MFUMO WA ULINZI NA USALAMA KATIKA FOLA YA UISLAMU MADINAH


image


Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)


  • Mfumo wa Ulinzi na Usalama katika Dola ya Kiislamu Madinah.

Dola (serikali) ya Kiislamu Madinah iliposimama na kuanza kazi za kuongoza jamii iliandamwa na maadui wa kila aina. Mtume (s.a.w) aliweka mikakati na mbinu madhubuti za kuilinda na kuihami serikali yake ikiwa ni pamoja na;

 

  1. Misafara ya Kujihami (Patrol) na Upelelezi.

Mtume (s.a.w) aliweka watu maalum kwa ajili ya kulinda mipaka ya Dola na kupeleleza harakati za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu.

Rejea Qur’an (4:71).

 

  1. Kuweka Mikataba ya amani.

Mtume (s.a.w) aliweka mikataba ya amani na makabila ambayo hayakusilimu yaliyopembezoni mwa Dola ya Kiislamu kama, Banu Dumra, Mudlaj, n.k.

Rejea Qur’an (9:13-15).

 

  1. Kupigana vita.

Njia hii ililazimika kutumika baada ya kuzidi uonevu, dhuluma na choko choko za wazi dhidi ya Waislamu na Uislamu.

Rejea Qur’an (2:193), (9:111) na (9:29)

 

  1. Sera ya wazi juu ya wanafiki.

Mtume (s.a.w) alichukua tahadhari na hatua dhidi ya wanafiki waliojidhihirisha wazi kutengana na ummah wa waislamu kwa kuwatenga.

Rejea Qur’an (9:73), (9:84) na (9:80).

 

  1. Sera ya Uislamu juu ya amani.

Mtume (s.a.w) alitekeleza na kuelekeza mafundisho ya Uislamu juu ya kutunza na kulinda amani kama fursa na dhamana katika kueneza Uislamu. 

Rejea Qur’an (8:61), (16:90), (2:84), (8:5-8).



 

  1. Uhusiano wa Kiplomasia na nchi za nje.

Mtume (s.a.w) aliweka sera ya wazi juu ya uandikashaji na utekelezaji wa mikataba mbali mbali na maadui wa Uislamu kama Aqaba, Hudaybiyah, n.k.

Rejea Qur’an (5:8), (42:40-42), (60:8).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za Imani (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

image Kuamini siku ya mwisho
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

image Umuhimu na nafasi za hijjah katika uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Wanaostahiki kupewa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kwa nini Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?
Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu) Soma Zaidi...

image Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

image Kumkafini (kumvisha sanda maiti)
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mali zinazojuzu kutolewa zaka, nisaab yake na viwango vyake
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...