
Ujauzito umegawanyika katika hatua kuu tatu, au vipindi vikuu vitatu ambavyoni:-
1.trimester ya kwanza (first trimester)
Hiki ni kipindi katia ya wiki 1 mpaka 12 yaani ndani ya miezi mitatu ya kwanza. Kipindi hiki mjamzito awe makini sana kwani ni kipindi ambacho kutoka kwa ujauzito ni rahisi sana. Kipindi hiki ndicho ambacho mtoto anaanza kukuwa ubongo, uti wa mgongo na viungo vingine ama moyo na masikio. Tafiti zinaonyesha kuwa takribani asilimia 85 ya mimba zinazotoka huwa zinatoka katika kipindi hiki. Hata hivyo wanaotowa mimba pia hutoa katika kipindi hiki.
Mabadiliko ya mwili katika kipindi hiki
A.Uchovu
B.Kukosa haja kubwa
C.Kichefuchefu
D.Maumivu ya kichwa
Nini hakitakiwi kufanyika katika kipindi hiki?
A.Wacha kuvuta sigara
B.Wacha kunywa pombe
C.Wacha kutumia dawa kiholela bila ya ushauri wa daktari
D.Kuwa makini sana kwani kosaadogo ujauzito upo hatarini
E.Punguza kuchwa chai kupitiliza
F.Punguza kula samaki kwenye magobeta jaamii ya tondo
2.Trimester ya pili (second trimester)
Kipindi hiki ni kati ya wiki 13 mpaka 27 yaani kuanzia mwezi wa 3 mpaka wa 6 kwenda wa saba. Katika kipindi hiki mwanamke atafanyiwa vipimo vya utrasound kuangalia mkao wa mtoto na kama yupo katika afya njema. Katika kipindi hiki hata jinsia ya mtoto itaweza uonekana kwa ambaye anataka kuiona kwenye kipimo cha utrasound. Hapa mtoto anaweza kuishi nje ya mwili wa mama yake kuanzia wiki ya 23. na endapo mtoto atazaliwa hapa atakuwa njiti hivyo vifaa maalumu vitahitajika kumlea kabla ya kuanza kuishi huru. Katika kipindi hiki mama mjamzito atasikia vurugu za mtoto tumboni, kupiga mateke, kugeuka na nyinginezo.
Katika kipindi hiki karibia dalili zote za ujauzito za mwanzo hupotea. Nguvu itarudi vyema na utawza kulala usingizi mnono usiku. Katika kipindi hki tumbo litaanza kuonekana kukuwa. Katika kipindi hiki jiepushe sana yafuatayo:-
A.Kuvaa nguo za kubana
B.Kuwa na hasira mara kwamara. Yaani jitahidi kkutafuta furaha, kaa na maafiki cheka na furahia.
C.Usikibane tumbo hata likiwa kubwa vipi.
Katika kipindi hiki unawezakuhisi kuingulia mra kwa mara, na maumivu ya miguu. Hamu ya kula inawea kuongezeka, na uzito pia kuongezeka katika kipindi hiki. Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya mgongo. Hata hivyo anaweza kujihisi kama ana mafua ama pua zimeziba ila akifina hakuna kitu. Pia anaweza kuiona mishipa inatokeza kwa nje hasa kwenye miguu.
Katika kipindi hiki mama mjamzito ataanza kusikia mijongeo ya mtoto. Hata hivyo mtoto ataweza kuitambuwa sauti ya mama yake na watu wa karibu sana na mama yake. Baadhi ya viungo vinavyoweza kuonekana kwenye utrasound katika kipindi hiki ni kama figo, mapafu, moyo na ubongo na jinsia. Katika kipindi hiki mama mjamzito anaweza kupimwa kisukari cha mimba kuanzia wiki ya 26 mpaka 28.
3.Trimester ya tatu (third trimester)
Kipindi hiki huanzia wiki ya 28 mpaka 40, yaani kuanzia miezi 7 kwa makadirio. Katika kipindi hiki mara kwa mara utahitajika kumuona daktari kwa vipimo zaidi. Daktari atakuwa anakuangalia maendeleo yako kwa jumla na afya ya ujauzito wako. Atakuwa anakucheki:-
A.Anapima mkojo kuangalia protini
B.Atakuwa analkuangalia shinikizo la damu (presha)
C.Atasikiliza mapigo ya moyo wa mtoto
D.Atakuwa akipima njia ya uzaziatakuwa acheki miguu na mikono kama itakuwa inavimba.
Pia daktari anaweza kukupima uwepo wa bakteria wanaoitwa Group B streptococcus (GBS) kwenye uke. Uwepo wa bakteria hawa unaweza kuhatarisha afya ya mtoto anayezaliwa. Katika kipindi hiki ni vyema kuanza kufuatilia habari za kujifungua, mazoezi ya kujifungua na namna ya kujiandaa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye Matiti kwa Mama mjamzito, hali hii utokea pale ambapo mama akibeba mimba Kuna mabadiliko kwenye Matiti kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Uchungu wa uzazi hutokana na kubana nakuachia kwa misuli hii husababishwa kufunhuka kwa mlango wa tumbo la uzazi pamoja na shingo ya kizazi na kumuongezea mama uchungu wakati wa kujifungua(during labour) Pia kubana na kuachia huanza polepole wakati wa
Soma Zaidi...Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.
Soma Zaidi...Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha
Soma Zaidi...Idadi ya siku hatari za kupata mimba hutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja namwinhine. Kinda ambao idadivyavsikuvzao za hatari ni nyingi kuliko wengine.
Soma Zaidi...Posti hii hasa inahusu kasoro ,utatuzi,na jinsi ya kutunga mimba kwa upande wa mwanamke na mwanaumeย .itatupelekea jinsi ya kuangalia kasoro na jinsi ya kutatua hizo kasoro katika jamii zetu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia au namna ya kufunga kitovu cha mtoto mara tu anapozaliwa, kwa kawaida tunafahamu kwamba ili mtoto aweze kuishi akiwa tumboni anategemea sana kula na kufanya shughuli zake kwa kupitia kwenye plasenta kwa hiyo mtoto akizaliwa tu
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kupasuka kwa kondo la nyuma (plasenta) (abruptio placentae) ni tatizo lisilo la kawaida lakini kubwa la ujauzito.Kondo la nyuma (Placenta) ni muundo ambao hukua ndani ya uterasi wakati wa ujauzito ili kumlisha mtoto ana
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za mimba kutoka, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mimba zote ambazo utaka kutoka kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Je anapatwa maumivu รฐลธหยญ makali wakati wa tendo la ndoa ama ukiwa katika hedhi? Soma makala hii hadi mwisho
Soma Zaidi...