picha

Mimba iliyotungia nje, sababu zake na dalili zake. Nini kifanyike kuizuia?

Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?

Mimba iliyotungia nje, sababu zake na dalili zake. Nini kifanyike kuizuia?



MIMBA ILIYOTUNGIA NJE:




Mimba ya namna hii kitaalamu hufahamika kama ectopic pregnancy. Je hii ni mimba gani? Hii ni mimba ambayo yai lililorutubishwa linaendelea kukuwa nje ya mji wa mimba (uterus). mimba inaweza kukuwa sehemu yeyote kwenye tumbo ila nje ya mji wa mimba. Kwa asilimia kama 90% mimba hukuwa kwenye mirija ya falopia. Hii ni mimba hatari sana na inahitaji uangalizi wa haraka sana, kwani inaweza kuhatarisha maisha ya mama. Inakadiriwa kuwa mimba za namna hii huchukuwa kati ya asilimia 1 mpaka 2 ya miba zote.



Kwa nini mimba hii ni hatari?
1.Mimba inatkuwa nje ya mji wa mimba hivyo haiwezekani mtoto kupona
2.Inaweza kusababisha kupasuka kwa mirija ama sehemu ilipokuwa.
3.Inaweza kusababisha ulemavu kwa mama endapo itachelewa kuonekana
4.Kwa asilimia 30 mimba hii haina dalili hii ni hatari zaidi.
5.Inaweza kusababisha uvujaji wa damu kwa kiasi ikubwa
6.Inaweza kusababisha mwanamke kuhitajiwa kufanyiwa upasuaji kamma tiba.



Sababu za kutokea mimba hii
Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa asilimia 30 ya mimba hizi hazina dalili. Lakini kwa kiasi kikubwa mimba hizi huwa na dalili. Tafiti zinaonyesha kuwa dalili zake hutokea kabla ya wiki ya 10. Sasa hapa nitakutajia baadhi tu ya dalili za mimba hii:-
1.Maumivu ya tumbo upande mmoja wa nyonga.
2.Maumivu ya mabega
3.Kutokwa na damu kwenye uke.
4.Maumivu ya nyonga.
5.Mvurugiko wa tumbo na kutapika
6.Maumivu ya upande mmoja wa mwili.
7.Kizunguzungu na uchovu
8.Maumivu ya mabega, shingo na mkundu.



Sababu za kutokea kwa mimba hii.
1.Kuwa na maambukizi kwenye via vya uzazi yaani PID
2.Uvutaji wa sigara
3.Kama una umri wa miaka 35 na kuendelea
4.Kama unatumia madawa ya kuivisha mayai
5.Kama ulishapata ujauzito huu hapo mwanzo upo uwezekano kuja kupata tena
6.Kama ulifanyiwa upasuaji kwenye mirija ya falopia
7.Kama una tatizo la endometriosis
8.Baadhi ya njia za kuthibiti uzazi mfano, IUD



Nini tena yapasa kujuwa?
1.Ujauzito uliotungia njea haurithiwi yaani kama mama aliwahikupata ujauzito huu hali hii hairithiwi.
2.Kutoka kwa ujauzito sio sababu ya kupata mimba hii
3.Kutoa ujauzito pia hakuna mahusianao na ujauzito huu
4.Mazoezi na michezo pia hihusiani na kutokea kwa ujauzito huu.



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 2963

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉3 ai web app    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Ongezeko la homoni ya estrogen

Posti hii inahusu zaidi ongezeko la homoni ya estrogen, kwa kawaida homoni hii ya estrogen inapaswa kulingana ikitokea ikaongezeka uleta madhara mbalimbali kwenye mwili na Kuna dalili ambazo zzz inaweza kujionesha wazi mpaka tukafahamu kuwa ni tatizo la o

Soma Zaidi...
utaratibu wa lishe kwa Mjamzito, Vyakula anavyopasa kula mjamzito

Ni vyakula gani anapasa kula mjamzito, na utaratibu mzima wa lishe kwa wajawazito

Soma Zaidi...
Vyakula vinavyosaidia katika uzalishaji wa homoni ya testosterone

Posti hii inahusu zaidi vyakula ambavyo usaidia katika uzalishaji wa homoni ya testosterone.

Soma Zaidi...
Sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake

Soma Zaidi...
Utaratibu kwa wajawazito na wanaonyonshesha wakiwa na virusi vya ukimwi na ukimwi

Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha

Soma Zaidi...
Je mwanamke anaweza pata mimba ikiwa wakati watendo la ndoa hakukojoa Wala kusikia raha yoyote ya sex wakati watendo landoa

Je wewe ni mwanmake unayepata shida kufika kileleni? (Kukojoa wakati wa tendo lwa ndoa). Post hii itakujibu baadhi ya maswali yako.

Soma Zaidi...
Dalili za mimba inayotishi kutoka

Posti hii inahusu zaidi dalili za mimba inayotaka kutoka yenyewe, Kuna wakati mwingine mama anabeba mimba na mimba hiyo I atishia kutoka na huwa inaonyesha dalili mbalimbali kwa hiyo zifuatazo ni dalili za mimba kutaka kutoka yenyewe.

Soma Zaidi...
Namna za kujilinda na fangasi ukeni

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuepuka fangasi za ukeni, ni njia ambazo usaidia kuepuka madhara ya fangasi za ukeni.

Soma Zaidi...
Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito

Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.

Soma Zaidi...
Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza

Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili.

Soma Zaidi...