Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA TENDO LA NDOA

 

Mara nyingi maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa sio tatizo sana kiasi cha kuogopa. Kwani hali hii husababishwa na gesi iliyoppntumboni mama kama uume ulikuwa ukiingia ndani sana, na hii hutokea endapo uume ni mrefu sana ama mtindo uliotumika katika tendo la ndoa. Tatizo la kupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa ama baada hutambulika kama dyspareunia.

 

Inakadiriwa kuwa asilimia 10 mapka 20 ya wanawake huweza kusumbuliwa na tatizo hili. Ila pia tatizo hili si kwa wanawake tu hutokea pia kwa wanaume, ila kwa kiasi kidogo yapata lamda asilimia 5. lakini tatizo hili linatibika bila ya wasi hivyo si vyema kuendelea kuteseka.

 

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.Tofauti na sababu ya ya gesi ama uume kuingia ndani sana, tatizo hili linaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:-

 

1.Fikra, hisia na mawazo ya mtu. Hii hutokea kama mtu ana misongo ya mawazo kibao, ama ana woga juu ya tendo la ndoa ama mahusianao yake na ya mwenzie sio mazuri lamada amembaka ama kumlazimisha, haya yote yanaweza kutengeneza mazingira ya kuumwa na tumbo baada ya tendo.

 

2.Endapo tendo la ndoa litafanyika kwa kiasi kuwa uume uliingia ndani sana. Hii inaweza kusababisha maumivu ya tumbo, ila ni ya muda mfupi na yataweza kuondoka baada ya kupumzika. Ni vyema kubadili mikao ama kupunguza kukandamiza sana uume.

 

3.Wakati mwingine hali huweza kutokea endapo mwanamke ameingia kileleni. Wakati wa kufika kileleni misuli inayozungukia mfumo wa uzazi, maeneo ya kiunoni na nyonga misuli hii kusinjaa na kujikaza na kusababisha maumivu ya chini ya tumbo. Hali jii kitaalamu hufahamika kama dysorgasmia.

 

Watu wanaosumbuliwa sana tatizo hili ni:-A.WajawazitoB.Wenye matatizo kwenye ovariC.wenye mashambulizi ya kwenye mfumo wa uzazi (PID)D.Wenye matatizo kwenye korodani.

 

4.Gesi; wakati wa kupushi uume ndani unaweza kupushi hewa kuingia ndani ya tumbo. Sasa kama hewa hii itanaswa sehmemu humo ndani inaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa juu ama kifuani. Mtu anaweza kuhisia kama gesi inatembea tumboni na maumivu haya yanaweza kuelekea maeneo mengine ya mwili.

 

5.Kama mtu anasumbuliwa na UTIUTI inaweza kuwa ni katika sababu za maumivu haya. Mtu pia anaweza kuhisi dalili kamaA.Maumivu wakati wa kukojoa kama anaunguaB.Kukojoa mara kwa maraC.Mkojo kuwa mchafuD.Kuwa na damu kwenye mkojoE.Maumivu ya mkundu.

 

6.Kuwa na maradhi ya ngono kama gonoria na chlamydia. Pia mtu anaweza kuona dalili kama:A.Kutoa harufu mbaya sehemu za siriB.Kutokwa na uchafu sehemu za siriC.Maumivu wakati wa kukojoa

 

7.Kama mfuko wa uzazi umeinama, hii inaweza kupelekea kuguswa kwa mfukowa uzazi wakati wa tendo la ndoa hivyo kupelekea maumivu

 

8.Kama kunashida kwenye ovari

 

9.Kama kuna uvimbe kwenye kizazi. Dalili zake ni kamaA.Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhiB.Hedhi kutokata ndani ya siki 7C.Kukosa chooD.Maumivu ya miguu ama mgongo

 

10.Kama mirija ya falopia imeziba.

 

11.Kama mwanaume ana maradhi kwenye mfumo wa uzazi.

 

?

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/10/Wednesday - 09:39:35 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1501

Post zifazofanana:-

Sababu za kushuka Surat al Kafirun
Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto. Soma Zaidi...

Dawa ya fluconazole kama dawa ya fangasi
Post hii inahusu zaidi dawa za fangasi na matumizi yake kwa kutumia dawa ya fluconazole kama dawa mojawapo ya fangasi. Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa uvimbe na mashambulizi ya bacteria kwenye korodani
Posti hii inaonyesha dalili,Sababu,na namna ya kujikinga na ugonjwa wa uvimbe na mashambulizi ya bacteria kwenye korodani ambao kitaalamu hujulikana Kama orchitis. Soma Zaidi...

Kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa,ni Dalili ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha estrogen kwenye mwili ukilinganisha na homoni ya projestoren. Soma Zaidi...

Namna ya kuangalia Maambukizi kwenye mifupa.
Posti hii inahusu zaidi njia zinazotumika ili kuangalia Maambukizi kwenye mifupa. Soma Zaidi...

Kutokwa maji yan seminal swhemu za siri kwa mwanamke nidalili ya ugojwa gan?
Kutokwa Majimaji sehemu za siri kwa mwanamke sio jambo la kushangaza na kuhisivunaumwa. Majimajivhaya ndio huboresha afya ya uzazi kwa kusafisha na kulinda via vya uzazi. Lakini majimajivhaya yakiwa mengi, ama yanawasha ama yanaharufu haa ndipo kwenye tat Soma Zaidi...

Mambo ya lazima kufanyiwa maiti ya muislamu
Mambo ya faradhi kuhusu maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Madhara ya fangasi ukeni
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za Siri za mwanamke husababishwa na fangasi wanaoitwa CANDIDA ALBICANS pia maambukizi haya hujulikana kama YEAST INFECTION. Pia hupatikana katika midomo, mpira wa kupitisha chakula,kibofu Cha mkojo ,uume na uke. Soma Zaidi...

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume.
Tatizo la nguvu za kiume linawwza kuzuiliwa ama kupunguzwa kwa kutumia muunganimo wa njiankadhaa kama kubaduki vyakula, kutumia dawa, kupata ushauri kwa wataalamu wa afya ya mahusiano ama kufanya nazoezi. Je na wewe unasumbuliwa na tatizo hili? Makala hii Soma Zaidi...

Matatizo ya tezi dume hazijashuka.
Posti hii inaonyesha matatizo ya tezi dume zilizoshuka. Soma Zaidi...

Tango (cucumber)
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula tango Soma Zaidi...

Zijue dalili za upungufu wa maji mwilini
Posti hii inaelezea kuhusiana na upungufu wa maji mwilini Soma Zaidi...