image

Orodha ya vyakula mbalimbali na kazi zake mwilini na virutubisho vyake

Orodha ya vyakula mbalimbali na kazi zake mwilini na virutubisho vyake

Zijuwe aina mbalimbali za vyakula na kazi zake mwilini

Bongoclass-afya

ORODHA YA VYAKULA MBALIMBALI NA AINA ZAKE NA UPATIKANAJI WAKE

ORODHA YA VYAKULA
Makala hii inakwenda kukuorodheshea vyakula mbalimbali na kazi zao mwilini. Orodha hii imepangiliwa kulingana na virutubisho vinavyopatikana kwenye vyakula hivyo. Hivyo basi nitakuletea orodha ya vyakula vya protini, fati, madini, vitamini, wanga na mafuta. Makala hii ni moja kati ya makala zetu zihusuzo afya na lishe bora.


VYAKULA VYA PROTINI
Samaki
Mayai
Maziwa
Nyama
Kunde
Maharagwe
Mbaazi
Mboga za majani
Dagaa
Kumbikumbi
Senene
Nafaka


Faiza na kazi za protini mwilini:


Protini husaidia katika kkujenga miili yetu. Pia husaidia katika uponaji wa vidonda, utengenezwaji wa homoni na utengenezwaji wa enzymes. Kwa ufupi protini ni kirutubisho kinachochukuwa nafasi kubwa zaidi katika miili yetu.


VYAKULA VYA VITAMINI K
Nyama
Mayai
Siagi
Maziwa
Mchicha
Kabichi
Spinachi
Kisamvu
Mapalachichi
Zabibu
Matunda mengine
Mboga nyingine za kijani


Faida na kazi za vitamini K mwilini
Husaidia katika kuganda kwa damu
Husaidia katika kuboresha afya ya ubongo
Husaidia katika kuthibiti matumuzi ya madini ya calcium mwilini
Husaidia katika kulinda afya ya mifupa
Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo



VYAKULA VYA VITAMINI C
Nyanya
Mapera
Pilipili
Papai
Tufaha (apple)
Karoti
Kitunguu
Palachichi
Embe
Kabichi
Pensheni
Zabibu
Nanasi
Limao
Chungwa
Papai


Faida za vitamini C
Husaidia katika utengenezwaji wa tishu mwilini
Husaidia katika uponaji wa vidonda
Ni antioxidant ambayo husaidi katika kuondosha sumu za vyakula mwilini
Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye



VYAKULA VYA VITAMINI B
Nyama
Mapalachichi
Mboga za majani
Mimea jamii ya karanga
Alizeti
Mayai
Pilipili
Ndizi
Viazi
Maharagwe na kunde
Nafaka kama mchele, mtama na mahindi


Kazi za vitamini B
Husaidia mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema
Huhitajika kwa ajili ya uzalishaji wa nishati (nguvu) mwilini
Husaidia katika utengenezwaji wa seli mwilini
Husauidia katika utengenezwaji wa hemoglobin hizi ni chembechembe katika seli nyekundu za damu
Husaidia katika kuchakata DNA
Husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya na kukomaa kwa seli



VYAKULA VYA VITAMINI E
Karanga
Palachichi
Maziwa
Samaki
Siagi
Viazi mbatata
Mchele
Siagi
Korosho
Spinachi
Alizeti
Mayai
Maini
Nyama


Kazi za vitamini E
Husaidia kuondosha sumu za kemikali na vyakula mwilin
Husaidia katika utengenezwaji wa utando wa seli mwilini
Husaidia katika utengenezwaji wa utando maeneo mbalimbali ya mwili kama neva
Husaidia katika ukuaji mzuri wa mifupa



VYAKULA VYA VITAMINI D
Chanzo kikuu cha vitamini D ni mwanga wa jua, vyanzo vingine katika vyakula nu:-
Mayai
Maziwa
Maini
Uyoga


Faida za vitamini D
Kusaidia unyonzwaji wa madini kutoka kwenye chakula kwenda kwenye damu
Hudaidia kuboresha afya ya mifupa
Mifupa kuwa imara, madhubuti na isiyopasuka kiurahisi
Hudaidia kwa afya ya moyo na mishipa ya damu
Pia husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani


VYAKULA VYA VITAMINI A
Maziwa
Maini
Karoti
Machungwa
Mchicha
Kabichi
Spinach
Kisamvu
Matango


Mboga za majani


Kazi za vitamini A
Husaidia katika kuimarisha afya katika mfumo wa upumuaji
Husaidia kulinda afya ya amcho
Pia huboresha mfumo w fahamu
Tatizo la kutoona vyema na upofu huweza kusababishwa na upungufu wa vitamini A mwilini.


VYAKULA VYA FATI
Karanga
Nazi
Maziwa
Mayai
Korosho
Palachichi
Nyama
Samaki
Nafaka


Kazi za fati mwilini
Kazi kuu ya fati mwilini ni kutupatia joto.
Fati pia ni chanzo cha nishati mwilini
Utando wa seli umetangenezwa na chembechembe za fati
Ubongo umetengenezwa na fati kwa asilimia 60
Fati husaidia katika ubebwaji wa vitamini ndani ya mwili



VYAKULA VYA WANGA
Mahindi
Mtama
Mihogo
Viazi
Ngano
Mikate
Mtama
Mchele
Keki
Krosho
Karanga
Ndizi
Nyama
Mayai
Maziwa


Kazi za wanga
Kazi kuu ya wanga ni kutupatia nguvu yaani nishati
Husaidia katika kuvunjavunja fati mwilini
Hupunguza matumizi ya protini kwa ajili ya kuzalisha nishati
Hutumika katika kutengenezea bidhaa na madawa



VYAKULA VYENYE MAJI KWA WING
Tikiti
Tango
Nanasi
Machungwa
Madanzi
Mapensheni
Miwa
Mapapai
Mastafeli
Matunda damu
Komamanga



Faida za maji mwilini
Kulainisha viungo
Husaidia katika utengenezwaji wa mate na makamasi
Husaidia katika usafirishwaji wa oksijeni mwilini
Huboresha afya ya ngozi
Huboresha afya ya ubongo, ugwe mgongo na milango ya fahamu
Husaidia katika kupunguza joto
Mfumo wa mmengenyo wa chakula unategemea maji
Husaidia katika kuondosha ushafu ndani ya mwili
Hutdhibiti shinikizo la damu
Huzuia uharibifu wa figo
Husaidia katika kupunguza uzito







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2283


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula tangawizi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za tangawizi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kunywa maziwa
Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia, sababu zake na dalili zzake
Hapa utajifunza sababu za kupatwa na maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia Soma Zaidi...

Fahamu vitamini K na kazi zake, vyakula vya vitamini k na athari za upungufu wake
kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake mwilini. Soma Zaidi...

Fahamau protini na kazi zake, vyakula vya protini, na athari za upungufu wake.
unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kitunguu thaumu
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Pilipili
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Kabichi
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kunazi/ lote tree
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kunazi/ lotetree Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Fyulisi
Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Matunda yenye vitamin C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukuletea matunda yenye vitamin C kwa wingi Soma Zaidi...