image

H-D HASSANI SUKARI YA MASHAIRI: (ndege, sababu ya neno lako, penzi penzini, wa ndotoni)

H-D HASSANI SUKARI YA MASHAIRI: (ndege, sababu ya neno lako, penzi penzini, wa ndotoni)

kitabu cha mashairi

By Sukari ya mashairi

KITABU CHA MASHAIRI

SUKARI YA MASHAIRI
NENO LA AWALI:
Ni kitabu kilicho andaliwa kwa lugha ya kiswahili katika lugha iliyo nyepesi zaidi na yenye ufundi wa kishairi. Kitabu hiki kinapatikana kwa free yaani buree kutoka kwetu. Kwa yeyote anayetaka kukichapisha kitabu hiki awasiliana nasi kwa haraka zaidi.

Mtunzi wa kitabu hiki ni nguli chipkizi wa fani hii anayefahamika kwa jina la HD-Hassan. Kitabu hiki ni katika kazi zilizoandaliwa na mtunzi wetu huyu wa mashairi. Tumetarajia katika kitabu hiki kuelimisha na kuburudisha na si vinginevyo. Kama na wewe ni mshairi chipkizi na unataka kazi zako ziweze kusambawa nasi. Wasikiana nasi kwa 0620555380 au 0655832944 WhatsApp.

KUTOA NI USHUJAA

Salamu kwanza awali, wasikizi tikieni,
Mwambaje nazenu hali, kheri nawatakieni,
Mungu awape sahali, muifuzu mitihani,
Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,

Kila alie akili, hutunza yake thamani,
Hilo sote twakubali, sitaraji upinzani,
Zingata yangu kauli, ikufae maishani,
Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,

Mja ulie na mali, mtazame masikini,
Kwani wake udhalili, niqadari ya manani,
Kumtenga niajali, tena mbaya hukumuni,
Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,

Natena usikubali, aingie dhilalani,
Maliyo siibakhili, nikuipa kisirani,
Mungu kwayake ajili, mlinde huyo jirani,
Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,

Kumwacha niukatili, tena usio kifani,
Fikiria mara mbili, mali kwakomtihani,
Hakutatosha kuswali, namisaada toweni,
Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,

Ukitaka afadhali, nauishi kwa amani,
Mafunzo haya nakili, uyatie matendoni,
Kiombwa siwe mkali, toa kwadhati moyoni,
Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,

Maisha nipande mbili, kuna nyuma na usoni,
Ukatae ukubali, lambeleni hulioni,
Kesho hashindwi jalali, nawe kukushusha chini,
Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,

Mtunzi:HD.Hassan
@SUKARI YA MASHAIRI@
Pangani Tanaga
0655832944


NDEGE WAFIKISHIE

Hebu paa ndege paa, ufise habari hizi,
Ufike wanako kaa, imi kufika siwezi,
Paa bila kuzubaa, upae anga iwazi

Naujumbe huu twaa, tekeleza hiikazi,
Kawape utawafaa, watapo fanyiakazi
Kwa watakaokataa, usifanye lazimizi,

Wambie lamanufaa, niwasihilo mtunzi,
Elimu iso chakaa, ni ifanyiwayo kazi,
Ili wawe mashujaa, waepuke upuuzi,

Waache kata tamaa, katikalao amuzi
Subira ikiwajaa, lilofichwa huja wazi,
Shidani wakikomaa, lazima lije tatuzi,

Wasivunje ujamaa, sababu yamachukizi,
Wasiishi kwahadaa, nichukizo kwa mwenyezi,
Nawaache kuzubaa, wafanyapo andalizi,

Wambie elimu taa, kuikosa niajizi,
Mwenye elimu hun'gaa, sioleo tangu juzi,
Ujinga kizaazaa, mfano kama uchizi,

Yasaba beti nakaa, sitaki uendelezi,
Shikeni hayo kadhaa, yalainishe ulezi,
Tungo hii nibidhaa, nawaipe mapokezi,

Mtunzi:HD.Hassan
Tanga pangani
0655832944



NDEGE WAFIKISHIE

Hebu paa ndege paa, ufise habari hizi,
Ufike wanako kaa, imi kufika siwezi,
Paa bila kuzubaa, upae anga iwazi

Naujumbe huu twaa, tekeleza hiikazi,
Kawape utawafaa, watapo fanyiakazi
Kwa watakaokataa, usifanye lazimizi,

Wambie lamanufaa, niwasihilo mtunzi,
Elimu iso chakaa, ni ifanyiwayo kazi,
Ili wawe mashujaa, waepuke upuuzi,

Waache kata tamaa, katikalao amuzi
Subira ikiwajaa, lilofichwa huja wazi,
Shidani wakikomaa, lazima lije tatuzi,

Wasivunje ujamaa, sababu yamachukizi,
Wasiishi kwahadaa, nichukizo kwa mwenyezi,
Nawaache kuzubaa, wafanyapo andalizi,

Wambie elimu taa, kuikosa niajizi,
Mwenye elimu hun'gaa, sioleo tangu juzi,
Ujinga kizaazaa, mfano kama uchizi,

Yasaba beti nakaa, sitaki uendelezi,
Shikeni hayo kadhaa, yalainishe ulezi,
Tungo hii nibidhaa, nawaipe mapokezi,

Mtunzi:HD.Hassan
Tanga pangani
0655832944


KITANZI CHA MOYO

Niliwanyima wengine, upendo kuleta kwako,
Sikupenda tukosane, nikalinda hadhi yako,
Tukapanga tuowane, uwewangu niwe wako,
Amakweli naamini, penzi kitanzi chamoyo,

Nilichunga usinune, nikapunguza vituko,
Sikutaka tuchoshane, nikafata kilalako,
Tukasema tulindane, lakolangu langulako,
Amakweli namin, penzi kitanzi chamoyo,

Yote hayo hukumbuki, leowenda kwa mwengine,
Nina moyo sina siki, japo tuhurumiane,
Sawa kwako mamluki, ila sihaya mengine,
Amakweli naamini, penzi kitanzi chamoyo,

By@HD.Hassan SUKARI YA MASHAIRI@

NIMEUJERUHI MOYO,

Nalikiri langukosa, kupenda mia kwamia,
Ndio mana wanitesa, huku unafurahia,
Sijajua nini hasa, ulichonikusudia,
Nimeujeruhi moyo, kwakuvumilia yako,

Nilibembeleza penzi, kwazote nyingi heshima,
Hata sikuonakazi, kubeba kila lawama,
Ukaniona mshenzi, nakunitenda unyama,
Nimeujeruhi moyo, kwakuvumilia yako,

Nilisahau rafiki, ulivyo nishughulisha,
Nikawa kwako sitoki, kumbe bure najichosha,
Leo ninapata dhiki, nayachukia maisha,
Nimeujeruhimoyo, kwakuvumilia yako,

By @HD.Hassan sukari ya mashairi@



SANAA YANGU
@@@@@@@@

SIJIKWEZI SIJISIFU,
UTUNZI NDOFANI YANGU,
MARUFUKU KWANGU BIFU,
WALA CHUKI ASILANI,
#################

UCHESHI UCHANGAMFU,
HUO NDO WASIFU WANGU,
MIZOZO NA KHITILAFU,
MOYONI HAVINAFUNGU,
##################

NINA YANGU MAPUNGUFU,
SIWADHARAU WENZANGU,
SIJIPI UTIMILIFU,
HIYO NISIFA YA MUNGU,
##################

NINGALI BADO ALIFU,
NARINGA KWA KIPI CHANGU?
SITAKI KUCHEZA RAFU,
NIKA UDHI WALIMWENGU
###################

NI MUNGU NINO MUKHOFU,
SI WANADAMU WENZANGU,
WALA SIVAI UPOFU,
KUSHUSHA HESHIMA YANGU,
@@@@@@@@@@@@@@@

by.HD.Hassan




SABABU YA NENO LAKO

Sababu ya neno lako, nasema nimesikia,
Sababu ya neno lako, nasema hongera pia,
Sababu ya neno lako, nishajua yakonia,
Wasema afukuzwae, sihadi pasemwe toka,

Sababu ya neno lako, maumivu yanijia,
Sababu ya neno lako, nami leo nakwambia, 
Sababu ya neno lako, sitoweza kurudia,
Ndege unae muinga, hujua pakukimbia,

Sababu ya neno lako, sisiri nimeumia,
Sababu ya neno lako, mengi sasa najutia,
Sababu ya neno lako, najibadili tabia,
Pilau bila viungo, pishi halijatimia,

Sababu ya neno lako, sitoweza kukawia,
Sababu ya neno lako, sasa nabadili nia, 
Sababu ya neno lako, nimesha kushitukia,
Muwinda simba kwafimbo, maisha kayachukia,

Sababu ya neno lako, nilitamani kulia,
Sababu ya neno lako, sikuweza vumilia,
Sababu ya neno lako, shairi nakutungia,
Tamu ya ndimu sikula, hunoga haswa supuni,

Sababu ya neno lako, jibu nimejipatia,
Sababu ya neno lako, siwezi kun'gan'gania,
Sababu ya neno lako, kwengine nita hamia,
Baharia simkwezi, namkwezi sikwa mbizi,

Sababu ya neno lako, ngazi nishaiachia,
Sababu ya neno lako, waje wengine kungia,
Sababu ya neno lako, haya nimedhamiria,
Sitojali mambo yako, chochote sito kwambia.

(inakuhusu)

by HD.Hassan



CHUKI

Kwako lifike darasa, lisilo lamembarini,
Lisilo hitajipesa, adakama yashuleni,
Litambue hili kosa, silitie matendoni,
Mvaachuki moyoni, mwenyewe hujamtesa,

Kisikie hikikisa, utafakari kichwani,
Sichakale nicha sasa, sikiliza kwamakini,
Upate kiini hasa, nakipi utabaini,
Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa,

Bwana mmoja afisa, wacheo serikalini,
Alie akitikisa, kwa mbwembwe zote mjini,
Mkewe ekuwa tasa, ndio wake mtihani,
Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa,

Nduguye damu kabisa, kwake hali masikini,
Ekuwa na wana tisa, na wakumi e tumboni,
Ikatokea furusa, kuitwa kibaruani,
Mvaachuki moyoni, mwenyewe huja mtesa,

Bwana akaanza visa, vya kuvunja tumaini,
Ila ndugu hakususa, akatazama usoni,
Kumbe kilichomtesa!, apate vyote kwanini?
Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa,

Lilo likimtonesa, atarithiwa nanani,
Nahakutaka kabisa, wale wana wafulani,
Donda hilo halebesa, lemuweka taabani,
Mvaa chuki moyoni, huja mtesa mwenyewe,

Kufumbua na kupwesa, aondolewa cheoni, 
Bila kosa bila kisa, karudi uriyani,
Machungu akaalisa, kwahuzuni na nun'guni,
Mvaa chuki moyoni, hujamtesa mwenyewe,

Shida kuanza mnusa, msaada hauoni,
Hana nduru hana hisa, akangia majutoni,
maisha yakibubusa, ikawa kwake ngani,
Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa,

by HD.Hassan



SIOKOSA

Siokosa kwa mpenzi, kusoma tabia zako,
Siokosa tangu enzi, nahayo yalikuweko,
Siokosa saahizi, wala sionwe kituko,
Siokosa nihalali, muache ajiridhishe,

Siokosa kwa mkeo, kulijua chumo lako,
Siokosa juwa leo, muambie namwenzako,
Siokosa ndio cheo, anahaki hio kwako,
Siokosa nihalali, muache ajiridhishe,

Siokosa kwamchumba, kupima uwezo wako,
Siokosa siushamba, vitabuni pia liko,
Siokosa wala pumba, kuleta maswali kwako,
Siokosa nihalali, muache ajiridhishe,

Siokosa hilipia, kucheza na mkewako,
Sikosa kukufanyia, japo madeko madeko,
Sikosa akikwambia, apande mgongo wako,
Siokosa nihalali, muache ajiridhishe,

by.HD.Hassan




MWAMBIENI,

Mwambieni namtaka, pingu nizifungenae,
Mwambieni sitachoka, nikweli asishangae,
Mwambieni sitacheka, bila kuowana nae,
Mwambieni basi jama, ajue hili mapema,

Mwambieni nampenda, niwe baba awe mama,
Mwambieni nitakonda, pindi atapo nihama,
Mwambieni nitatenda, kila atakalosema,
Mwambieni basi jama, ajue hili mapema,

Mwambieni kwake chali, moyo ngwara kautia,
Mwambieni hata mali, zangu nitamuachia,
Mwambieni nakubali, isibaki hata mia,
Mwambieni basi jama, ajue hili mapema,

Mwambieni namuwaza, asubuhi na jioni,
Mwambieni sitaweza, kumtupa asilani,
Mwambieni nanyamaza, anionee imani,
Mwambieni basi jama, ajue hili mapema

by HD.Hassan



WARAKA

Waraka ninakutuma,
Ubebe yangu kalima,
Wende kwake hima hima,
Haraka ukamwambie,

Waraka kifika kwake,
Muulize hali yake,
Na huu ujumbe wake,
Haraka ukamwambie,

Mwambie sili silali,
Kichwani memnakili,
Namuwaza marambili,
Haraka ukamwambie,

Amegusa wangu moyo,
Mapigo yaenda mbiyo,
Yanitesa hali hiyo,
Haraka ukamwambie,

Waraka nenda sicheze,
Leo punguza ubize,
Nenda uje unijuze,
Haraka ukamwambie,

Tena mwambie namwita,
Jicho kwake limegota,
Aje bila yakusita,
Haraka ukamwambie,

Mwambie nitaabani,
Huba litele moyoni,
Na yeye ndo tumaini,
Ninae tumainia,

HD.Hassan
@SUKARI YA MASHAIRI





SIONI

Sioni kasoro yake, moyo chali kauweka,
Sioni mithili yake, bila yeye nitachoka,
Sioni nieleweke, simacho yalo pofuka,
Nisioni ya moyoni, kumpenda pekeyake,

Sisikii upuuzi, wauzushao fulani,
Sisikii uchochezi, walo nao majirani,
Sisikii uchafuzi, wa shombo za visirani,
Nisisikii yamoyo, kumsikiza ya kwake,

Sitaki mwengine kando, anitosha mahabuba,
Sitaki vingi vishindo, lanitosha lake huba,
Sitaki tena magendo, ikanikumba dhoruba,
Nisitaki ya moyoni, kutenda mabaya kwake,

Nikiwete wamawazo, mekuwa siwazi jambo,
Nikiwete mwenye tuzo, kwakuwaza yake mambo,
Nikiwete wavikwazo, hata anichape fimbo,
Nikiwete cha moyoni, kutopinga takwa lake,

Twabibu wangu wandani, betiri mgawa chaji,
Twabibu waperesheni, hodari mwenye kipaji,
Twabibu wakitandani, fundi mtoa masaji,
Nitwabibu matendoni, napenda hudumayake,

Ni yeye wangu wadhati, alonikaa moyoni,
Ni yeye mwenye bahati, kupendwa nami jamani,
Ni yeye mwenye sauti, yakunitoa pangoni,
Ni yeye kabisa ndiye, nimpendae kwa shani,

HD.Hassan
@SUKARI YA MASHAIRI
TANGA PANGANI




BENDERA

Bendera hueleweki, zachosha safari zako,
Kufatwa hustahiki, m'baya mwenendo wako,
Waishi kimamluki, upepo ndo bwana kwako,
Acha kufata upepo, hebu fanya lako zingo,

Bendera uno pepea, ujumbe huu niwako,
Usizidi kupotea, utashusha hadhi yako,
Utakako elekea, kuwe kule upendako,
Acha kufata upepo, hebu fanya lako zingo,

Bendera hatari sana, kukosa muelekeo,
Tena sio uungwana, hata kama una cheo,
Kitakua cheo jina, natena cheo kimeo,
Acha kufata upepo, hebu fanya lako zingo,

Bendera ninakuasa, tetea yako nafasi,
Kufata mkumbo kosa, kwachochea wasi wasi,
Achana nako kabisa, sitafute mada kesi,
Acha kufata upepo, hebu fanya lako zingo,

Bendera mlingotini, kusi asikuburuze,
Kaskazi kija ndani, umwambie niko bize,
Kwalengo na madhumuni, malengoyo utimize,
Acha kufata upepo, hebu fanya lako zingo,

Bendera kua imara, upepee upendavyo,
Sio burura burura, chambilecho kwenda ovyo,
Acha mikwara uchwara, mambo hivo so yalivyo,
Acha kufata upepo, hebu fanya lako zingo,

Bendera fanyia kazi, haya niliyo kwambia,
Bendera uyamaizi, yaweza kusaidia,
Bendera nafunga kazi, ukomo hapa natia,
Acha kufata upepo, hebu fanya lako zingo,

By HD.HASSAN


Pata kitabu Chetu Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 663


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

H-D HASSANI SUKARI YA MASHAIRI: (ndege, sababu ya neno lako, penzi penzini, wa ndotoni)
Soma Zaidi...