picha

Damu, majimaji na uteute unaotoka kwenye uke wa Mjamzito, sababu zake na dalili zake

Unataka kujuwa sababu za mjamzito kutokwa na damu, utelezi ama majimaji kwenye uke wake. Na dalili gani zinaashiriwa na majimaji haya

Damu, majimaji na uteute unaotoka kwenye uke wa Mjamzito, sababu zake na dalili zake



DAMU NA UTEUTE NA MAJIMAJI YANAYOTOKA UKENI WAKATI WA UJAUZITO:




Majimaji yanayotoka ukeni wakati wa ujauzito (Damu na uteute)
Ni kawaida kwa mjamzito kushuhudia kwenye uke wake kutokwa na kama uteute na huongezeka kila mimba inapoendelea kukomaa. Wakatiflani anaweza kuona nguo zake zina madoa ya damu, ama akashuhudia matone kadhaa ya damu. Wapo pia wanaingia hedhi kwa damu chache. Sasa hebu tuangalie kwa ufupi hali hizi:-



1.Baada ya kutoka hedhi uke wa mwanamke unakuwa mkavu bila ya kuwa na utelezi telezi. Hiki ni kipindi ambacho mwanamke hawezi kubeba ujauzito. Katika kipindi hiki hata akitia kidole hakitoki na utelezitelezi. Kipindi hiki kinaweza kuchukuwa takribani siki tano hadi 10 inategemea na mzunguruko wa mwanamke. Huu ni kuda mzuri wa kushiriki tendo kwa wale ambao hawahitaji kulea ujauzito.



2.Zitakapoanza kuingia siku hatari mwanamke ataanza kuhisi uwepo wa uteute kwenye uke wake anapotia kidole kwa ndani. Siku hizi pia zinatofautiana kulingana na idadi ya mzunguruko. Ila zinaweza kuazia siku ya 11 hadi 14 inaweza pia kuwa chini ya papo lwa baadhi ya wanawake ama juu ya hapo.



3.Siku moja kabla ya kukomaa kwa yai na kuwa tayari kwenye mirija ya falopian tayari kutungisha mimba, uteute huu huongezeka zaidi. Sifa za uteute huu ni kuwa ni wenye kuteleza sana ila sio mzito na wenye kunatanata ama kuvutikana. Kwa wanaotumia njia za uzazi wa mpango hasa zile za homoni uteute wao upo muda wowote kwa hiyo ni ngumu sana kwao kuiona hali hii.



4.Siku ya hatario zaidi mwanamke atapata mabadiliko ya hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa. Yaani hamu itaongezeka zaidi siku hii kuliko siku iliyotangulia. Hapa kwa wale ambao hawataki ujauzito sio siku salama kwao kushiriki tendo landoa.



5.Uteute huu katika siku hizi kuandaliwa kwa ajili ya kusaidia mbegu za kiume ziweze kusafiri vyema, kuogelea vyema na kulifikia yai. Pia kuhakikisha kuwa mbegu za kiume haziathiriwi na asidi ya tumboni kwa mama kwa kiasi kikubwa. Hivyo uteute huu katika kipindi hiki ni muhimu sana.



6.Kali hii inaweza kudumu kwa masiku kadhaa toka 14 hadi 17 kwa makadirio inaweza kupungua ama kuongezeka kulingana na mzunguruko wa mwanamke. Baada ya hapo kama mwanamke alibeba ujauzito majimaji haya yanaongezeka uzito saa na kuwa yenye kunata na kufanana na utelezi wa yai pindi unapolibanja. Baada ya mimba majimaji haya yataendelea kutoka na kuongezeka na kuwa mazito zaidi hadi atakapojifungua.



Katika ujauzito majimaji haya yanakazi ya kulinda njia ya kuingilia kwenye mji wa mimba dhidi ya mashambulizi na aambukizi ya bakteria. Yaani kuhakikisha kuwa hakuba bakteria ama fangasi atakayeweza kuingia na kumzuru mtoto tumboni.



7.Kama hakuna ujauzito uliobebwa majimaji yataanza kurudi kutoka hali yake ya kawaida na kuwa safi, yenye harufu kwa mbali ila si harufu ya kukera, pia yanaweza kuwa na rangi ya maziwa hivi.



Majimaji haya pia nayaweza kuashiria shida kwenye afya endapo yatakuwa na sifa hizi:-
A.Yana rangi ya njao, kijani ama buluu
B.Yana harufu kali mbaya
C.Yanakusababishia muwasho kwenye uke na mashavu ya uke
D.Yanakusababishia kuvimba kwa uke na mashavu ya uke



8.Ama kuhusu kutokwa na damu, ikiwa chache ni kawaida. Ikiwa unaambatana na maumivu makali ya tumbo, ama maumivi makali ya kichwa na homa, basi vyema kumuona daktari kwa ushauri zaidi. Kama nilivtotangulia kusema kuna wanawake wanapata hedhi wakiwa wajawazito. Wenyewe wanaita kupunguzia, kwa ufupi hii si hedhi na pia haiashirii kama kuna tatizo. Ila kama inatoka nyingi na kuambatana na maumivu yasiyo ya kawaida ni vyema kumuona daktari.



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 16837

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 web hosting    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

mpenzi wangu nimeshiriki nae tendo la ndoa akiwa siku zake za hatar kwa siku 3 lakin hajashika mimba tatizo linaweza kuwa ni nini?

Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.

Soma Zaidi...
Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa

Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoabkunaweza kuashiria kuwa kuna majeraha yametokea huwenda ni michubuko ilitokea ndio ikavujisha damu. Lakini kwa nini hali kama hii itokee. Posti hii itakwwnda mujibu swali hili.

Soma Zaidi...
Mabadiliko ya via vya uzazi kwa Mama mjamzito.

Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye via vya uzazi kwa wajawazito, tunajua kuwa Mama akibeba mimba tu kuna mabadiliko utokea katika sehemu mbalimbali za mwili.

Soma Zaidi...
Dalili za kujifungua hatua kwa hatua

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kujifungua hatua kwa hatua

Soma Zaidi...
Njia za kiasili zilizotumika zamani kqtika kupima ujauzito

Somo hili linakwenda kukuletea njia za asili walizotumia zamani katika kupima ujauzito

Soma Zaidi...
SIKU HATARI ZA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE MZUNGURUKO WA SIKU KIDONGO AU NYUNGI

SIKU YA KUPATA UJAUZITO Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo.

Soma Zaidi...
Ni vipi nitagundua kuwa nina ujauzito?

Hali ya ujauzito huanza kutabirika Mara tu ya kujamiana, pia chemikali (hormon) za mwili huanza mchakato wa kuongeza na kupunguza utendaji kazi wa kemikali hizo mfano.follical stimulating hormon (FSH) na lutenazing hormon kuivisha yai tayari kwa kutengen

Soma Zaidi...
Kondomu za kike

Posti hii inaonyesha Faida na hasara za Kondomu za kike

Soma Zaidi...