Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako
3.Palachichi (avocado)
Hili ni katika matunda yenye fat (mafuta). Itambulike kuwa si kila mafuta ni hatari ndani ya miili yetu. Tunahitaji vyakula vya fat yaani mafuta kwa ajili ya kutupatia joto kwenye miili yetu. Pia fati husaidia kuipa miili yetu nguvu. Katika tunda hili palachichi mafuta yake ni aina ya oleic acid yaani yapo katika aina flani ya asidi ambayo husaidia katika kupunguza uvimbe mwilini na kusaidia kuboresha afya ya moyo.
Palachici pia hutambulika kitaalamu kuwa lina lina madini ya potassium na magnesium kwa wingi sana. Pia ni katika vyakula vyenye kambakamba yaani fiber. Vyakula hivi vyenye fiber husaidia katika kuweka usalama wa tumbo yaani kuhakikisha chakula kinatembea ipasavyo ndani ya tumbo kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine mpaka kufika kwenye njia ya haja kubwa.
Pia tunda hili husaidia kupungusa hatari za kupata maradhi ya stroke yaani kupalalaizi kutokana na kiwango kikubwa cha madini ya magnessium ambayo husaidia katika kupunguza shinikizo kubwa la damu. Hivyo palachichi husaidia katika kudhibiti afya ya moyo. Palachichi moja linaweza kutoa 28% ya mahitaji ya mwili ya madini haya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kungumanga/nutmeg
Soma Zaidi...Zijuwe sababu kuu za kuwepo kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula
Soma Zaidi...Kwa nini hutakiwi kumpa mtoto wa umri wa chini ya mwaka mmoja kumpa asali?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mapema, kwa sababu ya kuwepo kwa saratani ya matiti, kuna dalili ambazo zikijitokeza zinapaswa kutolewa taarifa mara moja bila kuchelewa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kungumanga
Soma Zaidi...