MAGONJWA SUGU
MAGONJWA
Kama tulivyoona huko juu kuwa kuumwa ni hali ya kutokuwa sawa kimwili na kiakili. Sasa katika kurasa hii tutaangalia zaidi kuhusu magonjwa, na namna ambavyo yanaambukizwa na kusababishwa. Pia tutaangalia zaidi namna ambavyo mwili hupambana na magonjwa hayo. Ukurasa huu utakuwa ni mwangaza kwako msomaji wetu juu ya maradhi na yanayohusiana na maradhi hyo. Pia tutaangalia namna ambavyo maradhi huambukizwa katika mazingira na kutoka mtu na mtu mwingine. Tutaangalia kwa undani mawakala wa kueneza maradhi.
Kabla ya kuendelea mbele zaidi ningependa kuwajulisha wasomaji kuwa hapa tutatumia pia maneno ya kitaalamu. Maneno haya nitaanza kuyatolea ufafanuzi wake kabla ya kuendelea mbele. Maneno hayo ni kama haya;-
1.Maradhi ya kuambukiza (infection diseases) haya ni magonjwa ambayo yana sababishwa na mawakala wa maradhi waliovamia mwilini.
2.Pathogen ni mawakala wa maradhi ambao husababisha maradhi mwilini
3.Virusi nivijidudu vidogo sana ambavyo ni wakala wa kusababisha maradhi
4.Fungus ni vijidudu vidogo ambavyo huula miili ya vitu milivyokufa
5.Antibiotic resistance ni hali ambapo mwili unashindwa kabisa kuuwa virusi
MAWAKALA WA MARADHI (PAHOGEN)
Hawa tumesema ndio mawakala wakubwa wa kuambukiza maradhi. Hawa husababisha maradhi haya ya kuambukiza. Wapo aina nyingi lakini tunaweza kuwagawanya katika bakteria, virus, fungi, protozoa na parasites.
1.Bakteria
Hawa ni vijidudu vidogo sana ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho maavu bila ya kutumia hadubini (microscope). Vidudu hivi vina seli moja tu. Wapo bakteria ambao hawasababishi maradhi na wapo a,mbao husababisha maradhi. Bakteria karibia dunia nzima wamejaa na hata sehemu ambazo zana mabarafu bakteria pia wapo. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kuna aina zisizopungua 300 za bakteria ambao wanaishi kwenye mdomo wa binadamu. Ila karibia bakteria hawa wote hawana madhara kwetu kwa upande mwengine wengi wao ni msaada na ni faida kwetu.
Mfano mzuri ni kuwa kwenye utumbo mdogo kuna bakteria ambao wanatengeneza vitamini ambavyo ni msaada kwa afya zetu. Pia ijulikane bakteria wengine wana madhara makubwa wakiwa ndani ya miili yetu kwa mfano baktria aina ya tuberculosis hawa husababisha kifua kikuu. Tetanus hawa huleta tetenasi.
2.VIRUSI
Virusi ni vidogo zaidi kuliko hata bakteria. Virusi ni vijidudu vidogo sana ambavyo vyenyewe vina genetic material na protein coat. Genetic material ni chembechembe zinazowafanya waweze kuzaliana. Virusi vinaweza kushi tu kama vipo ndani ya kiumbe hai. Vyenyewe vinaweza kuzaliana kwa kutumia seli za kiumbe hai ambapowamo. Maradhi ya Ukimwi, mafua ni baadhi tu ya maradhi ya virusi.
3.FUNGI
Hawa huwa tumezoea kuwaita fangasi hawa wanakula kwenye seli za kiumbe hai. Mfano mzuri ni uyoga huu ni katika jamii ya viumbe hawa wanaokula kutokana na seli au kiumbe kilichokufa. Kama bakteria hata wadudu hawa wapo wanasababisha maradhi na wengine hawasababishi. Fangasi wa miguuni ni mfano mzuri wa maradhi ya wasudu hawa. Mfano mwengine ni wale wa sehemu za siri wanaopelekea kuchubua kwa koreodani kwa wanaume na madahra menginey wa wanawake.
4.PROTOZOA
Hawa pia ni vijidudu vidogo visivyoonekana kwa macho makavu. Hawa pia wana seli moja tu katika miili yao. Ila hawa ni wakubwa kuliko bakteia. Hawa wanasababishwa magonjwa ambayo yanaongoza kuuwa watu wengi sana dunianii. Kwa mfano malaria husababishwa na vijidudu hivi. Kwaribia watu milioni moja kila mwaka wanakufa kwa malaria katika nchi zilizopo kwenye uoto wa tropic.
5.PARASIT
5.Hawa ni wadudu wanaokula kiumbe hai. Mfano mzuri ni chawa, kupe, mbu na wengineo wenye mfano huu. Wadudu hawa wanajipatia chakula kwa kunyonyo viinilishe kwenye mwili wa kiumbe hai. Hawa wanaweza kuwa nche ya mwili kama chawa au ndani ya mwili kama minyoo.
NJIA AMBAZO MARADHI HUAMBUKIZWA
1.kutoka mtu kwenda mtu mwingine. Hii ni njia nzuri ya kuambukiza maradhi kutoka mgonjwa kwenda mzima, ama kutoka mtu kwenda mtu. Inaweza kuwa kwa njia ya hewa kama mafua pindi mgonjwa anapopiga chafya, au kifua kikuu pindi mgonjwa napokohoa. Pindi mgonjwa akikohoa au chafya anatowa mamilioni ya wadudu ambao wanabakia hewani kwa muda. Na ikitokea mtu ameivuta hewa ile anaweza kuambukizwa.
Kupitia kugusa maradhi yanaweza kutoka mtu hadi mtu, kwa mfano kitambaa alichotumia mtu mwenye mafua au kifuua kikuu na wewe ukashika unaweza kuwabeba wadudu wale na wakaingia kwako. Pia maradhi kama kipindupindu, homa ya mafua a ndege na ebila huweza kuambukizwa kwa kugusana.
Wakati mwingine kupitia kumkisi mgonjwa unaweza kupata maradhi kwa mfano homa ya ini inaweza kuambukizwa kwa kukisi kupitia mate. Pia kupitia vyombo kama kijiko au kikombe cha kunywea maji kama mgonjwa ametumia na wewe ukatumia palelpale kuweka mdomo wako.
2.kupitia vyakula tumeshaona mifano yake kwenye kurasa zilizopita.
3.Mazigura pia tumeona kurasa za juu
4.Wanyama kwa mfano mbwa kusababisha tetenasi na panya kusababisha ugonjwa wa taun. Hawa wanyama wanakuwa wanabeba pathogen wa maradhi hawa.
NAMNA AMBAVYO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI
Tumeona huko juu kuhusu visababishi vya maradhi na namna ambavyo maradhi yanaweza kusambaa, sasa hapa tutaona namna ambavyo miili yetu unapambana na maradhi haya kwa ajili yetu. Mwili una njia nyingi tuu na namna ya kupambana na maradhi kama utakavyoona hapo chini
1.KA KUTUMIA KUTA ZUIZI (PHYSICAL BARRIERS
Itambulike kuwa ili mtu aumwe ni kwamba wadudu wa maradhi wanatakiwa waingie mwilini. Sasa mwili una vizuizi yaani kuna ukuta maalum ambao unakazi ya kuzuoa wadudu hawa wasipate njia ya kuingia ndani. Vizuizi hivyo ni;-
A).Ngozi:ngozi yenyewe ni ukuta wa kuzuia vijidudu hivi. Ngozi hutumia chemikali kama jasho na mafuta ili kuuwa vijidudu hivi.ngozi inatabia ya kujitibu kwa haraka zaidi kama itapata jeraha ili kuzuia wadudu wasiingie.
B).Utando wa utelezi: huu ni utando maalumu ambao unateleza na kunata. Utando huu unapatika na sehemu nyingi za mwili kama puani kwa ajili ya kunasa mavumbi na vijidudu hawa. Utando huu pia upo machoni kwa ajili ya kunasa vijidudu hivi na kuvitoa nje.
C)Vinyweleo: hivi ni njia nyingine ya kunasa wadudu wowote wanaoraka kuingia ndani. Kwa mfano ndani ya pua kuwa vinyweleo hivi kwa ajili ya kunasa wadudu na mavumbi kuingia ndani.
D)Kemikali: kwa mfano mwili huzalisha asidi ya hydrocloric ambayo husaidia kuuwa bakteria waliopo kwenye vyakula.
2.INFLAMATORY RESPONSE (YAANI KUVIMBA)
Inatokea wadudu hawa wanaingia mwilini kwa mfano mtu anpojikata. Hivyo inflammatory response hali ya mwili kupambana na ma majeraha ambapo sehemu husika huvimba, huwa njeundu na kuwa na maumivu. Kitendo hiki hufanya eneo hili liwe limoto na kusababisha vimishipa vidogo vinavyoleta damu vilete damu kwa wingi na hatimaye seli kutoka kwenye damu hupambana na wadudu walofanikiwa kuingia kwenye eneo lile.
3.IMMUNE SYATEM (MFUMO WA KINGA)
Njia zilizotajwa hapo juu pekee haziwezi kupambana na wadudu hawa. Hivyo kuna mfumo maalumu wa kuukinga mwili dhidi ya majambazi hawa (pathojens) mfumo huu huitwa immune system ambao unatengenezwa na seli hai nyeupe za damu na aina flani ya protin ambayo kitaalamu huitwa antibodies ambazo zipo kwenye mfumo wa lymph (lymphatic system).
Mfumo wa lymph huu umezunguka mwili mzima na unahusika katika kubeba majimaji mwilini. Katika kufanya hivi unafanya kazi ya kuwatowa bakteria na pathogen wengine nje ya mwili. Mfumo huu una seli hai nyeupe nyingi nna hizi ndizo ambazo zinapambana na pathogen na kuwauwa.
Seli nyeupe za damu, kazi yao kuu seli hizi ni kuulinda mwili dhidi ya wavamizi. Kuna aina fani ya seli hizi hutowa kemikali ziitwazo antibodies ambazo huwakamata pathogens na pitowa tahadhari kwa seli nyingine ili wawaue hawa pathogens. Pindi unapoumwa hutokea tezi za lymph zinauma kama mtoki ni kwa sababu seli hizi nyeupe zipo kwa wingi eneo lile kupambana na wadudu hawa.
NAMNA YA KUUSAIDIA MWILI KUPAMABANA NA WADUDU HAWA
1.Jilinde kwa nza mwenyewe kwa mfano usipate majeraha
2.Kula mlo kamili
3.Kunywa maji mengi
4.Punguza mawazo
5.Fanya mazoezi mara kwa mara/,br>
6.Nenda ukachunguze afya yako
7.Jiepushe kuwa karibu zaidi na wenye magonjwa ya kuambukiza hasa kwa njia nya hewa
8.Pata usingizi wa kutosha
BAADHI YA MARADHI YANAYOSABABISHWA NA HALI ZA MAISHA
Hapa tutaangalia kwa ufupi namna a,mbavyo hali zetu za maisha kama tabia na utaratibu ambao tunaishi unavyochangia katika kupata maradhi. Kama ambavyo tumeona huko mwanzo kuwa Afya ya mtu inaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali kama vile tabia ya mtu. Sasa hebu tuone baadhi ya magonjwa yanayohusiana na hali za maisha yaani namna mtu anavyoishi.
1.MAGONJWA YA MOYO:
Moyo unanasibiana na magonjwa mengi sana ambayo wengi hawayajui. Watu wamezoea presha kuwa ndio gonjwa la moyo wanalolijua, ila sio hivyo kuna mengi zaidi. Hali za maisha zinaweza kuwa sababu nzuru ya kupata magonjwa ya moyo, miongoni mwa hali hizo ni kutofanya mazoezi ama vyakula mtu anavyokula
Cardiovascular diseases (CVD) ni maradhi au upungufu flani unaotokea kwenye moyo au mishipa ya damu. Moyo na mishipa ya damu hutengeneza mfumo unaoitwa cardiacvascular system. Hivyo magonjwa yote na matatizo yeyote yanayotokea kwa kuathiri moyo na mishipa ya damu huitwa magonjwa ya cardiacvascular diseases. Tafiti zilizofanywa marekani zinaonesha kuwa maradhi haya ndio yanayochangia vifo vya watu wengi marekani. Miongoni mwa magonjwa haya ni kama shambulio la moyo (heart attact), kupalalaiz (stroke), shinikizo la juu la damu yaani presha ya kupanda na atherosclerosis. Magonjwa haya hushambulia zaidi watu walio na umri zaidi di ya miaka 40. Na maradhi haya yanaweza kutokea tangia utototni.
Unawezakupata maradhi haya kwa kurithi kutoka kwa wazazi, ila inategemea namna unavyoishi ndio tatizo linaweza kuwa kubwa ama dogo. Kwa mfano kuvuta sigara, kuwa na uzito mkubwa, kuwa na kisukari na kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu husababisha tatizo hili kuwa kubwa zaidi. Tafiti zinaonesha karibia milioni 60 marekana wana moja kati ya magonjwa hya na karibia watu milioni moja hufa kwa sababu ya magonjwa haya kila mwaka.
AINA ZA MAGOJWA HAYA (CARDIACVASCULAR DISEASES)
1.Kupalalaizi (stroke); karibia watu 160,000 hufa kwa stroke. Stroke ni shambulio la harka amablo linatokea pindi damu inayotembea kwenye ubongo ikapata hitilafu yoyote. Hutokea pindi damu ikaganda katika vimishipa hivyo na kuzuia mzunguruko wa damu kwenye ubongo. Au hutokea mishipa ikapasuka na kusababisha damu kuvuja kwenye ubongo. Hali hizi zote zikitokea hueza kusababisha kupalalaizi. Mishipa hii huweza kupasuka kama shinikizo la damu likawa kubwa sana. Wataalamu wa afya wanatueleza dalili ya tatizo hili kabla halijatokea. Dalili hizi ni kama:-
A).Kuchoka kwa ghafla kwa mikono, miguuna kuona maluelue.
B).Kushindwa kuona jicho moja au yote
C).Kizunguzungu cha ghafla au kupoteza fahamu.
D).maumivu ya kichwa ya ghafla bila ya sababu maalum
2.Shinikizo la juu la damu (high blood pressure);Kitaalamu tatizo hili huitwa high blood pressure au hypertension. Watu wengi hawajijui kama wana tatizo hili ila wanakuja kujikuta wamepatwa na shambulizi la moyo (heart attack) au stroke. Shinikizo la damu ni hali inayotokea katika mfumo wa damu ambapo kasi ya mzunguruko wa damu inakuwa kubwa zaidi kiasi kwamba njia haitoshi hivo kujalibu kutanua kuta za mishipa ya damu na misuli ya moyo. Huweza kusababisha stroke au kuufanya moyo kufanya kazi kwa taabu ama moyo kushindwa kabisa kufanya kazi. Pia huweza kuathiri baadhi ya viungo vya mwili kama figo, na macho. Kuganda kwa mafuta kwenye kuta za damu huenda ikawa ni sabubu kubwa ya kutokea kwa tatizo hili kama tutakavoona hapo mbele.
3.Shambulio la moyo (heart attack); mishipa ya coronary arterries inakazi ya kusafirisha dabu yenye oxyjen na virutubisho (nutrients) kwa ajili ya kulisha seli za moyo zinazoufanya moyo ufanye kazi yake. Mishipa hii ni myembamba na imeuzungurika moyo.sasa ikitokea damu imeganda kwenye mmoja ya mishipa hii na kuzuia damu isipite kwenye mshipa ule na kuifanya damu isifike kwenye moyo, hii huweza kusababisha seli za moyo zikafa kwa kukosa hewa ya oksijeni na virututisho vilivyotakiwa kuletwa kupitia mshipa ule. Na hapa mtu atasikia maumivu kwenye kifua chake. Na hii ni kwa sababu ya moyokutoweza kupata damu ya kutosha. Shambulio la moyo ni kuathirika kwa misuli ya moyo au kushindwa kufanya kazi misuli ya moyo. Shambulio la moyo halinaga dalili za waziwazi ila wataalamu wa afya wanataja hizi;-
A)kuhisi kubanwa na maumivu katikati ya kifua na hali hii huendelea kwa muda wa dakika kadhaa.
B)Maumivu yanayoendelea mpaka kwenye mabega, shingo na mkono.
C)Kutokujisikia saswa kifuani kunakofuatana na kuzimia, kutoka jasho jingi sana, damu za pua, au kuvuta punzi chache sana.
4.Atherosclerosis; hii hutokea pale mishipa ya damu inapokuwa na mafuta (fatty) yaliyoganda kwenye mishipa hiyo na kuathiri mzunguruko wa damu wa kawaida. Hali hii ni hatazi kwani inaweza kuzuia damu kuzunguruka katika shemu kadhaa za damu. Pia kama donge la mafuta haya likibanduka na kuingiea kwenye damu na likaingia kwenye coronary arterries (vimishipa vinavyolisha misuli ya moyo) inaweza kusababisha shambulio la moyo na kama litaingia kwenye ubongo litasababisha stroke. mafuta Kawaida
NAMNA YA KUPAMBANA NA MARADHI HAYA
1.Punguza kula kula vyakula vya mafuta kwa wingi na upunguze pia kula chumvi nyingi.
2.Hakikisha uzito wako upo katika kiwango kinachotakiwa. Nnda kapime ujuwe unazito sahihi.
3.Wacha kuvuta sigara
4.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
5.Punguza misongo ya mawazo.
2.SARATANI (CANCER)
Saratani ni ugonjwa unaotokana na kukuwa kwa seli ndani ya mwili bila ya mpangilio maalumu. Kukuwa huku kunashindwa kuthibitika ndani ya mwili. Seli hizi hukuwa na kusababisha kitu kinachoitwa kitaalamu tumor. Hii ni mkusanyiko wa hizi seli ambazo zimekuwa bila ya mpangilio maalumu ndani ya mwili. Hizi tumor husababisha kutokea kwa malignant tumor na hii ni mkusanyiko mkubwa wa hizi seli ambao huuwa seli nyingine za mwili na tishu. Hutokea wakati mwingine huu mkusanyiko ukawepo ila ukawa hauna madhara kwa seli nyingine, huu utaitwa benign tumor ila zikikuwa zaidi huweza kuathiri tishu za mwili. Hizi tumor zinaweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kuenea sehemu zingine za mwili.
Seli za saratani ni hatari zaidi kwani zinaweza kuharibu tishu na viungo vingine vya mwili kama ubongo na maini. Kiti hatari zaidi kwenye seli hizi ni kuwa zinaweza kuhama sehemu moja ya mwili kwenda sehemu nyingine. Kwa mfano saratani ya maini inaweza kuenea kwenye ubongo na kusababisha saratani ya ubongo. Saratani ya matiti na korodani inaweza kuenea kwenye mifupa na kusababisha saratani ya mifupa. Hali hii hufanya seli hizi ziwe hatari zaidi. Mchakato huu wa kuhama sehemu moja kwenda nyingine huitwa kitaalamu metastasisi.
Seli ya saratani ya kwanza hutokea pale gene zinapopata hitilafu. Gene ni chembechembe ambazo huhusika katika kutengenezwa kwa selimmpya. Mtu anaweza kurithi gene hizi ambazo zimeharibiwa toka kuzaliwa ama akawa anazo zimeharibiwa kwa sababi zingine. Ila mtu huyu aliyerithi gene ambazo zina hitilafu ni rahisi kwake kupata saratani zaidi kuliko huyu ambaye hajarithi. Kama tulivyoona juu kule kuna mawakala wa kueneza maradhi, hali kama hii kuna mawakala wa kusababisha saratani ambao huitwa carcinogens hawa pia huhusika katika kutia hitilafu kwenye genes. Mifano ya mawakala hawa (carcinogens ) ni ;-
1.Aina flani ya virusi kama vile papilloma virus (HPV)
2.Mionzi kama radio na ulteraviolent (UV) na mionzi mingineyo.
3.Kemikali zinazopatikana kwenye tumbaku kama arsenic, benzene na formaldehyde
4.Asbestos haya ni malighafi zinazotumika kutengezea vifaa vya umeme na vifaa vingine vya nyumba kama vya kuzuia moto.
Ni vigumu sana kuepukana na mawakala hawa kwenye maisha, kwani huweza kupatokana kwwenye vyakula vyetu, shuhuli zetukwenye maji na hewa. Ila tutakujaona kwamba unaweza kujiepusha na hatari za saratani kwani karibia mawakala walotajwa hapo juu hueneza saratani ila kwa uchache ila tumbaku ni kwa kiasi kikubwa sana.
Unaweza ukagunduwa saratani kwa kutumia vifaa vya kitaalamu kama MRI, x-rays, biospy, na DNA test. Pia unaweza ukajijua mwenyewe kama una tumor kwa kujishika sehemu husika na kuona kama kuna uvimbe wowote usio wa kawaida. Pia ijulikane kuwa zipo tiba za saratani ijapokuwa kuimaliza kabisa mwilini ni kazi mzito ila ukweli ni kuwa karibia aina zote za saratani zinaweza kutibiwa kama mtu atawahi kwa haraka.baadhi ya njia wanazotumia kupambana na saratani ni kama
A)kufanyiwa upasuaji, hufanyika kwa ufasaha zaidi kama saratani haijaenea zaidi
B)Kufanya chemotherapy ni matumizi ya dawa kwa ajili ya kuuwa seli za saratani, ila kwa bahati mbaya njia hii pia huuwa seli nyingine za mwili
C)Radiation therapy ni kutumia mionzi kwa ajili ya kuuwa seli za saratani
DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI
Ugonjwa wa saratani hutokea pale seli za mwili zinapokuwa bila ya mpangilio maalumu na kusababisha uvimbe. Uvimbe huu huenda ukawa mkubwa zaidi na kusababisha uharibifu wa viungo vya mwili kama maini ubongo na mishfupa. Uvimbe huu pia hueza kusambaa mwilini na kusababisha vimbe mbalimbali ndani ya mwili.
Kikawaida seli ndani ya mwili huzaliwa na baadaye huweza kufa baada ya kipindi maalumu. Kwa mtu mwenye saratani seli hizi hazifi hivyo huendelea kukuwa bila ya mpangilio. Seli hizi huweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kusambazwa kuelekea sehemu zingine za mwili na hatimaye kusambaa kwa saratani viungo vingine vya mwili.
Katika sababu za kutokea kwa saratani ni pamoja navyakula 35%, sigara30%, mionzi ya jua 10%, virus 7%, shughuli za kazi 4%, pombe 3%, mionzi 1% na sababu nyinginezo kwa 10%. Hivyo hapa utaona kuwa vyakula na uvutaji wa sigara vipo katika msitari wa mbele kusababisha ugonjwa wa saratani.
Mwaka 2000 WHO wametowa ripooti inayoeleza kuwa ugonjwa wa saratani ndio unaoongoza kwa kusababisha vifo vya watu wengi duniani.mwaka 2004 watu milioni 7.4 wamefariki kwa ugonjwa wa saratani ambayo ni sawa nsa 13% ya vifo vyote vilivyotokea duniani mwaka huu. Saratani ya maini, tumbo, utumbu na saratani ya matiti ndo zimeongoza kwa vifo vya watu duniani. Vifo vinavyosababishwa na saratani vinatarajiwa kuongezeka kila siku na vinatarajiwa kufikia milioni 12 ifikapo mwaka 2030. (WHO. 2009).
Dalili za ugonjwa wa saratani hutofautiona sana kulingana na aina ya saratani ambayo mtu anayo. Zipo aina zingine za saratani hazioneshi dalili zozote mpaka zitakapokuwa zimeenea vizuri mwilini. Ingawa hali ipo kama hivyo lakini wataalamu wa afya wameonesha baadhi ya dalili ambazo zinaonekana kwa watu wengi wanaopata saratani ambazo ni;-
Homa;
Haya ni maumivu ya kishwa yasiojulikana chanzo chake. Maumivu haya sio ya ugonjwa wowote wenye kuonekana, hata mgonjwa akipimwa huenda asikutwe na kitu chochote .maumivu haya ni yenye kuendelea kwa muda mrefu
Uchovu;
Huu ni uchovu ambao hauishi katu. Hata mtu apate muda wa kupumzika lakini katu uchovu huu hautaondoka. Japo mgonjwa wa kisukari pia hupata uchovu kama huu lakini saratani ina uchovu wa kipekee. Hivuyo ni vizuri kumuona daktari akwambie aina ya uchovu ulonao.
Mabadiliko katika mfumo wa chakula;
Mabadiliko haya ni pamoja na kushindwa kumeza chakula au kukosa choo. Dalili hizi huenda zikafanana na magonjwa mengine, hivyo ukiona mabadiliko haya wahi ukamuone daktari.
Kushindwa kupumua vizuri;
Saratani ya mapafu huweza kuonesha dalili hii ya kushindwa kupumuwa vizuri. Hii hutokea pale ambapo kuna vimbe sa saratani katika mfumo wa upumuaji. Inaweza kuwa kwenye mapafu au koo.
Kikohozi;
Hiki ni kikohozi ambacho sababu yake hasa ni ngumu kujulikana. Kikohozi hizi hakisikii dawa yoyote na ni chenye kuendelea. Saratani katika mfumo wa upumuaji kama mapafu huweza kuonesha dalili hii
Mabadiliko katika ngozi;
Hapa ngozi inaanza kubadilika rangi. Pia vimbe ndani ya ngozi huanza kutokea. Madoa meupe kwenye ngozi, mdomo, na kwenye ulimi. Pia mtu anaweza kuwa na makovu ambayo hayaponi.
kutokwa na damu;
Damu zinaweza kutoka katika maeneo mbalimbali kama vile sehemu ya haja kubwa na haja ndogo kwa wanaume na wanawake. Pia damu huweza kutoka kwenye matiti ambayo ni dalili ya saratani ya matiti.
Uvimbe kwenye matiti na korodani;
Huu ni uvimbe usio wa kawaida ambao unaanza kukuwa kwnye matiti kama dalili ya saratani ya matiti. Wakati mwingine ngozi ya matiti inakuwa ngumu. Hali hii pia hutokea kwenye korodani ambapo kunatokea uvimbe usio wa kawaida. Vimbe hizi pia huweza kusababishwa na mambo mengine hivyo hakikisha unamuona daktari kwa mabadiliko haya.
Kupoteza fahamu au kifafa;
Kwa saratani ya ubongo huweza ikamfanya mtu aweze kupoteza fahamu. Pia hutokea mtu akaanza kupata aina za kifafa. Saratani hii hutokea pale ubongo uapotengeneza uvimbe.
Hitimisho;
Ushauri wangu ni kuwa watu waishi kwa uangalifu kwani matibabu ya saratani ni ya gharama kubwa sana ni ni machache hutolewa bure. Halikadhalika hospitali zinazotowa matibabu ya saratani ni chache pia.
NJIA ZA KUPAMBANA NA SARATANI
1.Wacha kuvuta. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kuna kemikali nyingi kwenye tumbaku ambazo ni hatari.
2.Wacha kunywa pombe
3.Kula mboga za majani kwa wingi na punguza kula mafuta, kula matunda kwa wingi hii husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani
4.Fanya mazoezi na udhibiti afya yako
5.Linda ngozi yako
VYAKULA VYA KUPAMBANA NA KANSA
Kansa ni katika magonjwa yanayosumbuwa kwa kiasi kikubwa leo duniani. Kansa huweza kusababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo uvutaji wa sigara kwa 31%, vyakula kwa 37%, pombe kwa 3% na nyingine nyingi. Katika sababu hizi vyakula huchukuwa nafasi kubwa katika kusababisha kansa.
Mwaka 2015 watu milioni 90.5 waligungulika kuwa na kansa. Inakadiriwa kuwa kila mwaka takribani watu milioni 14.1 wanaupata kansa kila mwaka. Watu milioni 15.7 walikufa na kansa ambayo ni sawa na asilimia 15.7% ya vifo vyote mwaka huo.
VITUNGUU SAUMU ( GARLIC)
Hivi vina kiasi kikubwa cha madini ya salfa (sulphur compounds) ambayo husaidia kuimarisha mfumo wa afya mwilini (immune system) Pia wanasayansi wanafahamu kuwa kitunguu thaumu kinasaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya tumbo.
Samaki
Tafiti za kisayansi zilizofanyika Australia zimegunduwa kuwa ulaji wa samaki mara 4 au zaidi humuepusha mtu na kansa ya damu ( blood cancers leukemia, myekoma, and non- Hodgkin’s lymphoma). Samaki wanaoshauriwa zaidi ni wale wenye mafuta kwa wingi kama salmon.
Kama ilivyoosheshwa kuwa mpangilio mbovu wa vyakula na uvutaji wa sigara huchangia kwa kiasi kikubwa kupata kansa, leo tutakuletea baadhi ya vykula ambavyo vinasadikika kupambana na kansa. Vyakila hivi huweza kuzuia seli za kansa kutengenezwa ndani ya mwili na kutowa msaada wa kupambana na zo . Vipo vyakula vingi tuu lakini kwa uchache tunakuletea hivi kwa leo;-
Apple (maepo)
Matunda haya yanafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kuuwa seli za kansa. Tafiti za kisayansi zilizofanywa nchini Ujerumani zinathibitisha uwepo wa procyanidins ambayo hufahamika kudhibiti seli za kansa kutengenezwa ndani ya mwili.
Avocado (palachichi)
Matunda haya pia husaidia kwa kiwango kikubwa kupambana na seli za kansa. Fat iliyoko kwenye matunda haya huweza kusaidia kwa iwango kikubwa kupambana na kansa.
Kabichi ( cabbage)
Kabichi hujulikana kwa kuwa na bioflavonoids kemikali ambazo hupambana na seli za kansa. Kabichi kusaidia kupambana na kansa ya tumbo kansa ya matiti na aina zingine za kansa.
Karoti ( carrots)
Karoti zina alpha-carotene na bioflavonoids ambazo husaidia katika kupambana na seli za kansa. Karoti huweza kupambana hasa na kansa ya ini. Wanasayansi pia wanatahadharisha matumizi ya karoti kwa kiasi kikubwa kwa mtu anayevuta sigara.
7.Tende
Tende hujulikana kuwa na polyphenols ambazo husaidia kupambana na kansa kwa kiwango kikubwa. Vitamin B12 na fiber katika tende husaidi kwa kuiwango kupambana na aina mbalimbali za kansa.
Mayai yana vitamin D kwa kiwango kukubwa. Vitamin hivi pia hufahamika kwa uwezo wake wa kupambana na seli za kansa.
Tangawizi
Komamanga
njegere
MWISHO
Tungependa kutoa ushauri kwa dada na ndugu hao ambao huvuta na kunywa pombe kwamba haya yote yana kemikali ambazo zinajulikana kwa kuwa na uwezo wa kusababisha kansa. Kwa hivyo wanapaswa kuchukua maandalizi kabla hali inakuwa mbaya zaidi katika afya yao.
3.KISUKARI (DIABETES)
Mwili unahitaji nguvu na uwezo wa kufanya kazi, nguvu hii husababishwa na glucose iliyopo ndani ya mwili. glucose ni aina ya sukari ambayo hupatikana kwenye vyakula vya wanga. Mwili hauwezi kutumia glucose bila ya insulin. Insulin ni homoni ambayo inatengenezwa kwenye kongosho. Hii inakazi ya kudhibiti kiwango cha glucose ndani ya mwili. Yaani wakati kwenye damu kukiwa na glucose nyingi insulini huletwa ili kuipunguza na ikiwa ni kidogo insulin hailetwi.
Ikitokea mwili hauna uwezo wa kuzalisha insulini ya kutosheleza mwilini au seli zinashindwa kutumia insulini inayozalishwa hapa kisukari hutokea. Yaani mwili utashindwa kudhibiti kiwango cha glucose. Katika hali hii seli zitashindwa kupata glucose hivyo kusababisha damu kuwa na glucose nyingi na hivyo figo hutowa maji mengi na kusababisha kukojoa mara kwa mara. Katika hali hii tumesema kuwa glucose ni aina ya sukari ambayo inahitajika kwa ajili ya kupata nguvu na uwezo wa kufanya kazi (energy) hivyo mwili utatumia fat na protin kujitengenezea energy hivyo kupelekea kuzalisha sumu ndani ya mwli. Na hali hii ikiendelea mtu aanweza kupoteza fahamu na hali hii huitwa diabetic coma.
AINA ZA KISUKARI
1.Type 1 Diabetes; aina hii huotokea wakati mfumo wa kinga mwilini (immune system) unaposhambulia seli zinazozalisha insulin katika kingosho. Seli hizi zinaposhambuliwa mwili utashindwa kuzalisha insulin. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa aina hii ya kisukari husababishwa na virusi pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Aina hii ya kisukari pia huitwa insulin-dependent au juvenile diabees. Hii hutibiwa kwa kutumia dawa na mara nyingi huweza kuonekana kabla ya miaka 18. Dalili za aina hii ni za hatari sana na hutokea kwa ghafla. Miongoni mwazo ni kiu kikali, kuchoka sana na kupunguwa uzito.
2.Type 2 Diabetes; pia aina hii huitwa noninsulin-dependent diabetes na mara nyingi huwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 40 na wale watu ambao wana uzito wa kuzidi.
Katika aina hii ya kisukari mwili unazalisha insulin lakini seli zinashindwa kuitumia insulin inayozaliwa. Miongoni mwa dalili zake ni kukojoakojoa, kiu kikali, kutokuona kwa ufasaha, kuchelewa kupona kwa majeraha na maambukizi ya mara kwa mara.
3.Gestation Diabetes; hii huwatokea sana wajawazito mwishoni mwa mimba na hupotea baada ya mtoto kuzaliwa. Hii huweza kuongeza hatari wakati wa kijifungua na kama mama amerithi kisukari kutoka kwa wazazi hali inaweza kuwa mbaya zaid. Dalili zake ni sawa na zile za hizo aina mbili hapo juu,
SABABU ZA UGONJWA WA KISUKARI
Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mwili unaposhindwa kuzalisha homon za insulin au mwili kushindwa kuzalisha homon za insulin za kutosha au mwili kushindwa kutumia homon za insulin. Wakati mwingine hutokea pale mfumo wa kinga mwilini (immune system) unapoathiri organ ya pancrease na kuathiri uzalishaji wa homon ya insulin.
Ugonjwa wa kisukari husababishwa na mabo mengi yakiwepo kurithi kutoka kwenye familia, mazingira na ufumo mbaya wa maisha (life style). Japkuwa ugonjwa wa kisukari huweza kurithi kutoka kwa wazazi au familia lakini mfumo mbaya wa maisha huchangia kwa kiasi kikubwa pia katika kusababisha ugojwa huu wa kisukari. Katika post hii nitazungumzia kwa namna gani mfumo mbaya wa maisha unavyoathiri kupatikana ugonjwa wakisukari.
Kuzidi uzito mwilini; kikawaida mwili unahitaji uzito maalumu kulingana na kanuni za afya. Uzito ukiwa mkubwa sna ni tatizo na ukiwa ni mdogo sana pia ni tatizo. Uzito kuwa mkubwa zaidi unapelekea homon ya insulin kutokuzalishwa kiwango kinacho takiwa au mwili kushindwa kutumia insulin vizuri (insulin resistance). Zipo njia nyingi za kupunguza uzito zikiwepo kupitia vyakula, mazoezi au kubadilisha mfumo wa maisha. Hakikisha kuwa uzito wako upo katika hali ya kawaida. Muone daktari akupe ushauzi kuhusu uzito wako.
Kutokufanya mazoezi; kikawaida mazoezi yana faida kubwa sana mwilini, zikiwemo kuufanya mwili uwe imara. Mazoezi huweza kusaidia mifumo mbalimbali ya mwili kufanya kazi vizuri kama vile mfumo wa chakula, mfumo wa damu na mfumo wa afya. Mazoezi huweza kumkinga mtu na magonjwa ,mbalimbali kama vile mafua, presha ya damu, shambulio la moyo na kisukari. Mazoezi hupunguza mlundikano wa mafuta kwenye mwili na kusaidia kuondowa uchafu mwilini kwa njia ya jasho. Kiafya inashauriwa mtu afanye mazoezi japo kwa wiki asikose mara tatu. Yapo mazoezi mengi tuu na yasiyo na haja na kujiumiza saana kama vile kuruka kamba au kukumbia jogging.
Mpangilio wa lishe, chakula ni muhimu kwa maisha ya kiumbe chochote, ila ulaji mbaya pia ni tatizo kwa afya ya kiumbe pia. Mtu anatakiwa ale chakula kwa namna ambayo haitamletea madhara katika afya yake. Mtu anatakiwa ale chakula ambacho hakitamletea kuzidi uzito au utapia mlo au kitambi. Haya huenda yakawa na madhara katika afya ya mtu na hatimaye kupata kisukari. Chakula chenye mafuta mengi, sukari nyingi ama chumvi nyingi vyote sio vizuri kutumia.
Mazingira; wakati mwingine inatokea mazingira watubwanayoishi yakapelekea kupata kisukari kwa mfano mashambulizi ya virusi. Kuna aina ya virus ambao wanashambulia mwili na kufanya mwili kushindwa kusazalisha homoni za kutosha kwa ajili ya kushibiti kiwango cha sukari ndani ya damu.
Kutithi; unaweza kupata ugonjwa wa kisukari kwa njia ya kurithi kutoka katika familia. Kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya kurithiwa kwa kupitia vizazi au kurithi rangi ya ngozi urefu au ufupi kutoka kwa wazazi vivyo hivyo kisukari huweza kurithiwa. Haijalishi kati ya baba nani ana kisukari lakini huenda ukakipata kwa kurithi. Pia huenda wazazi wakakwa na kisukari na wewe ukakisosa pia.
Hitimisho
Ijapokuwa ugonjwa wa kisukari ni hatari sana lakini kama mtu atafata masharti anaweza kuishi maisha mazuri tuu kama watu wengine. Jambo la msingi hapa ni kufuata masharti na kuendelea kutumia dawa za kisukari . Kufanya mazoezi na kubadilisha utaratibu wa chakula.
NAMNA YA KUISHI NA MARADHI YA KISUKARI
Japo kuwa ugonjwa wa kisukari ni hatari kwa afya lakini mtu anaweza kuishi vizuri kama atafata utaratibu na kanuni nzuri za kuishi na ugoonjwa huu. Kwa mfano nchini marekani zaidi ya watu milioni 23 wanasumbuliwa na kisukari lakini wanaishi maisha mazuri tuu. Hivyo kama mgonjwa atafata kanuni na masharti pamoja na kubadilisha fife style yaani namna anavyoishi anaweza kupunguza athari za uginjwa huu. Hapo chini utaona ushauri juu ya mwenye kisukari aishi
Chakula; mgonjwa wa isukari anatakiwa ale chakula kisicho na mafuta mengi, ckisicho na chumvi wala sukari nyingi. Kuala matunda na mboga za majani. Hakikisha unakula katika muda maalumu siku zote pia angalau upate chakula mara tatu kwa siku kula chakula kisicho kobolewa. Pia hakikisha unakunywa maji mengi zaidi kwa siku
Mazoezi; hakikisha unafanya mazoezi si chini ya mara tatu kwa wiki. Hii huenda ikasaidia kupunguza usito na kuthibiti kiasi cha sukari ndani ya mwili wako. Pia kufanya mazoezi ni muhimu kwa afya yako kwa ujumla. Mazoezi yanaweza kupunguza mlundikano wa mafuta kwenye ngozi na mishipa yta damu. Hali hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa kuapata strock na shambulio la moyo.
Dhibiti uzito wako; hakikisha kuwa hauna uzito usio wa kawaida. Yaani hakikisha kuwa unapunguza uzito kama uzito wako ni mkubwa. Pata ushauri wa daktari kuhusu uzito wako kama unakufaa au umezidi kulingana na afya yako. Zipo njia nyingi za kupunguza uzito kupitia vyakula, mazoezi na nyinginezo. Muone daktari au pata ushauri kwa walio na ujuzi wa njia salama ya kupunguza uzito.
Tumia dawa; kama kisukari kimeshindikana kuthibitiwa kwa nyia hizo hapo juu anza kutumia dawa. Zipo dawa maalumu kwa wagonjwa wa kisukari. Pia inashauriwa kuwa mtu aanze kutumia dawa za kumeza kabla ya zile za sindano. Muone daktari atakupatia dawa hizo kulingana na afya yako. Watu wengi wanakuwa wavivu wa kunywa dawa lakini kwa baadhi ya magonjwa uvivu huu ni hatari zaidi kwa afya zao.
Ugonjwa wa kisukari usipopata matibabu mapema au usipo fata ushauri jinsi ya kuishi na ugonjwa huu matatizo mengi yanaweza kutokea ikiwemo presha, shambulio la moyo na kupapalaiz (strock), matatizo ya macho na upofu pia na matatizo ya meno na finzi. kwa ujumla afya ya mtu inaweza kuwa katika hali mbaya zaidi na pia huenda ikamsababishia kifo.
Hutokea wakati mengine mgonjwa mwenye kisukari sukari inashuka chini kabisa, hapa mgonjwa anaweza kuonesha dalili mbalimbali zikiwemo;- kutoka na jasho jisngi,kupiga myayo mara kwa mara, kushindwa kuzungumza na kushinda kufikiri vizuri, kukosa fahamu, kukosa nguvu hata kidogo, kupata uchovu usio wa kawaida pia mtu anaweza kujihisi kama ndo anataka kufa vile. Hali ikiwa hivi kuna huduma ya kwanza ambayo anatakiwa afanyiwe kama kupewa juisi ya matunda nusu kijombe. Glucose vijiko 3, maziwa kikombe kimoja,
Katika magonjwa yanayosumbuwa leo kisukari ni moja wapo japo halichangii kuuwa watu wengi kama magonjwa mengine. Ni vizuri kujuwa kama unakisukari au huna ili uweze kuchukuwa hatuwa mapema. Pia kwa wale wanaovuta sigara kisukari ni hatari na tabia hii, ni vizuri kuacha uvutaji wa sigara na kuacha kabisa pombe kwa ni yote haya ni hatari zaidi kwa mwenye kisukari.
KUPAMBANA NA KISUKARI
A)hakikisha una uzito wa kawaida
B)Wacha kutumia bidhaa za tumbaku
C)Punguza misongo ya mawazo
D)Fanya mazoezi ya mara kwa mara
E)Kula mlo kamili
4.UGONJWA WA UTI
UTI ni kifupisho cha Urinary Track Infection. Ni ugonjwa unaoshambulia katika mfumo wa mkojo, hususan kibofu, figo na mirija ya urethra. Ugonjwa huu umekiwa ukiwapata sana wanawake kwa kiasi kikubwa kuliko wanaume. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu 5 mmoja ana UTI.
Maambukizi ya ugonjwa huu yanapatikana hasa chooni. Pia huenda ugonjwa huu ukaenezwa kupitia kuingiliana kimwili na utaratibu mbovu wa kujisafisha baada ya kukidhi haya. Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata zaidi watu ambao wanatumia vyoo vya shirika yaani vyoo vinavyotumiwa na watu wengi.
Ugonjwa wa UTI umekuwa ukisababishwa na bakteria kwa kiasi kikubwa. Bakteria aina ya E.coil ambao wanapatikana kwenye utumbo mkubwa wamekuwa wakisababisha UTI kwa kiasi kikubwa kuliko bakteria wengine. Pia fangasi (fungi) na virusi huweza kusababisha UTI japo kwa kiwango kidogo.
Mtu anaweza kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa huu kwa,;-
1.Jisafishe kutokea mbele kuelekea nyuma baada ya kukidhi haja kubwa (kwa wanawake). Hii husaidia kuzuia bakteria wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wasipate nafasi ya kuingia kwenye njia ya haja ndogo.
2.mwaga maji kila uingiapo chooni kwaajili ya nkujisaidia. Kitendo hiki kitaondosha vijidudu vilivyopo pale chini.
3.Jisafishe sehemu za siri kabla ya kuingiliana na baada.
4.Hakikisha unakwenda kutoa haja ndogo (kukojoa) baada ya tendo la ndoa. Kitendo hiki kitasaidia kuondosha vijidudu vilivyoingia wakati wa tendo.
5.Nenda katoe haja ndogo haraka sana baada ya kuhisi.
6.Kunywa maji mengi zaidi. Husaidia kuondowa vijidudu kwa njia ya mkojo.
7.Vaa nguo za ndani za pamba, kavu na zisizobana.nguo za mpira na zinazobana husababisha jasho (majimaji) sehemu za siri. Majimaji haya husaidia bakteria kukuwa na kuishi hivyo wanaweza kuathiri njia ya mkojo.
Ugonjwa wa UTI una dalili nyingi na huenda nyingine zikafanana na dalili za malaria. Miongoni mwa dalili hizi ni;-
1.Maumivu wakati wa haja ndogo
2.Kutowa mkojo mchafu. Mkojo unawea kuwa na rangi sana, ua kama wa mawingu na kadhalika.
3.Harufu kali sana ya mkojo.
4.Mkojo kuwa na damu
5.Kukojoa marakwa mara hata kama mkojo utakuwa ni mchache sana.
6.Maumivu ya mgongo na tumbo kwa chini.(lower abdomen)
7.Maumivu ya kichwa.
8.Kuhisi uchovu sana
9.Miwasho sehemu za siri.
Itambulike kuwa ugonjwa wa UTI unatibika bila ya matatizo. Jambo la msingi ni kuwa wagonjwa wengi wamekuwa hawamalizi dozi. Kwakuwa ugonjwa huu umeenea sana na ni rahisi kuupata imetokea hali za kujirudia rudia. Hivyo mgonjwa ni muhimu kuchukuwa tahadhari tulizotzja hapo juu wakati akiwa anatumia dozi. Pia watu wawe makini na tiba za kiasili ambazo husemekana zinatibu UTI.
5.MAFUA
Mafua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya mafua na pia inasadikika kuwa zipo takribani aina 200 za virusi hawa wa mafua wakiwemo rhinoviruses, parainfluenza viruses, enteroinfluenza viruses na vingine vingi. Virusi hivi hupatikana kwa kukutana na hewa yenye virusi hawa, pindi unapovuta hewa yenye mchanganyiko wa virusi hawa. Sababu zingine zinazosadikika kusababisha mafua ni panoja na sigara, moshi, mavumbi, baridi kuwa kali au kuchafuka kwa hewa.
Udonjwa wa mafua unadalili tofauti tofauti na huenda zikafanana na ugonjwa wa malaria. Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kuhisi uchovu, kutokwa na makamasi mengi, koo kukereketa, maumivu ya kichwa na kupiga chafya mara kwa mara. Japo dalili za mafua hutofautiona kwa mtu na mtu kulingana na uwezo wa mwili wake kupambana na magonjwa ila hizi dalili tulizozitaja huwa maarufu kwa watu wengi.
Mgonjwa wa mafua huenda akawa amechoka sana kiasi kwamba analala kitandani kwa homa kali aliyo nayo. Mafua huwaathiri zaidi watoto na wazee kwani miili yao haina kinga za kutosha kupambana na maradhi. Kwa wale wenye HIV+ ugonjwa wa mafua pia hueza ukawaletea athari kubwa sana ikiwemo homa kali na uchovu.
Mtu ana weza kujikinga na mafua kwa kuosha mikono kabla na baada ya kula, kuziba mdomo anapopiga chafya. Kula vyakula vyenye vitamin A na C kwa wingi, kunywa maji mengi na kupunguza mawazo yaani ”stress” kwa lunga ya kigeni hapa kinacho maanishwa ni kuwa na furaha. Jambo la msingi limgine ni kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mare humuepusha mtu na mafua kwa kiasi kikubwa.
Miongoni mwa vyakula anavyotakiwa ale mwenye mafua ni kama mboga za majani zenye vitanimi kwa wingi, kwa mfano spinach, na mchicha. Pia kula matunda yenye vitamin C kwa wingi kama mapapai, na machungwa. Vyakula hivi husaidia katika kuupa mwili uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi na mashambulizi mengine. Maji ya kutosha humsaidia mtu mwili wake kuweza kufanya kazi ya kudhibiti maambukizi kwa urahisi. Hali kadhalika kufaya mazoezi husaidia mwili kufanya kazi vizuri. Pia anashauriwa mgomjwa wa mafua awe chai.
Wapo baadhi ya wataalamu wa tiba mbadala wanazungumzia matumizi ya kitunguu maji kuhusu kutibu mafua. Wanatumia harufu ya kitunguu maji kutibu mafua. Mgonjwa atachukuwa kitunguu kasha ataondowa majani, au maganda ya juu kisha atakuwa anavuta haruvu ya kitungu. Atafanya hivyo kwa mara kadhaa hasa anapokwenda kulala.
6.VIDONDA VYA TUMBO
Ni vidonda vinavyotokea katika ukuta wa tumbo. Vidonda hivi tumezoea kuviita vidonda vya tumbo ila hapa nitataja kitaalamu kuwa vidonda hivi hufahamika kama peptic ulcers. Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa H.pylori au kulika kwa ukuta wa tumbo kutokanana na athari za tindikali zilizopo tumboni (stomach acids) kama vile tindikali ya hydrocloric yaani hydrocloric acid. Kwa wakati tulio nao hili ni tatizo la kawaida maana limewapata watu wengi na halisabababishi vifo vya watu wengi kama maaradhi ya saratani na kisukari.
Vidonda hivi vimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:-
1.gastric ulcers hivi hutokea ndani ya tumbo la chakula
2.Esophageal ulcers hivi hutokea ndani ya esophagus. Hii ni sehemu inayounganisha kati ya koo la chakula na tumbo la chakula.
3.Duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum
Sababu za kutokea vidonda hivi
1.mashambulizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori (H.pylori). Hawa bakteria wanaweza kusabababisha mashambulizi na kuathiri sehemu tajwa hapo juuu na kusababisha vidonda hivi.
2.Matumizi ya baadhi ya aina za madawa mara kwa mara. Kuna aina za dawa ambazo kwa sasa zimepigiwa marufuku lakini hutumika kwa njia za panya. Madawa haya huweza kusababisha vidonda hivi kwa mfano aspirin, ibuprofen na naproxene n.k
3.Uvutaji wa sigara
4.Kunywa pombe kupita kiasi
5.Athari ya miozi
6.Saratani ya tumbo
7.Misongo ya mawazo (stress)
8.Kukaa na njaa kwa muda mrefu.
DALILI ZA VIDONDA HIVI.
Dalili hizi hutofautiana kulingana na aina za vidonda. Ila hapa nitaorodhesha baadhi ambazo ni kawaida kwa vidonda hivi.
1.maumivu ya tumbo kutokea kitomvuni mpaka kifuani
2.Kukosa hamu ya kula
3.Kutoka na damu na kupata choo cheusi sana
4.Kupungua uzito bila sababu
5.Kutapika
6.Maumivu ya kifua
7.Tumbo kujaa.
8.Kuchoka ana
KUTHIBITI VIDONDA HIVI
1.wacha au punguza kunywa pombe
2.Usichanganye vilevi na madawa mengine
3.Punguza kutumia madawa aina ya aspirin n.k
4.Osha mikono yako mara kwa mara kuepuka maambukizi ya bakteria
5.Punguza misongo ya mawazo
6.Kula katika muda uleule.
<
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 686
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zifazofanana:-
Dalili za maambukizi ya sikio kwa watu wazima
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Maambukizi ya sikio mara nyingi ni maambukizi ya bakteria au virusi ambayo huathiri sikio la kati, nafasi iliyojaa hewa nyuma ya ngoma ya sikio ambayo ina mifupa midogo ya sikio inayotetemeka.
Maambukizi ya si Soma Zaidi...
Dalili za maumivu ya uti wa Mgongo
Posti hii inahusu zaidi dalili za uti wa mgongo ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uti wa Mgongo. Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster. Kwa hiyo ili kugundua kubwa mtu ana Ugonjwa huu Dalili kama hizi zifuatazo zinaweza kutokea kwa mgonjwa. Soma Zaidi...
Ugonjwa wa upele na matibabu yake
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa upele na matatibabu yake, ni ugonjwa unaosabavishwa na mdudu kwa kitaalamu huitwa mites sarcoptes scrabie mdudu huyu usababisha miwasho kwenye ngozi. Soma Zaidi...
Sababu zinazopelekea tumbo kujaa gesi
Kiufipi posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na sababu zinazopelekea tumbo kujaa gesi Soma Zaidi...
Saratani ya matiti (breasts cancer)
Post yetu inaenda kuzungumzia kuhusiana na Saratani ya Matiti ni Saratani ambayo hutokea katika seli za matiti. Baada ya Saratani ya Ngozi, Saratani ya matiti ndiyo Saratani inayojulikana zaidi hugunduliwa kwa wanawake Mara nyingi. Saratani ya Soma Zaidi...
Maradhi ya macho, dalili zake na matibabu yake
Makala hii itakufundisha maradho makuu ya macho, matibabu yake na tiba zake Soma Zaidi...
Fahamu Ugonjwa wa misuli kuwa dhaifu.
hali ambayo misuli unayotumia kwa hotuba ni dhaifu au unapata shida kuidhibiti mara nyingi inaonyeshwa na usemi wa kufifia au polepole ambao unaweza kuwa mgumu kuelewa. Sababu za kawaida za Ugonjwa huu ni pamoja na matatizo ya mfumo wa neva (neurolojia Soma Zaidi...
Ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa kisukari hurejelea kundi la magonjwa yanayoathiri jinsi mwili wako unavyotumia sukari kwenye damu (glucose). Glucose ni muhimu kwa afya yako kwa sababu ni chanzo muhimu cha nishati kwa seli zinazounda misuli na tishu zako. Pia ndio chanzo ki Soma Zaidi...
Dalili za kwanza za HIV na UKIMWI kuanzia wiki ya kwanza toka kuathirika
DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Soma Zaidi...
Je dalili za kisonono au gonoria kwa mwanamke huonekana baada ya mda gani
Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa uvimbe na mashambulizi ya bacteria kwenye korodani
Posti hii inaonyesha dalili,Sababu,na namna ya kujikinga na ugonjwa wa uvimbe na mashambulizi ya bacteria kwenye korodani ambao kitaalamu hujulikana Kama orchitis. Soma Zaidi...