Mimba inapotoka ina dalili, na zipo sababu kadhaa za kutoka kwa mimba. Je utazuiaje mimba kutoka. Soma makala hii

Kutoka kwa ujauzito mara nyimgi hutokea katika hiki kipindi cha kwanza yaani ndani ya wiki 12 za mwanzo. Inakadiriwa kuwa robo ya mimba hutoka. Mwanamke anaweza akatokwa na mimba kwa kujuwa ana bila ya kujuwa. Inaweza kutokea pia mwanamke akabeba ujauzito na ukatoka bila kuwa na habari yeyote kama alikuwa na miba na imetoka. Ni kuwa mimba inaweza kutoka bila ya kuwa na dalili za wazi kama kutoka na damu.
Dalili za kutoka kwa mimba:
A.Maumivu ya mgongo
B.Kuharisha
C.Kichefuchefu
D.Maumivu ya maeneo ya nyonga na kiuno kama unahisi unataka kuingia kwenye siku zako
E.Maumivu makali ya tumbo
F.Kutokwa na majimaji kwenye uke.
G.Kutokwa na vitu kama vijioande vya nyama vijidogo kwenye uke
H.Uchovu mkali sana usio na sababu
I.Kupotea kwa dalili nyingine za ujauzito
J.Kutokwa na damu mabonge manonge ama damu nyingi
Kumbuka hizi ni dalili tu, unaweza kuwa nazo na ujauzito ukawa salama kabisa. Ukiona unahisi dalili hizo muone daktari atathibitisha vyema kwa vipimo ikiwemo utrasound ama kuangalia kiwango cha homoni ya ujjauzito kwneye damu yako.
Ni zipi sababu za kutoka kwa mimba?
Mara nyingi kutoka kwa ujauzito kunaweza kusababishwa na chromosomal abnormalities. Hili ni tatizo la kigenetics. Hapa seli za mtoto zinashindwa kugawanyika vyema na kukuza mtoto. Sababu nyingine za kutoka ujauzito ni:-
A.Matatizo katika homoni kuwa nyingi sana ama kidogo sana
B.Kama mama mjamzito ana kisukari na hafuati masharti vyema
C.Mazingira yanaweza kuchangia kama kuna mionzi hatari kama ya madini ya uranium
D.Maambukizi na mashambulizi ya vijidudu kama bakteria kwenye via vya uzazi.
E.Shida katika mlango wa uzazi (cevix)
F.Kutumia madawa kiholela ama kutumia madawa kusudi kwa lengo la kutoa ujauzito
G.Ugonjwa wa endometriosis (kuvimba kwa kuta za mji wa mimba βuterusβ)
H.Magonjwa ya ngono kama gonoria
Sababu nyingine za kutoka kwa mimba
A.Utapia mlo
B.Kuwa na kitambi
C.Matumizi ya vilevi na sigara
D.Maradhi ya tezi ya thyroid
E.Shinikizo la damu la juu sana
NITAZUIAJE MIMBA KUTOKA?
Mimba nyingi zinazotoka husababishwa na genetics ama mambo ya kiafya ambayo si rahisi kuzuilika. Hivyo kwa mimba hizi ni ngumu sana kuzuia kutoka kwake. Hata hivypo kitu ambacho unaweza kukifanya ni kuhakikisha kuwa unabakia katika afya salama kabla na baada ya kubeba ujauzito. Fafya mabo yafuatayo yatasaidia katika kuboresha afya yako na kuzuia kiutoka kwa ujauzito:-
A.Kula mlo kamili wenye virutubisho (balanced diet)
B.Fanya mazoezi mara kwa mara. Si lazima eti mazoezi ya kukutoa mijasho, unaweza kufanya mazoezi ya viungo pia hata ukiwa kitandani.
C.Wacha ama punguza kutumia pombe, sigara ama dawa za kulevya.
D.Punguza unywaji wa chai kama unakunywa kwa wingi kupitiliza. Hapa ninazungumzia chai ya majani ya chai ambayo ina caffein.
E.Fanya uchunguzi wa afya yako mara kwa mara.
F.Wacha kutumia dawa kiholela
G.Jiepushe na mambo ambayo yataweza kuwa ni hatari kwa ujauzito kama kupigana ama miereka.
H.Fuata maelekezo vyema kutoka kwa wahudumu wa afya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito, ni chakula anachopaswa kutumia na ambavyo hapaswi kutumia kwa Mama mjamzito mzito, kwa sababu Mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika matumizi ya chakula ili kuweza kuongeza vitu muhimu mwil
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni ya estrogen na dalili zake, aina hii ya homoni ikipungua mwilini uleta madhara na matatizo mbalimbali kwenye mwili.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa Mwanaume, ni sababu ambazo umfanye mwanaume ashindwe kumpatia mwanamke mimba.
Soma Zaidi...Dalili za mimba pekee haziwezi kuthibitisha uwepo wa mimba. Bila vipimo kwa. Muda sahihi huwezi kuwa. Na uhakika. Je na wewe unasumbuliwa na dalili za mimba na ukapona hakuna mimba? Makala hii ni kwa ajili yako. Swali
Soma Zaidi...Makala hii itakujuza baadhi ya njia utakaoweza kuzifuata ili kukabiliana na fangasi sehemu za siri kwa wanaume
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo ni moja katika dalili za ujauzito. Maumivu wanawake wengi hushindwa kujuwa kuwa ni ujauzito ama laa. Na hii ni kwa sababu kwa wanawake wengi maumivu ya tumbo ama changu ni jalivya kawaida kwao.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wanaotoa hedhi yenye mabonge, ni tatizo ambalo uwakumba wasichana hata wanawake wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango, Ni watu ambao Wana matatizo mbalimbali endapo wakitumia wanaoweza kuleta madhara mbalimbali.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, ni malengo ambayo yametolewa ili kuweza kusaidia mtoto azaliwe vizuri na mambo mengine kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...