picha

Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito

Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.

Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito



KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA UJAUZITO




Hili ni swali ambalo wengi ya wajawazito wanajiulizaga. Kwa ufupi hakuna shida yeyote kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito, bila kujali hatua ya ujauzito. Unaweza kuzungumza na daktari kuhusu swala hili, ila usiwe na shaka kabisa. Tafiti zinaonyesha kuwa endapo mwanamke akifika kileleni akiwa katika ujauzito ni jambo jema kwa afya yake na afya ya mtoto na afya ya ujauzito. Najuwa maneno haya machache hayawezi kumaliza kiu ya maswali yako. Sasa hebu tuone mabo kadhaa.



1.Kwa baadhi ya wanawake wanapata maumivu wanaposhiriki tendo hili wakiwa wajawazito. Yes hii huweza kutokea kwani kzunguruko wa damu umeongezeka maeneo ya chini na kufanya maeneo hayo yawe na hisia nyingi sana. Hii inaweza kuleta hali ya kuumia kwa mjamzito wakati wa kuingia kwa uume. Wajitahidi wakati wa tendo hili kutumia muda mwingi kujiandaa, pia spidi upungue, na tendo lisifanyike kwa nguvu kama siku za kawaida.



2.Kuna baadhi ya wanawake wanajikuta uke wao umepunguza hali ya kubana yaani wanahisi unabwebwea. Ukweli ni kuwa kutokana na ongezeko la majimaji mwanamke anaweza kuhisi kuwa ule mnato na msuguano aliouzoea haupo. Hali hii inaweza kuwapunguzia hamu ya tendo baadhi ya wanawake.



3.Kwa baadhi ya wanawake majimaji yanakuwa mengi kiasi cha kuhisi kumkosesha raha mwenziwake. Hii hutokea baada ya msisimko kuzidi ama kwa sababu kuna mabdiliko ya homoni. Kama hali ni hii hakuna budi kuvumiliana.



4.Mkao wowte unaweza kutumika maadamu hautakandamiza tumbo la mama. Hapa wawe makini sana hasa ujauzito ukiwa mkubwa wasijelibana tumbo. Mkao wa ubavu ubavu na inayofanana na namna hiyo inaweza kuwa ni mizuri. Zungumza na daktari atakupa maelekezo vyema



5.Je kushiriki tendo kunaweza kusababisha ujauzito kutoka? Hapana si kweli kabisa. Ujauzito hauwezi kutoka eti kwa kushiriki tendo la ndoa.



6.Baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa mjamzito anaweza kuona damu ama kutokwa na damu. Hii pia sio tatizo. Ila kama itakuwa inatoka kwa wingi vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.



7.Kwa baadhi ya wanwake inafikia wakati hahisi chochote anaposhiriki tendo na anakosa hamu kabisa ya kushiriki. Hili sio tatizo kubwa anaweza kumuona daktari kwa maelezo zaidi.



8.Kama atahisi dalili zifuatazo ni vyema kumuona daktari:
A.Maumivu makali zaidi yasiyovumilika
B.Damu nyingi
C.Kushindwa kupumuwa vyema



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 5374

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 web hosting    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 ai web app   

Post zinazofanana:

Dalili za upungufu wa homoni ya projestron

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.

Soma Zaidi...
Dalili za uchungu

Uchungu wa uzazi hutokana na kubana nakuachia kwa misuli hii husababishwa kufunhuka kwa mlango wa tumbo la uzazi pamoja na shingo ya kizazi na kumuongezea mama uchungu wakati wa kujifungua(during labour) Pia kubana na kuachia huanza polepole wakati wa

Soma Zaidi...
Siku za kupata ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata ujauzito

Soma Zaidi...
Mimi Nina tatizo kila nkishika mimba huwa zinatoka tu ni mara 5 Sasa nifanyaje?

Mimba inaweza kutoka kutokana na maradhi, majeraha ama misukosuko mimgine. Kutoka kwa mimva haimaanishi ndio mwisho wa kizazi.

Soma Zaidi...
NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME

Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.

Soma Zaidi...
Huduma kwa mama mwenye kifafa cha mimba.

Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wajawazito wanaweza kuzipata wakiwa na Dalli au tayari wana kifafa cha mimba.

Soma Zaidi...
Mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama ananyonyesha

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama anaenyonyesha

Soma Zaidi...
mim ninaujauzito wa mwezi mmoja lakini naona kama hali fulani ya damu inanitoka sehemu ya Siri inafanana na damu ya wakati wa period

Kutokuwa na damu wakati wa ujauzito ni hali uliyo ya kawida lakini inapaswa kujuwa sifa za damu hiyo nabje unatoka kwa namna gani. Kama unasumbuliwa na tatizo hili makala hii ni kwa ajili yako.

Soma Zaidi...
Kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.

Post hii inahusu zaidi kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii utokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kwa sababu maalum kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...