protini, kushunwa kukuwa na kusinyaa. Soma Zaidi...

Dalili za mtu mwenye ugonjwa wa kuishiwa damu
Posti hii inahusu zaidi dalili za mtu mwenye ugonjwa wa kupungukiwadamu, ni dalili zinazoonekana kwa mtu Mwenye tatizo la upungufu wa damu. Soma Zaidi...

Fangasi wanaosababisha mapunye dalili zao na jinsi ya kupambana nao
Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni. Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa uchovu sugu.
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa uchovu sugu ni ugonjwa tata unaoonyeshwa na uchovu mwingi ambao hauwezi kuelezewa na hali yoyote ya matibabu. Uchovu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa shughuli za kimwili au kiakili, lakini haiboresha kwa kupumzika Soma Zaidi...

Minyoo na athari zao kiafya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu minyoo na athari zao kiafya Soma Zaidi...

Athari za ugonjwa wa Dondakoo
Posti hii inahusu zaidi athari za ugonjwa wa Dondakoo,hali hii utokea iwapo ugonjwa haukutibiwa mapema au umetibiwa lakini bado Kuna matokea hasi ambayo yanaweza kujitokeza kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Njia za kupambana na fangasi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na fangasi Soma Zaidi...

Dalili za moyo kutanuka
Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza na kuonyesha kwamba moyo umetanuka. Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa upele
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa upele, ni dalili au mwonekano wa mgonjwa wa upele. Soma Zaidi...

Matibabu ya fangasi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya fangasi Soma Zaidi...

Njia za kuzuia ugonjwa wa kisonono
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo utumiwa Ili kuweza kuzuia kuwepo ugonjwa wa kisonono, kwa kufuata njia hizi ugonjwa huu wa kisonono unaweza kupungua kwa kiasi au kuisha kabisa. Soma Zaidi...