Utaratibu kwa wajawazito na wanaonyonshesha wakiwa na virusi vya ukimwi na ukimwi

Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha

Utaratibu kwa wajawazito na wanaonyonshesha wakiwa na virusi vya ukimwi na ukimwi



MWANAMKE MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI AKIWA MJAMZITO AMA ANAVYOVYESHA.




Watu wengi wamekuwa kijiuliza sana kuhusu hatma ya ujauzito kwa mwenye virusi vya ukimwi. Je ni kiasi gani mtoto aliye tumboni atakuwa salama?. ni tahadhari gani mjamzito mwenye virisi vya ukimwi achukuwe. Na atakapojifunguwa ni muda gani ataendelea kunyonyesha? Katika kipengele hiki tutaangalia kwa ufupi habari hii kama ifuatavyo:-



1.Je inawezekana kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kupata HIV/UKIMWI?
Yes inawezekana, na hili ni swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Itambulike kuwa kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika si lazima kuwa nawe utaathirika, ila kauli hii isieleweke vibaya. Kwani njia ambayo inaongoza leo katika kueneza maambukizi ya HIV ni kushiriki tendo la ndio. Mtu anaweza kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kuathirika endapo:-



A.Endapo hakutatokea michubuko wakati wa tendo
B.Endapo muathirika ametumia dawa za ART kwa muda mrefu kwa kufuata masharti hata viral load yake ikawa haionekani (undetected) na akadumu kwa hali hii walau miezi 6
C.Endapo walitumia kinga wakati wa kushiriki tendo.



2.Je HIV ma UKIMWI hupelekea mimba kutoka?
Inategemea, ila kwa ufupi HIV na UKIMWI huhatarisha ujauzito endapo muathirika hatakuwa mwangalifu ama hatafata maelekezo vyema. Wajawazito walioathirika inashauriwa wafike kituo cha afya mapema sananili kupatiwa maelekezo jinsi ya kulea mimba yake kwa usalama bila ya kuathiri afya ya ujauzito wake. Hata hivyo wanatakiwa wafuate maelekezo vyema.



3.Je maisha ya mtoto yapo hatarini endapo mama mjamzito ana HIV na UKIMWI?
Ni kweli kama mama mjamzito hatakuwa makini, anaweza kuweka maisha ya mtoto wake hatarini. Na si maisha ya mtoto tu bali hata maisha yake pia.



4.Je mtoto anapataje HIV na UKIMWI kutoka kwa mama?
A.Wakati wa kujifunguwa kama kuna kosa litafanyika.
B.Wakati wa kumnyonyosha kuanzia miezi sita toka kuzaliwa mtoto
C.Wakati wa kumlea kama mama hatakuwa makni



5.Kwa nyakati za sasa wajawazito wote wanatakiwa kuzalia kwenye kituo cha afya maalumu. Hii ni kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Hatahivyo wakunga wa jadi pia wamepatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya dharura. Ila inalazimika kwa mwenye HIV afanye juu chini azalie hospitali kwa usalama zaidi wa mtoto wake.



6.Je kunyonyesha mtoto kunawza kumuambukiza HIV?
Yes inawezekana, hata hivyo mama akiwa makini na maelezo aliyopewa, katu hatoweza kumuambukiza mwanaye. Inashauiwa mtoto kunyonya kwa muda wa miezi 6 tu ama chini ya hapo. Ni kuwa endapo mtoto atakuwa na michubukomdomoni ama tumboni.



7.Mama asimchanganyie mtoto ziwa lake, maziwa ya kopo na chakula. Kama ataamuwakumnyonyesha ndani iwe ni ndani ya miezi 6 tu na asimpe chakula chochote. Na kama ameamuwa kumpa chakula asimnyonyeshe tena. Na kama ameamuwa kumpa maziwa ya makopo ampe hayo tu na asimnyonyeshe. Anaweza kuchanganya chakula na maziwa ya kopo ama ya ng'ombe na si yake na kitu chingine chochote. Mama awe makini sana na jambo hili, asimchanganyie mtoto maziwa yeke na kitu kingine chochote. Hali hii inaweza kusababisha michubuko mdomoni ama tumboni na kusababisha kupata maambukizi.





Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 268


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-