MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)

MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)

Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik.

MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)

PAMBANA NA MALARIA KWA KUMTAMBUA MDUDU MBU (MOSQUITO)

 

Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Mbu anafahamika kwa kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa malaria pamoja na matende na ngiri maji. Chakula cha mbu ni maji, bakteria pamoja na damu. Mbu dume huweza kumjua mwanamke kwa kutumia sauti ya mbawa. Mbu ni katika wadudu wadogo lakini wana maajabu makubwa. Katika mkala hii tutaangalia kwa ufupi mambo matano kuhusu mbu.

 

Tofauti na kuwa mbu ni mdogo lakini anaweza kunyonya damu iliyokuwa nzito kuliko mwili wake. Yaani sawa na mtu mwenye uzito wa kilo 70 kula chakula chenye uzito wa kilo 100. mara mbu anaponyonya damu mwili wake huchukuwa mpaka siku tatu kuweza kuimeng’enya damu ile na kuimaliza. Baada ya hapo mbu atakwenda kunyonya damu tena. Itambulike kuwa chakula cha mbu ni bakteria, maji pamoja na damu. Mbu jike hula damu pindi anapotaka kutaga. Wataalamu wanaeleza kuwa kuna aina 2000 za mbu.

 

Kabla ya mbu kutaga mayai yake anaanza kupima ardhi kama ina majimaji pamoja na joto la kutosha kwa maisha ya mayai yake. Mbu hutaga mayai juu ya maji, ardhi, miti na nyasi pamoja na maeneo mengine yaliyo na majimaji. Pia mbu anaweza kutaga yai lake hata pakiwa na maji kiasi cha tone moja tu. Nayai ya mbu ni chakula kwa samaki pamoja na watutu wengine hivyo mbu huwa makini sana wakati wa kutaga mayai yake.

 

Tofauti na wadudu wengine na ndege mbu anaweza kulizuia yai lake tumboni kulitaga pindia anapohofia usalama wa yai lake. Kuku na ndege wengine yai linapofikia kutagwa hana namna lazima akalitage, lakini hii ni tofauti kwa mbu. Yai la mbu linaweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila ya kufa na ndo maana ni vigumu kutokomeza kabisa mbu.

 

Yai la mbu lina rangi ya njano, tangi hii ni rahisi kulifanya yai hili lionewe na maadui walao mayai ya mbu. Hivyo ifikapo usiku yai la mbu hubadilika rangi na kuwa jeusi. Hali hii husaidia kuliepusha yai la mbu kuliwa na maadua. Pia yai la mbu halizami ndani ya maji, na linaweza kuelea hewani, njia zote hizi husaidia ulinzi wa yai hili lisidhuriwe.

 

Ijapokuwa mbu anakula binadamu lakini na yeye ni chakula kwa viumbe vingine kama popo. Hivyo popo hutusaidia katika mapambano dhidi ya wadudu hawa hatari. mbu pia anaweza kujuwa wati mtu yupo kwa kutumia pumzi anayopumua mwanadamu



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 3323

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 web hosting     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Maziwa ya mama: Faida zake kwa afya ya mtoto.

Maziwa ya mama, yanayojulikana kitaalamu kama "dhahabu nyeupe," ni chakula kamili na cha kipekee chenye virutubisho vyote vinavyohitajika na mtoto katika miezi sita ya kwanza ya maisha yake. Yanatengenezwa na mwili wa mama kulingana na mahitaji halisi ya mtoto, yakibeba kingamwili, vitamini, na madini muhimu. Makala hii inaangazia faida za kipekee za kunyonyesha kwa afya ya muda mfupi na mrefu ya mtoto.

Soma Zaidi...
Fahamu Ugonjwa wa Maambukizi kwenye mfupa

posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi kwenye mfupa ambao kitaalamu hujulikana Kama

Soma Zaidi...
Maajabu ya damu na mzunguuko wake mwilini.

Ukistaajabu ya Musa utastaajabu ya Firauni. Haya ni maneno ya wahenga. Sasa hebu njoo u staajabu ya damu

Soma Zaidi...
Fahamu aina mbalimbali za Magonjwa nyemelezi ya moyo

Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za Magonjwa ya moyo,kwa kawaida tunajua wazi kuwa kuna moyo mmoja lakini moyo huo unaweza kushambuliwa na magonjwa kwa kila aina kwa mfano kuna Maambukizi kwenye mishipa ya moyo,au kubadilika kwa mapigo ya moyo na m

Soma Zaidi...
Dalili za mtoto Mwenye UTI

Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.

Soma Zaidi...
Magonjwa ya moyo

Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya moyo, kwa kawaida watu wakisikia habari za magonjwa ya moyo huwa hawaelewi yanakuwaje kuwaje, Leo nataka niwafahamishe kuhusu magonjwa ya moyo na sehemu mbalimbali zinazoathirika.

Soma Zaidi...