Vyakula hivi hapasi kuvila mwanamke mwenye ujauzito kwa kiasi kikubwa, hasa yule mwenye mimba chaga

VYAKULA HATARI KWA MJAMZITO HASA KWA MIMBA CHANGA
1.Mayai mabichi: Mayai ni chakula kizuri kila mtu anatambuwa hili. Hata hivyo si jambo jema kula mayai mabichi. Hii inaweza kuwa hatari kwa ujauzito hasa kwa mwenye ujauzito mchanga. Hivyo epuka kula mayai mabichi ama yasiyowiva vyema.
2.Maini ya wanyama kwa wingi: Maini ni katika vyakula ambavyo vina virutubisho vingi sana. Kama ijulikanavyo ini lina kazi nyingi mojawapo ni kuondoa sumu mwilini. Hivyo unahitajika kutokula maini kwa mjamzito.
3.Shubiri: shubiri hufahamika kwa uchungu wake. kwa mwenye ujauzito hasa mimba changa shubiri sio salama. Shubirilinaweza kutoa ujauzito kama litatumika kwa kulinywa. Onyo hili linaandamana na miti mingine michungu.
4.Viazi mbatata vilivyoanza kuota: onyo hili ni kwa nafaka zote zinazoanza kuota sio nzuri kula. Hasa hasa viazi mbatata ambavyo vimeanza kutoa miche sio salama kwa mwanamke mjamzito kutuia kama chakula.
5.Mapapai hasahasa mapapai yasiyowiva: Matunda nimuhmu sana kwa mjamzito kwa afya yake na ya mtoto wake. Hata hivyo kuna matunda sio mazuri kuyala kwa wingi kwa mwenye mimba changa. Mapapai ni mojawapo, hasa papai ambalo halikuwiva, yaani lile la kijani lililokomaa.
6.Mananasi: nanasi ni kama papai, kama mjamzito atatumia kwa wingi, inaweza kuwa hatari kwa mimba iliyochanga.
7.Vyakula ambavyo havijawiva vyema hususani samaki na nyama: sio samaki tu na nyama, chakula chochote ambacho hakikuwiva vyema ni hatari sana kwa mwenye uauzito. Hii ni sawa na nyama ya kuku na vyakula vingine.
8.Kutumia majani ya chai yenye caffein kwa wingi. Mjamzito hakatazwi kunywa chai ya majani ya chai. Kilichokibaya ni kuzidisha unywaji wa chai yenye majani ya chai kupitiliza. Majani ya chai yana kemikali inayoitwa caffein, hii ikiwa nyingi inakuwa hatari kwa ujauzito.
9.Chumvi kwa wingi
10.Energy drink
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Post hii inahusu zaidi madhara ya kutoka kwa mimba, kwa kawaida tunafahamu kwamba mimba ikitungwa na mwili mzima huwa na wajibu wa kutunza kilichotungwa kwa hiyo ikitokea mimba ikatoka usababisha madhara yafuatayo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mda ambao mama anapaswa kukaa bila kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa Mama mjamzito, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama mjamzito, hizi Dalili zisipofanyiwa kazi mapema zinaweza kuleta shida kwa Mama kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua Dalili hizi na kuchukua hatua endapo zitajio
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa jamii, tunapaswa kujua kuwa uzazi wa mpango ukitumiwa vizuri na jamii nayo inapata faida kwa hiyo zifuatazo ni faida za uzazi wa mpango kwa jamii.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama, zoezi hili ufanyika kila mwezi pale mama anapokuja kwenye mahudhurio kwa kufanya hivyo tunaweza kuja maendeleo ya mtoto kwa kila mwezi.
Soma Zaidi...