picha

Faida za kula ukwaju

Uchachu wa ukwaju, ndio ubora wake, kuna virutubisho vingi kwa kula ukwaju, soma makala hii

Faida za kula ukwaju

22. Faida za ukwaju (Tamarind)
Ukwajju ni katika mimea ambayo matunda yake yanatumika katika kutengenezea madawa ya hospitali. Kinywaji cha ukwaju hutumika katika kutibu kuharisha, kukosa choo, homa na aina za vidonda vya tumbo. Tofauti na matunda pia majani na maganda ya mti huu pia hutumika katika kutibu vidonda. Wataalamu wa afya bado wanaendelea kuuchunguza mti huu kwa ajili ya kupata tiba zaidi.

Antioxidant ambayo ipo kwenye ukwaju husaidia katika kudhibiti na kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo, saratani na kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa ukwaju husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Pia kwa watu wenye kutaka kupunguza uzito, ukwaju pia husaidia.

Ukwaju una virutubisho vingi sana kama vile:- madini ya magnesium, potassium, chuma, calcium na phosphorous. Pia kuna vitamin B1 (thiamin), vitamin B2 (riboflavin), vitamin B3 (niacin). pia kuna vitamin C, k na B6 na B5. kwa ufupi ukwaju ni katika matunda ya asili yalotumiwa na watu toka zamani sana.

Katika ukwaju kuna polyphenols kama vile flavonoids ambayo husaidia katika kudhibiti kiwango cha cholesterol na triglycerides. Antioxidant zilizomo kwenye tunda hili husaidia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo. Pia ukwaju husaidia katika kutengeneza dawa za malaria.

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa ukwaju husaidia katika kupunguza uzito. Itambulike kuwa kuzidi uzito mwilini kunahusianishwa sana na maradhi ya moyo, ini, na figo. Hivyo ukwaju husaidia katika kupunguza choloesterol mbaya (LDL) na husaidia katika kuongeza cholesterol nzuri (HDL).

Ukwaju una potassium bitartipate ambayo hii husaidia katika upatikanaji wa choo na kuzuia kuganda kwa choo. Mizizi na maganda ya mkwaju husaidia sana kwa maumivu ya tumbo. Uw.epo wa procyanidins kwenye ukwaju husaidia katika kulinda ini dhidi ya uharibifu. Pia ukwaju hutumika katika kutibu along’atwa na nyoka.


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 6538

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Vyakula vyenye protini kwa wingi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vyenye protini kwa wingi

Soma Zaidi...
Yafahamu magonjwa nyemelezi kwa watoto chini ya miaka mitano

Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,. Ni magonjwa yanayowapata watoto wadogo kwa sababu kinga Yao bado ni ndogo.

Soma Zaidi...
Ulaji wa protini kupitiliza

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za ulaji wa protini kupitiliza

Soma Zaidi...
Vyakula salama na vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo

Kamala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Soma Zaidi...
Zijuwe faida za kula njegere

zijuwe faida za kula njegere kiafya na umuhimu wa kula jegere pia jifunze njegere zina kazi gani mwilini?

Soma Zaidi...
Faida za kitunguu thaumu

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kitunguu thaumu

Soma Zaidi...