Makundi ya watu walio katika hatari ya kupata Ugonjwa wa Ukimwi

Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,ni kutokana na kazi zao pamoja na mazingira yao kwa hiyo wako kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa ukimwi.

Makundi ya watu ambao wako hatarini kupata Ugonjwa wa Ukimwi.

1.Wanaofanya biashara ya ngono.

Kuna baadhi ya wasichana ambao wanafanya biashara ya kuuza miili yao wako hatarini kwa sababu wanakutana na watu mbalimbali na kwa wakati mbalimbali na pengine wana bei za kuuza ngono ,kuna bei kama hauna kondomu na bei kama una kondomu kwa hiyo walio wengi wanapenda bei kama hakuna kondomu na kwa hiyo haiwawezi kujua nani ni mwadhirika na nina sio mwadhirika kwa hiyo ni rahisi kusambaa kwa ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

2.Wanaofanya ngono za jinsia moja yaani wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume kwa hiyo hawa mara nyingi hawatumii kinga na pia ubadilisha wachumba kutokana na kusafiri au kuhama ambapo mtu akihama anatafuta mchumba mwingine ambaye anafanya kazi hiyo hali inayosababisha kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi.

 

3.Watoto yatima na watoto wa mitaani.

Kwa kawaida hawa watoto uishi kwa kutegemea watu wengine kwa hiyo kuna wakati ambapo wanaitwa na watu kwa lengo la kupata msaada na hatimaye kurawitiwa kama ni wavulana au kubakwa kama ni wasichana hali ambayo Usababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa na Ukimwi.

 

4.Wanaofanya kazi migodini na ziwani .

Kwa kawaida hawa ni watu ambao wanapata Ela za kila siku kwa sababu ya biashara zao kwa hiyo utumia pesa hizo kwa ajili ya kuonga na kusababisha kuongezeka kwa Maambukizi ya virus vya ukimwi kwa hiyo kila siku huwa wanabadilisha wanawake au wanaume kwa kigezo cha kupata pesa na mahitaji mbalimbali.

 

5.Wanaume ambao hawajatahiriwa.

Kwa kawaida wanaume ambao hawajatahiriwa wana asilimia sitini ya kutopata Maambukizi kwa sababu ya kutokuwepo kwa ngozi ya juu ya uume ambayo utunza wadudu, lakini wanaume ambao hawajatahiriwa wana uwezekano wa kupata ukimwi kwa sababu ya ngozi iliyo kwenye sehemu zao za siri kuwa na wadudu wanaosambaza Maambukizi.

 

6. Kwa hiyo tunajua wazi kwamba ukimwi unaua tuendelee kutoa elimu kwa makundi haya ili kuweza kupunguza kiwango cha maambukizo na vifo vinavyotokea kila siku na kila wakati.

.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/12/Tuesday - 03:04:43 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1125


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-