MGAWANYIKO WA ELIMU KWA MTAZAMO WA KIKAFIRI


image


Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera.


Katika akafiri na hata baadhi ya Waislamu kutokana na mtazamo wao finyu juu ya maana ya dini iliyowapelekea kuyagawanya maisha ya binaadamu kwenye matapo mawili; maisha ya dini na maisha ya dunia, wameigawanya elimu kwenye matapo hayo mawili.

 

Kwa mtazamo huu potofu elimu ya dini ni ile inayoshughulikia maswala ya kiroho (spiritual life) ya mtu binafsi inayoishia katika kumuwezesha mtu kuswali, kufunga na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi bila ya kuzihusisha na maisha yake ya kila siku ya kibinafsi, kifamilia na kijamii.

 

Hivyo elimu hii haina nafasi ya kumuwezesha binaadamu kuendea maisha yake ya kila siku ya kijamii.

 

Elimu ya Dunia kwa mtazamo huu wa makafiri, ni ile inayojishughulisha na masuala ya kijamii kama vile uchumi, siasa, utamaduni, sheria na maongozi ya jamii kwa ujumla kwa kufuata maelekezo na matashi ya binaadamu bila ya kuzingatia mwongozo wa Allah (s.w).

 

Kwa mtazamo wa mgawanyo huu, elimu ya dini ndiyo iliyofundishwa na Allah (s.w) kupitia kwa Mitume na Vitabu vyake na elimu ya dunia imebuniwa na binaadamu wenyewe kwa msukumo wa matashi na mahitaji yao katika kuendea kila kipengele cha maisha yao ya kimaada (Physical or Material life)



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Umbile la mbingu na ardhi linavyothibitisha uwepo wa Allah
Allah anatutaka kuchunguza umbile na mbingu na ardhi ili kupata mazingatio. Soma Zaidi...

image Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia
Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia. Soma Zaidi...

image Nafasi ya Elimu katika uislamu
Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu. Soma Zaidi...

image Mtazamo wa uislamu juu ya Elimu, nini maana ya elimu na nani aliye elimika.
Ni nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika? Uislamu una mtazamo gani juu ya Elimu? Soma Zaidi...

image Kwa nini uislamu umeipa elimu nafasi ya kwanza
Elimu imepewa nafasi kubwa sana katika uislamu. Soma Zaidi...

image Ni nini maana ya Ilhamu katika uislamu?
Ilhamu ni moja katika njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu na kuwafundisha mambo mablimbali. Soma Zaidi...

image Kwa nini Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa
Kwa nini uislamu ndio dini pekee ya haki ambayo watu wanatakiwa waifuate. Soma Zaidi...

image Njia ambazo Allah hufundisha wanadamu elimu mbalimbali
Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu? Soma Zaidi...

image Mwanadamu hawezi kuishi bila dini kutokana na vipawa alivyooewa na Allah
Je ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya kuwa na dini?. Vipawa alivyopewa na Allahni jibu tosha juu ya swali jilo Soma Zaidi...

image Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.
Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini. Soma Zaidi...