HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA WANAWAKE WATATU NA CHONGO WATATU

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA WANAWAKE WATATU NA CHONGO WATATU

wanawake watatu

By Rajabu Athuman

WANAWAKE WATATU WA BAGHADAD

ilipoishia.....
Mfalme akawa anawashawishi kwa maneno mazuri na kuwaambia 'nioneni kama mpo na rafiki zenu hapa na kuwa huru kusema chochote kile'. basi mabinti wakaanza kuangaliana wakitafakari ni nani aanze kusimulia hadithi yake. Kabla hawajaanza na wale machongo watatu wakaletwa ili wapate kusikiliza hadithi za wadada hawa. Basi wakaanza kusimulia hadithi zao kama ifuatavyo;-
sasa endelea nayo.....


HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA.
Kwanza jua ewe mtukufu mfalme kuwa wale mbwa wawili uliowaona ninawapiga ni ndugu zangu wa baba na mama mmoja. Tuliishi pamoja kwa zaidi ya miaka 10 toka kufariki kwa baba kabla ya kutokea yale ambayo umeyashuhudia usiku wa jana. Basi tambua ewe mtukufu mfalme kuwa dada zangu hawa walinifanyia ubaya ambao ndio chanzo cha haya yote. Basi wakati Zubeida anazungumza maneno haya mbwa walikuwa wakitingisha vichwa na kutowa machozi.


Tambua ewe mtukufu mfalme kuwa yote niliyokuwa nikiyafanya ni kwa ajili ya uhai wa mbwa hawa yaani dada zangu. Laiti kama sitawachapa fimbo zili wangelikufa papo hapo. Juwa ewe mfalme wa nchi hii kuwa yote niliyokuwa nikiyafanya sikuyafanya kwa hiari yangu ila nimeshinikizwa. Nini kulitutokea na nini ninachotakiwa kufanya. Nitaomba ushauri wako ewe mfalme baada ya kusikiliza hadithi yetu.


Basi pale kwenye ukumbi wa mfalme kukaingiwa na utulivu wa hali ya juu. Machongo watatu walikuwepo wakitaka kujua zaidi kilichowakuta wenzao. Wakati mfalme na waziri wake wananshauku ya kutaka kujuwa hasa nini kilimtokea Zubeida. Basi mfalme akaagiza hadithi hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye nyaraka maalumu. Basi Zubeida akaanza kuhadithia zaidi kama ifuatavyo;-


Tuliishi na baba yetu kwa furaha zaidi kwa muda wa miaka mingi. Mama yetu alifariki tukiwa wadogo, hivyo baba yetu akalazimika kuwa na majukumu ya umama. Baba yetu alikuwa ni mfanya biashara maarufu na alikuwa amefaniukiwa kwa kiasi kikubwa sana. Baba yetu alifariki kwa ghafla hata bila ya kuumwa. Baada ya mazishi tuligawana mirathi kwa mujibu wa sheria ya kuuslamu. Na kwa kuwa hatukuwa na ndugu wa kiume sote tulipewa mali ya mirathi kwa usawa kila moja.


Mimi na dada zangu wote tukawa tunafanya biashara. Wote tulinunua nyumba na kuendelea na biashara zetu. Kwa upande wangu nilifanikiwa sana na biashara zangu zilikuwa kwa haraka zaidi. kwa muda mfupi niliweza kurudisha mtaji wangu na kuanza kukusanya faida. Halikadhalika na dada zangu nao waliweza kutengeneza faida kwa muda mchache. Unaweza kusema lkuwa tulibarikiwa kibiashara.


Dada zangu waliolewa lakini mimi sikubahatika kupata mchumba. Siku szote nilikuwa namuomba Mwenyezi Mungu anipatie mchumba aliyekuwa ni mwema. Dada wa kwanza alipoolewa alihamishwa na mumu wake na kwenda mji wa jirani. Huko aliendelea na biashara zake pia, lakini kwa vituko vya mume wake hakuchukuwa muda akafilisika. Bila ya kuelewa chochote kumbe dada yangu aliposwa na mume yule si kwa sababu alimpenda ila ni kwa sababu ya mali zake.


Dada alipofiliskisa hakuweza kumuona mumewe tena kwake. Na alipokuja humpiga na kumtukana sana. Hakuwa hata anamletea cha kukila wala cha kuvaa. Nikiwa sina habari ya hili wala lile kwa yanayompata dada yangu. Hali iliendelea kuwa ngumu kwa dada yangu hata mambo yakamshinda. Kwa mujibu wa sheria za kadhi aliweza kudai talaka na kuachwa. Siku ile aloachwa yule mume wake alimvizia na kumpiga na kumchania nguo zake na kumnyang'anya kila alichokibeba.


Dada yangu alijikongoja hata akafika nyumbani kwangu. Kwa hakika sikumtambua kwa hali alonayo maana alikuwa ni nusu uchi. 'Ashakumu si matusi' dada yangu akaniambia nisitiri ndugu yangu kwa hakika nimekumbwa na msiba ambao sitausahau. Basi nilimpatia pesa ambayo nimeiweka akiba na kumpatia aanze na biashara. Dada aliweza kuanza biashara tena na kuanza kukuza mtaji. Alipotaka kunirudishia pesa nilompa nilikataa na kumwambia kuwa ilikuwa ni sadaka.


Kwa upande wa dada yangu wa pili yeye alipotaka kuolewa katu sikumilia kipingamizi. Na aliolewa na mfanyabiashara mwenzie wa nchi ya jirani.. Hawa walikuwa wakifanya biashara za majini kutoka kisiwa mpaka kisiwa. Basi dada na mume wake walifanya hivyo kwa juda wa miezi 6. kwa muonekano walionesha kupendana sana na kuishi kwa amani na furaha katika ndoa yao. Kwa ndani mambo hayakuwa hivyo. Kwa kuwa dada alibarikiwa kibiashara pia alikuwa na mali nyingi hata akamzidi mume wake zaidi ya mara tatu. Sasa bila ya yeye kutambua kumbe mume wake aliuwa napanga njama ya kumuibia mali zake na kumtelekeza. Siku moja walipokuwa kwenye dau mume wake alipanga njama na nahodha ili alizamishe dau kimaksudi. Kwa kuwa dada hakujuwa kuogelea waliamini atakufa tu. Basi walifanya kama hivyo na jahazi lilipozama dada alitumbukia majini.


Kwa kuwa ilikuwa ni njama nahodha na wenzake waliweza kuokoa mali na watu wengine na kumuacha dada yangu kuangamia majini. Mume wa dada waliendelea na safari zao wakiamini kwa kuwa dada ameshakufa kinachofata ni kugawana mali. Na mambo yakawa kama hivyo walivyopanga. Lakini kitu kimoja hakikuwa kama walivyotaka, ni kuwa dada yangu katu hakufia majini na aliokoka kwenye ajali hii. Kwa kweli Mwenyezi Mungu ni mkubwa.


Wakati dada alipotumbukizwa kwenye maji wanyama wa majini walikuwa wakicheza na samaki mkubwa alimbeba na kuja kumtupia ufukweni. Na kwa hali hii dada yangu aliweza kuokoka. Kwa bahati nzuri dada alipookolewa alitupwa kwenye ufukwe wa nchi yetu hii na kutegemea nguo alizoziokota ufukweni aliweza kuja nyumbani. Kwa hakika nilishindwa kumtambua isingelikuwa kidani chake alichokuwa anakipenda.


Sasa mimi na dada zangu tumekusanyika tena nyumbani baada ya utengano wa muda. Nilimpatia dada yangu huyu nae pesa kama nilompa dada yangu wa kwanza. Ana alianza kufanya biashara zake. Dada zangu hawa waliungana pamoja na kuanza kufanya biashara za majini. Hivyo wakawa wanatembea kwenye visiwa mbalimbali kufanya biashara. Kwakweli biashara zao zilikuwa vizuri sana na walipata umaarufu na mali nyingi pia. Walifanya hivi kwa muda mrefu takribani kwa miaka miwili. Sikujuwa kumbe waliweza kuwa na hisia za ubaya juu yangu.


Wakati fulani wakaniomba niungane nao kwenye biashara zao lakini nilikataa. Walirudia kuniomba kwa zaidi ya mara 4 kwa nyakati tofauti. Basi mara ya tano nikakubali na kwa haraka wakaanza kuandaa safari na kuniandalia pia kwa upendo walionesha kunijali sana.basi nikagawa pes zangu mafungu mawili, fungu moja nikalifukia kama akiba na fungu la piali nikalitumia kuandaa bidhaa. Basi maandalisi yalipokamilika sote tulitoka na kuelekea ufukweni na kupanda jahazi letu lililojaa bidhaa. Safari ilikuwa njema sana, na nilifurahia pia maana ilikuwa ni mara yangu ya kwanza japo nilitapika sana.


Tulikwenda kisiwa mpaka kisi tukifanya biashara. Kwa hakkika nilipata faida sana kuliko pale nyumbani. Kwa safri yote nilikuwa naomba tufike salama maana sikupenda mazingira ya majini. Basi tulipokuwa tukirudi nyumbani kwa ghafla upepo ulubadilika na mawimbi yakawa makubwa. Nahodha hakuweza kutia nanga hinyo akaliwachia jahazi lielekee kokote kule na hii ndio njia salama kwa manahodha. Basi jahazi lilikwenda mpaka upepo ulipotulia asubuhi ya siku ilofata.


Tulishangaa tupo karibu na kisiwa ambacho kinaonekana ni mawe tu. Basi nahodha alipoulizwa hakuwa na ujuzi wa eneo hili, ila akashauri watu waingie kisiwani ili wakapate maji ya kunywa na kupata hewa safi. Kitu cha kushangaza ni kuwa kisiwa kizima kilikuwa ni mawe. Yaani majimba, miti, wanyama, watu na mikokoteni ni mawe matupu. Hata walinzi wa magetini walionekana kuwa mawe matupu. Kwa hakika huu mji ulikuwa ni wa ajabu sana. Kila mtu alitaka kujuwa habari za mji ule lakini ni nani wa kuwaambia.


Jambo linhine la kushangaza ni kuwa pesa na dhahabu zilikuwa zikizagaa masokoni ambapo watu wake wamegeuka mawe. Watu wa kwenye jahazi walikuwa wakistaajabu na kuanza kukusanya pesa na dhahabu. Kwa upande wangu niliendelea ndani zaidiya mji ule kujuwa zaidi habari. Nilipokwenda nikaingia kwenye ukumbi wa mfalme na nikamkuta amekaa kwenye kiti chke akiwa ni jiwe. Dahabu alizovaa zilikuwa zikining'inia tuu. Nikasogea zaidi na kukuta baraza la malkia likiwa na wanawake wengi nao wakiwa ni jiwe na mapambo yao ya dhahabu yakining'inia tuu.


Kwa hakika nilistaajabu sana na niliendelea pia. Niliona mambo mengi na ya kushangaza. Nilipokuwa kwenye eneo la kulia chakula watu nikuta wamegeuka mawe na vyakula vikiwa vizima hata kuharibika bado. Nikiwa katika hali ya mshangao nikasikia sauti ya mtu anasoma Qurani. Sikuamini hivyo nikasikiliza vizuri sauti ile na kupata uhakika wa kuwa nimesikia vyema. Hivyo nikaanza kuifata sauti ile hata nikaingia kwenye kijichumba kimoja na kumkuta kijana wa kiume mzuri sana. Nilibakia nikistaajabu kwa uzuri wake hata nikasahau yaliyonistaajabisha hapo mwanzo.


Nilimsogelea kijana yule na kumsaalimia kwa salamu ya kiislamu na akaniitikia kwa upole zaidi. Sikuamini kama ni mtu au ni jini hivyo ikabidi nimuulize vizuri. Bila ya wasi akanijibu kuwa yeye ni mtu wa kawaida tu na ni mtu pekee aliyeokoka na janga liliowapata watu wa eneo lile. Kwa shauku nikamuuliza ni kipi basi kilichowapata watu wa eneo lile. Aliniangalia kwa huzuni kisha akaanza kufuta machozi yake na kunza kunisimulia hadithi ya yaliyotokea eneo lile kama ifuatavyo;-


HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.
Mimi ni mtoto wa mfalme wa nchi hii ambayo umemuona amegeuzwa jiwe kama watu wengine. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikilelewa na bibi mmoja laiyekuwa ni muiislamu. Watu wa mji huu walikuwa wanaabudu masanamu hivyo bib i yule alifanya siri imani yake. Na kwa usiri huo akanifundisha imani ya uislamu juu ya mungu mmoja na akanifundisha kusoma Qurani. Katika muda wote niloishi nae yapata miaka 10 alikuwa akinisisitiza kufanya siri imani ile na mambo yakawa hivyo mpaka bibi yule alipofariki.


Mwaka juzi alikuja mtu mmoja hapa nchini kwetu, mtu huyu ulikuwa ikilingania watu kuhusu kumuabudu mola mmoja tofauti na watu walivyozoea. Mfalme aliongea maneno ya ajabu na ya kipuuzi kuhusu sauti ile. Mtu yule aliondoka na akarudi tena mwaka jana na maneno yalikuwa ni yalelyale. Na mfalme yaani baba yangu alirudia maneno yaleyale. Na mara ya tatu mwaka huu alirudi tena Mtu yule na mambo yakawa vile vile.


Wiki mbili baada ya kuondoka kwa Mtu yule ikatokea sauti ikionya na kulingania juu ya imani ya munngu mmoja. Hali ikawa kama mwanzo Mfalme wetu akatoa kejeli na maneno machafu sana. Kwa hakika niliumia na nikataka kwenda kumtia adabu baba yangu mwenyewe lakini nilishindwa kufanya hivyo. Machozi yalinitoka na nisijuwe jambo la kufanya na hakina wa kunishauri. Basi haikupita muda mrefu ile sauti ikatoweka na hapo anga ikafunga kuwa nyeusi kutokana na wingu lisilojuliukana kama la mvua au upepo mkali.


Wingu lile liliendelea kusogea chini hata likakaribia kufunika nyumba. Ulikuwa ni wakati wa muda wa swala ya adhuhuri na watu wamechanganyika katika utaftaji. Wengine wapo masokoni na wengine mashambani na hali kadhalika. Wingu lile likaambatana na upepo mlaini ambao haukuweza kuharibu hata kipande cha nguo kilichokuwa kinaning'inia. Upepo ule uliingia masikion, puani na kila sehemu yenye tundu na kutokea upande mwingine.


Haukupita muda wat wote wakawa katika hali uloiona kuwa mawe. Na kia mtu vile alivyo ndivyo alivyobaki. Hata walokuwa wamelalaq wamebakia mawe kwenye vitanda. Nilitoka kuchunguza zaidi sikuona hata mnyama ambaye aligeuzwa jiwe. Kwa hakika msiba huu uliwapata wanadamu tuu. Basi nikawa sina pa kwenda hiyo nikabakia kisiwani hapa peke yangu kama unavyonioa. Na hii ndiyo historia ya kisiwa hiki kilichogeuzwa mawe.


Wakati kijana anamaliza kusimulia hadithi ile Zubeida akawa analia na machozi yanamtiririka kama chemchem iliyoanzia mlimani. Basi kijana kwa huruma akawa anamfuta machozzi Zubeida. Baada ya muda Zubeida akauliza 'sasa wanyama walikwenda wapi?' kijana akamjibu baada ya kutokea yaliyokwisha tokea ilikuja tena ile sauti na kuniambia kuhusu hatima ya wanyama. 'ama kuhusu wanyama amri yao ipo kwako, eidha utawatumia kama chakula chako mpaka Allah atakapoleta nusra , ama awahamishe awapeleke anakotaka ama wageuzwe kuwa vitu vya thamani na iwe kama zawadi ya Zubeida mwenye kupotea njia mwana wa tairi na msalitiwa na ndugu zake.


Basi nikachaguwa jambo la tatu, na pindi ulivyokuja nilifahamu hakika ni wewe Zubeidah. Zubeida akamuuliza 'ni kitu gani kilichokufahamisha' akaendelea ile sauti niliiulisa sasa ni kwa namna gani nitamfahamu Zubeidah ikajibu siku moja kabla ya kuja kwa Zubeiday bahari itakuwa chafu sana na upepo maini utaingia kisiwani hapa na kusafisha nyia ya Zubeida mwana wa tajiri, msalitiwa. Hivyo Zubeida atakuwa hana jinsi ila atakufikia tu popote utakapokuwepo muda huo. Basi nilipoziona ishara hizo nilifahamu ujio wako hivyo ili kukurahisishia kunipata nikawa nasoma Qurani kwa sauti ya juu ndivyo ukanisikia.


Ama kuhusu kusalitiwa kwa Zubeida na ndugu zake nilishindwa kujuwa mengi zaidi maana sauti ile ikanambia hainipasi kujuwa siri za mambo yajayo. Halikadhalika ninachofahamu zaidi kuhusu huo usaliti ni kuwa maisha yangu ama yako yatakuwa hatarini. Basi Zubeida na yule kijana wakatoka pale na Zubeidah akashauri waoane na wakakubaliana kufunga ndoa punde watakapofika nyumbani.


Basi kijana akampeleka Zubeidah kwenye zawadi yake na akakuta mali nyingi sana na tayari imeshafungwa vizuri kwenye mkokoteni. Basi wakaburuza mkokoteni wao mpaka kwenye chombo chao na kuuingiza ndani. Wakawa wanapunga upepo ufukweni na kubadilishana mawazo na kuchat. Wakiwa katika hali hiyo ghafla akatokea nge anakimbizwa na kunguru Zubeidah akachukuwa kijiwe na kumpiga kunguru na ukawa ndio mwisho wa maisha ya kunguru yule na nge akatokomea kwenye mawe. Na wawili hawa wakaendelea kuzungumza. Wakati yote haya yanafanyika dada zake na Zubeidah walikuwa wakiona wivu na kijicho kwa mafanikio ya ndugu yao.


USALITI UNANZA HAPA
Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Ndugu zake na Zubeidah kumbwe hawakupendezwa na mafanikio ya ndugu yao. Hali hii iliwafanya kuwa na wifu na kijicho. Basi zubeidah akaongea na ndugu zake na kuwapa mali zile zote na kuwambia mimi shida yangu ni kufika salama na huyu kijana ambaye kwa sasa ni mchumba wangu na tutaoana punde tu tufikapo nyumbani. Mali zile wakagawana ndugu wawili hawa.


Hili pia halikutosha wakataka na wawaue kabisa, na kawafanya hivyo katika majira ya usiku. Waliwachukuwa wawili hawa na kuwatia baharini. Anakuja kushituka zubeida yupo baharini anakunywa maji ya chumvi na hatimaye kupoteza fahamu na asijue nini kiliendelea. Basi kwa furaha ndugu wale wakaanza kugawana tena mali zile.


Kwa upande wa Zubeidah alopokuja kupata fahamu ilikuwa ni wakati wa jioni na akajikuta amezungukwa na kundi la wananwke wenye sura nzuri za kuvutia waliojipamba vizuri sana. Mbele yake kuna kiti kirefu sana kilichopamba na magodoro yaliyochovywa kwenye dhahabu nyekundu. Miguu ya kiti hicho ni meno ya tembo yaliyopambwa vizuri. Kwa hakika kiti hicho kilikuwa na kila aina ya mapambo mazuri. Aliponyanyua kichwa akaona amekaa juu ya kiti hicho mzee wa heshima mwenye ndevu ndefu zilizo kaa vyema.


Zubeida kwa mshangao alionekana kufurahia mazingira yale na asijuwe nini kinaendelea. Alikuja msichana wa makamo hivi aliyependeza sana na akampaka maji ya marashi yaliyochanganywa na misk na kutiwa manukato mazuri sana. Zubeidah akarudisha kumbulkumnbu zake zote na akajuwa kwa mara ya mwisho alitumbukia kwenye maji sasa akawa anajiulia yupo wapi?. Yule mzee akamwambia 'mwanangu furahia uwepo wako hapa kwa hakika hupo peponi wala kuzimu, hapa upo chini ya bahari na mbele yako ni mfalme mkuu wa majini yaendayo baharini na nchi kavu. Mzee yule akaagiza kuwa Zubeidah afanyiwe kila kinachostahiki kufanyiwa kisaha akatoweka.


Kwa shauku Zubeida alikuwa na maswali mengi sana, wakaja mabinti watatu waliokuwa na sura nzuri sana hata Zubeidah akajiona yeye si lolote wala si chochote, wakamchukuwa na kwenda nae bafunu. Huko maji yaliyo na umoto kwa mbali yalikwisha andaliwa. Kwa mara ya kwanza Zubeidaha anakwenda kuoga maji yaliyotiwa marashi pamoja na misk nyekundu, manukato mablimbali yenye kuvutia. Zubeidah alijihisi yupo ulimwengu wa raha. Kwa maringo na madaha wakamvua ngu Zubeidah na kumtumbukiza kwenye bafu lile na kuanza kumsuguwa.


Wakaendelea kumsuguwa kwa visugulio vyenye rangi ya silva vilivyochovywa kwenye marjani. Kwakweli utasema mwili wa Zubeidah umekuwa lulu iliyohifadhiwa vizuri. Uchafu wote mwilini mwa Zubeidah uliondoka hata akawa kama akawa kama aliyofanyiwa scrub na kumbakisha kama mtoto alozaliwa. Ngozi laini na nyusi za kupendeza. Hawakuishia hapo wakaendelea kumpmba na kumpaka manukato. Nguo safi za hariri zenye mapindo yalochovywa kwenye dhahabu, hakika siwezi kuelezea zaidi urembo walomchagulia.


MALIPO YA WEMA NI WEMA
Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi. Hapa Zubeida akawa anajiulia kuwa ni nani huyu anakuja? Aua ni yule mchumba wake? Maswali haya hayakupata amjibu. Baada ya muda kupita akatokea binti mmoja mreembi kama mwezi uliokamilika umbo lake. Binti yule akamsogelea Zubeidah na kupiga goti mbele yake na kuukamata mkono wa Zubeidah na kuubusu kisha akamwambia ' NI YAPI MALIPO YA WEMA? KWA HAKIKA NI WEMA TU'.


Lilikuwa ni swali ambalo halihitaji majibu kutoka kwa Zubeidah. Kwa malipo ya wema ni wema, Zubeida akamuuliza 'ni nani wewe ni ni nani mimi na nimefuka vipi hapa?. Yule mrembo akaanza kutoa kisa chake. Kuwa yenye ni mtoto wa mkuu mfalme wa majini ambaye alionana naye hapo mwanzo. Alipokiuwa matembezima jana akiwa amejibadili katika umbo la nge alipokuwa nakimbizwa na adui wake aliyekuwa katika umbo la kunguru alimsaidia kwa kumuuwa adui wake kunguru. Hivyo yule nge alikuwa ni huyu mtoto wa mfalme. Kwa ufupo ni kuwa Zubeidah amemuokoa mtoto wa mfalme katika kizingiti za kifo kuuliwa na adui wake na huu ni wema mabao analipwa.


Basi yule mrembo akamwambia Zubeida kuwa ndugu zako walipokutumbukiza baharini nilikuwepo kwenye jahazi lenu kwa nia ya kuku;inda mpaka ufikapo kwenu. Hivyo nilikuokoa kwenuye ajali ile na sikuweza kumuokoa mchumba wako, kwa hilo naomba unisamehe sana. Hata hivyo baba yangu anaweza kukupa chochote utakacho kiseme utapata, na hata ukitaka utaishi hapa na mimi. Ila kuhusu ndugu zako kwa hakika sitaweza kuwasamehe katu. Nitawapa adhabu kubwa sana nai ningewauwa ila kwa kuhofia chozi lako siwezi kufanya hivyo.


Basi Zubeidah akaitwa na mfalem wa majini yule na kuulizwa nini ameamua kati ya yale aloelezwa na binti mafalme. Zubeidah akachagua kurudishwa nyumbani kwao na hakuhitajia chochote. Basi binti mafalme akampa unywele wake na kumwambia ukiwa na shida na mimi choma nywele hii kwa hakika nitakuja hapo kwa haraka zaidi. Basi kufumba na kufumbua Zubeidah akajikuta yupo nyumbani kwake na mlangoni wamekaa mbwa wawili na kuangalia pembeni akakuta bahasha ambayo imewekwa mlangoni. Kufungua bahasha ile akakuta ndani kuna barua iloandika\wa 'Kutoka kwa Binti Mfalme wa majini ya majini na Nchi kavu kwenda kwa Zubeidah mwana wa tajiri mpotea njia mwenye kusalitiwa. Ama baada ya salamu napenda kukutaarifu kuwa hao mbwa unaowaona mlangoni kwako ni ndugu zako na hiyo ndio adhabu niloichagua. Watabaki hivyo kwa muda wa miaka 10 na utakuwa ukiwapiga fimbo za mijeledi 300 kwa kila mmoja na kila siku. Na kama hautafanya hivyo watakufa siku inayofata. Ama kuhusu mali zako zote nimeziokowa na zipo stoo. Hata hivyo baba yangu amekujengea nyumba karibu jirani na mji wa Mfalme mwadilifu Harun Rashidi mfalme wa Baghdah. Huko uende na ukakae na ndugu zako hao. Usisahau kufanya nilichokwambia Zubeidah.'


Hivyo Zubeidah akachukuwa mali zake na kuhamia katika nyumba ile aloambiwa mjini Baghdad na ndugu zake. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mbwa wakawa wanatoa machozi mengi sana na hata mfalme akawa anatoa machozi. Hivyo hii ndi sababu ya mimi kuwaadhibu mbwa hawa kila siku yalikuwa ni maneno ya Zubeidah. Mfalme baada ya kusikiliza hadithi hii akamgeukia Amina aliyekuwa na alama na makovu kwenye mwili wake na mumwambia aeleze hadithi yake, nae akaanza kama ifuatavyo;-


HADITHI YA BINTI WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE AKOVU.
basi juwa ewe mfalme wetu kuwa nilikuwa naishi na wazazi wangu na hatimaye wakanitoka na kuniwacha peke yangu. Niliachiwa mali za kunitosheleza kuishi kwa muda mrefu bila ya kuomba. Wate wengi walinisifi kwa uzuri nilio nao ijapokuwa nilihisi wananitania tuu siku nilipokuta na na Zubeidah kwa hakika alikuwa mzuri zaidi. Nili kaa pale nyumbani kwa muda mrefu niliwa peke yangu bila ya mume.


Sikumoja alikuja bib mmoja na kuniambia kuwa mjukuu wake anashuhuli na hakuna mtu wa kumsimamia shuhuli yake hivyo akanitaka niwe kama msimamizi wa mambo ya wananwake kwenye shuhulu hiyo. Basi niliongozana na bibi yule hata tukafika mwenye shuhuili ile na mambo yakaenda salama. Ilikuwa ni shuhuli ya kuwakumbuka walotanguluia kufa kama kawaida ya waislamau wanavyoifanya mjini pale. Basi shuhuli ilipokwisha yule bibi akaniita katika chumba cha ndani na bila ya kuwa na wasiwasi nikaenda. Kufika kule ndani nikakutana na kijana mmoja aliyekuwa mtanashati na katika mazungumzo akaniposa na mimi nikakubali. Kumbe lile ndo lilikuwa lengo la yule bibi toka mwanzo.


Basi maandalizi ya harusi yalifanyika na nikaolewa mwezi ulofata. Kwa hakika ndoa yetu ilikuwa ni njema na haina migigoro kwa muda wa miezi sita ya mwanzoi. Ama mimi sikuruhusiwa kutoka nje, hata sikuhiyo niikaomba ruhusa ya kuenda sikoni kununua mahitaji yangu binafsi na mume wangu akaniruhusu. Kule sokoni wakati narudi anilikutana na mlevi mmoja na tulipokuwa tunapishana akaning'ata kwenye shavu. Kumbe alikuwa ni mmtoto wa baba yangu mdogo ambaye nilimkatalia kunioa aliponiposa.


Wakati haya yote yanafanyika mume wangu alikuwa amejibanza na alikuwa anaona. Na pia alitambua pika kuwa yule alikuwa nai mtoto wa baba yangu mdogo. Na alidhani kuwa ni mzinifu mwenzangu nilipokuwa naishi peke yangu kumbe sivyo. Basi niliporudi nyumbani akaniuliza sababu ya kidonda kwenye shavu langu nikamjibu nimegongana na mkokoteni, basi akasema nitamtafuta huyo mwenye mkokoteni na nitamua, nikamwambia usimuue mtu asiye na hatia kwani ni ajali tu.


Basi akanikaba shingoni na kuniuliza kwa zaidi sababu ya kidonda kule na kunmbia anajua nimeng'atwa na mzuiinifu mwenzangu wa zamani basi akaamrisha nikakamatwa vizuri na na akaanza kinipiga fimbo za mijeledi mpkaka nikapoteza fahamu. Nilipozinduka akanifukuza na pale kwake na kufika nyumbani kikakuta nyumba yangu ameobomoa bomoa a nikakutana na Zubeidah kwa mara nyingine na kukubaliana kuishi pamoja. Niliendelea kuuguza vidonda vyangu hata nikapona na kubakia makovu ndio uloyaona. Hii ndia hadithi yangu ewe mfalme.


Basi mfalme akamgeukia Sadie na kumwambia azungumze hadithi yake na kusema kuwa yeye alikuwa ni mtoto yatima ombaomba ambaye alikutana na Zubeidah na kumkirimu kama dada yake na nikamkuta min anaishi nae pia, hatukuwahi kuzungumza hadithizetu kama hivi. Hivyo hii ndio hadithi yangu ewe mtukufu muadilifu mfalme wa Baghdad; harun Rashid.


Baada ya kusikiliza hadithi za mabinti hawa, Mfalme nae akaamua kufungua mdomo wake kwa kuwauliza maswali 'hivi mnafikiri kuwa kila mtu ana hadithi za kusisimua katika yale yalowapata kwenye maisha?' Zubeidah akajibu 'naam kwa hakika ana kila mmoja hadithi ya kusisimua katika maisha yake, aaanhaa nadiriki kusema hata wewe Mfalme unayo yako ijapo hatuwezi kukwambia utueleze'. Mfalme alimuangalia sana Zubeidah kisha akasema 'naam hata mimi na waziri wangu tuna hadithi yetu, na leo nitaisimulia kwenu hadithi ambayo katu hatujawahi lkuisimulia.' basi Mfalme nae akaanza kufungua mdomo kwa kusimulia hadithi yake.


HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE
Basi tambueni enyi rafikizangu kuwa mimi na waziri wangu huyu hatutokani na familia za kifalme wala mimi baba yangu hahusiani hata kidogo na ufalme. Tumepata vyeo vyetu hivi wakati tukiwa katika hali ngumu ya maisha. Mimi na waziri wangu tulipata vyeo vyetu tulipojifanya tunaswali baada ya kukimbizwa kuwa wezi tulipokuwa tunaiba msikitini. Bila shaka hamjaelewa nini ninamaanisha. Ila kwa ukweli zaidi mambo yalikuwa hivi


Tulikuwa ni watoto yatima tuliofiwa na wazazi wetu tungali wadogo. Sikuzote tuliitegemea chakula kwa kuokota ama kuomba. Tulianza tabia ya wizi, ingali tunajuwa kuwa wizi ni haramu, na ukikamatwa utakatwa mkono kwa mujibu wa sheria za dini. Tukiwa hatuna jinsi ya kutupatia rizki tulikuwa tukiiba vitu kwa watu na kuuza kujipatika pesa.i mwingine tunanakosa hata cha kuiba hivyo tunalala bila kula. Wakati mwengine tulikuwa tukipigwa pindi tunapokwenda kuiba.


Tulianza kujishughulisha na shuhuli za kufanya biashara ndogondogo ijapokuwa hali haikuwa nzuri pia. Tuliamua pia kujikita katika kibeba taka majumbani hali ambayo pia haukuwa na uwezo wa kutufanya tupate riziki kwa unafuu. Kwa hakika maisha yetu yalikuwa ni magumu sana. Hatukujuwa kusoma wala kuandika. Na kwa bahati mbaya tulisomaga dini tukiwa watoto na kukimbia masomo hivyo tulifanikiwa kujuwa kuswali na mambo machache tuu.


Wakati mwingine tulijiingiza katika misafara ya walinganiaji dini na kujifanya na sisi tukilingania, ila lengo ni kupata unafuu wa maisha lakini tulipogundulika tulikuwa tukifukuzwa. Maisha yaliendelea kuwa ni magumu. Unapoingia mwezi wa ramadhani sisi kwetu ilikuwa ni kama sikukuu maana tuliweza kushiba kwa kufuturishwa na mabaki ya ftari kwa matajiri na wenye uwezo tuliweza kuyatumia. Ila mwezi unapoisha hali ilirudi vilevile.


Basi mambo yalikuwa hivyo na masiku yakawa yanaendelea. Ilitokea sikumoja tulikosa cha kukila na tukakosa hata nafasi ya kuiba kiti chochote cha kutuingizia kipato au kutunisha matumbo yetu. Basi siku ile tuliamua kuingia msikitini na kuanza kufungua vibubu na masanduku ya sadaka pale msikitini ili kuiba sadaka. Haikupita muda tukasikia miguu ya watu wanakuja hivyo tulishindwa kuwahi kujificha na tukaamua kujifanya tunaswali. Mimi nikiwa imamu na waziri wangu huyu alikuwa ni maamuma katika swala yetu feki.


Basi kundi lile likaja mpaka msikitini na walip[otuona tunaswali wakawa wanatunyooshea vidole na wengine wakawa wanasema hawa ndo wenyewe, hawa ndo wanafaa. Basi nikiwa imamu wa swala feki nilijitahidi kurefusha swala lakini wale watu hawakukata tamaa na wakaendelea kusubiri. Hatimaye nikakata tamaa na kumaliza swala ile. Basi tulipotoa salamu tu wale watu wakatuita na kutuchukuwa kwenda kwa mfalme na kutuambia kuwa mfalme anatuita.


Kwakweli hatujawahi kuiba kwa mfalme hata siku moja hivyo tulipata woga sana na kuhisi leo ndo mikono yetu inakwenda kukatwa. Tulipofika kwa mfalme wale watu mmoja wao akasema 'muheshimiwa mfalme tumetafuta sehemu zote kwa siku nyingi lakini tumewapata hawa, na huyu alikuwa ndo imamu na mwenzie maamuma. Bale nilitamani kumwambia sisi sio wezi lakini nikasubiri kuona hatima yetu. Mfalme alifurahi kusikia vile na akaniambia ninakuozesha mwanangu. Nilishangaa kuona mfalme anasema maneno yale mbele ya wezi. Nikamuuliza sababu ya kufanya hivyo. Mafalme akanijibu kuwa yeye hana mtu wa kumrithi na ana mtoto wa kike tu, hivyo alikuwa akitafuta mtu wa kumuoa binti yake kwa sharti kuwa mtu hiyo awe anaswali hasa awe anaswali sunnah za usiku. Hivyo watu wake hawakupata mwenye sifa hiyo ila ameniona mimi,


Hapo nikamwambia mflme naomba muda kidogo, basi nikatoka nje na kuchukuwa udhu kisha nikasujudi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema alonipa. Yaani kwa swala feki ile amenipa neema ya kuwa mfalme je ingelikuwa ni swala ya kiukweli ni neema kiasi gani angenipa? Basi nikarudi kwa mfalme na kumwambia nimekubali. Na hapo ndoa ikapita na nikamuoa binti mfalme.


Kuanzia pale mimi na mwenzangu tukasahau wizi na haukupita muda mfalme alifariki na mimi nikawa mfalme wa nchi hii na rafiki yangu huyu nikamfanya kuwa waziri mkuu. Hivyo kwa kuwa tunatambua machungu ya maisha tumekuwa tukijitahidi kusaidia raia na tulikuwa tukitembea usiku kuona hali halisi ya maisha na kuwatambua wezi. Huwa tukiwapata wezi tunawapa kazi ili kuwasaidi. Hivyo imetokea jana tulipokuwa tukifanya uchunguzi wetu tukapita nyumbani kwenu. Hii ndio hadithi yangu na waziri wangu.


USULUHISHAJI WA WALODHULUMIWA.
Basi baada ya kusikiliza hadithi hizi mfalme akaanza usuluhishi na kumwambia Zubeidah achome huo unywele ili amuite jini binti mfalme. Basi Zubeidah akauchoma huo unywele na baada ya punde akaja jini yule na mfalme akataka msamaha kwa mabinti walogeuzwa mbwa, basi akawambwagia maji na wakageuka kuwa watu. Pia bint mfalme akazungumza kuwa alomfanyia unyama Amina ni mwanao mwenyewe ewe mfalme ni kuwa mtoto wako alimpenda Amina na kumposa na ndoa aliifanya kwa siri na hatimaye mambo yakawa hivyo. Basi jini akaondoka.


Mfalme akamuita mwanae na kumuuliza yalotokea na akamjibu kama mambo yalivyo elezwa. Basi akatoa amri mrejee mkewe na kisha Zubeidah ana dada zake akawaozesha kwa wale machongo watatu na yeye mwenyewe mfalme akamuoa Sadie. Inasemekana ndoa zao zilikuwa ni za upendo wa hali ya juu na hakukutokea ugomvi mpaka Allah akapitisha amri yake.


Baada ya Schehra-zade kumaliza kusimulia hadithi hii Dinar-zade alifurahi sana. Lakini furaha hii haikumzidi sultani. Hapo Schehra-zade akamwambia basi hadithi hii haifiki hadithi ya Sinbad mwenda baharini. Sultani akuliza ni kipi kilompata sinbad mwenda baharini hata hadithi yake ikawa nzuri hivyo? Hapo Schehra-zade akaanza kusimulia hadithi hii;-



Pata kitabu Chetu Bofya hapa

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 240

Post zifazofanana:-

Maana ya Kuamini Mitume wa Allah (s.w) katika maisha ya kila s iku.
Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s. Soma Zaidi...

Masomo ya Dua na Faida zake Dua
Soma Dua mbalimbali hapa, Soma Zaidi...

English tenses test 005
Soma Zaidi...

Kiwango cha mahari katika uislamu
Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari? Soma Zaidi...

Vyakula vya fati na mafuta na kazi zake
Soma Zaidi...

Kuandaliwa Mtume(s.a.w) maandalizi ya kimafunzo na maandalizi ya ki ilham
Mitume huzaliwa Mitume. Soma Zaidi...

Faida za kula Nazi
Nazi ni katika matunda bora sana kiafya, Soma faida zake kwa afya yako Soma Zaidi...

SABABU YA NENO LAKO
Sababu ya neno lako, nasema nimesikia,Sababu ya neno lako, nasema hongera pia,Sababu ya neno lako, nishajua yakonia,Wasema afukuzwae, sihadi pasemwe toka,Sababu ya neno lako, maumivu yanijia,Sababu ya neno lako, nami leo nakwambia,Sababu ya neno lako, sit Soma Zaidi...

dharura
14. Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

Nadharia ya uchumi kiislamu
1. Soma Zaidi...

English tenses test 006
Soma Zaidi...