AINA ZA MINYOO: tapeworm, livefluke, roundworm, hookworm, flatworm
AINA ZA MINYOO Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa.
AINA ZA MINYOO
AINA ZA MINYOO
Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa. Aina hizi ni Minyoo wanaotambulika kama flatworm, roundworm na thory-headed worm. Majina ya minyoo hawa yanafanana na maumbile yako kama tutakavyoona hapo chini. Wengi katika hawa minyoo wanaweza kuonekana kwa macho
1.Minyoo inayotambulika kama Tapeworm
Hawa ni katika aina za flatworm, minyoo hawa wanaumbo lililo bataa yaani flati. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kunywa maji ambayo yana mayai ya minyoo hawa au lava. Pia unaweza kuwapata. Minyoo hawa kwenye chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuiva vizuri.kama nyama hasa ya ngurue. Karibia nyama za wanyama wote zina wadudu hawa.
Minyoo hawa wanaonekana kama pingili zilizoungana na kutengeneza cheni ndefu. Minyoo hawa wanaweza kuwa warefu mpaka kufikia futi 80 na wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu mpaka miaka 30.
2.minyoo inayotambulika kama flukes
Hawa pia ni katika aina za minyoo waitwao flatworm. Mwanadamu anaweza kuwapata minyoo hawa kupitia maji yasiyo salama,kupitia mboga ambazo hukuwa ndani ya maji.pia kwa kula samaki ambaye ana minyoo hawa. Pia inatokea ukaosha mboga, tunda kwa kutumia maji ambayo yana minyoo hawa.
Minyoo hawa wanapoingia mwilini wanaelekea kwanye utumbo mdogo na huko ndipo huishi, pia maeneo mengine wanapoishi ni kwenye damu, na tishu za mwili kama ini. Kuna aina nyingi za aina hii ya minyoo, lakini ukubwa wao hawazidi nchi kadhaa.
3.minyoo wanaotambulika kama Hookworm
Hawa ni minyoo aina ya roundworm. Minyoo hawa wanaweza kusambazwa kwa kupitia kinyesina udongo. Hasa kwa wale wanaokula udongo ni rahisi sana kupata aina hii ya minyoo. Njia nyingine nyepesi kwa kupata minyoo hawa ni kwa kutembea miguu peku kwenye udongo ambao una mayai au lava wa aina hii ya minyoo. Malava haya yanaweza kuingia kwenye ngozi yako.
Minyoo hawa wanaishi kwenye utumbo mwembamba, na kwa kuwa kichwani kwao kuna kama miimba ilofanana na ndiwano, wanaitumia kujitundika kwenye utumbo mdogo. Ukubwa wao hauzidi nusu nchi.
4.minyoo wanaotambulika kama pinworms (threadworms)
Hawa ni katika minyoo wadogo sana na maranyingi hawana madhara. Minyoo hawa ni maarufu sana kwa watoto, walezi wa watoto wadogo na maeneo yeye watoto wadogo wengi unweza kuwapata sana hawa. Wana rangi nyeupe na ukubwa wao hauzindi nusu nchi.
Minyoo hawa unawapata kwa kuyala mayai yao kutoka kwa mtu mwenye minyoo hii. Mayai ya minyoo hawa hayawezi kuonekana kwa macho. Pindi unapokula mayai haya yanakwenda kukaa kwenye utumbo mdogo mpaka kutotolewa. Wakati wa usiku minyoo wanawake wanakwenye chini kwenye puru na kutaga mayai kwenye mikunjo ya puru. Kama mtu atajikuna sehemu ya puru mayai yale yanabakia mkononi zaidi ya masaa kadhaa.
Ikitokea mtu huyu ameshika kitu bila ya kunawa mayai yele yanabaki pale. Kama mtu mwingine akapashika pale na akala kitu bila ya kunawa anaweza akayala mayai yale na kupata minyoo. Pia minyoo hii unaweza kuipata kwa kuvuta hewa yenye mayai ya minyoo hii.
Minyoo hii haina athari zaidi kwa afya lakini mwenye minyoo hii atahisi kuwashwa kwenye puru, ama kuzungukia sehemu ya haja kuwa, wakati mwingine maumivu yatumbo. Wakati mwingine ngozi inawasha sana. Minyoo hawa pia kwa wanawake wanaweza kuhama kutoka kwenye puru na kuelekea kwenye uke wa mwanamke na kuingia ndani. Huenda hali hii ikapelekea kupata UTI na matatizo mengine ya kiaya.
Kupambana na minyoo hawa hakikisha unaosha mikono unapoamka, unapotaka kula chochote, kuingia kwenye choo safi na usipende kushikshika vitu hasa maeneo ya vyoo vya watu wengi. Minyoo hawa ni rahisi kutibika tofauti na minyoo wengine.
5.minyoo wanaotambulika kama trichinosis worm
Minyoo hawa ni katika minyoo ambao wanapatikana kutoka kwa wanyama. Mtu anaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula nyama ambayo haukuiva vyema, ama kwa kula nyama mbichi. Malava ya minyoo hawa yanakwenda kwenye utumbo mdogo, na huko huweza kuingia kwenye mirija ya damu na kuenda maeneo mengine ya mwili, kwenye misuli na tishu za mwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 Simulizi za Hadithi Audio π3 ai web app π4 kitabu cha Simulizi π5 Bongolite - Game zone - Play free game π6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Dalili za ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster. Kwa hiyo ili kugundua kubwa mtu ana Ugonjwa huu Dalili kama hizi zifuatazo zinaweza kutokea kwa mgonjwa.
Soma Zaidi...Dalili za Mimba Kabla ya Kipimo:
βKipindi cha kusubiri ili kufanya kipimo cha mimba kinaweza kuwa na msisimko na wakati mwingine wasiwasi. Makala hii inakupatia mwongozo wa ishara za awali ambazo mwili wako unaweza kuzionyesha kabla hata ya kupata majibu ya vipimo vya maabara au vya nyumbani.
Soma Zaidi...Dalili za maambukizi kwenye ovari
Posti hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye ovari, ni maambukizi ambayo hutokea kwenye ovari na kusababisha matatizo makubwa kama mgonjwa haujatibiwa mapema.
Soma Zaidi...Bipolar disorders
Bipolar disorder ni hali ya afya ya akili inayohusisha mabadiliko makubwa katika hisia, nishati, na shughuli za kila siku za mtu. Dalili za bipolar disorder zinaweza kuwa kwenye kipindi cha mania na kipindi cha unyogovu, zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa bipolar.
Soma Zaidi...Samaani nilikuwa nauriza ninasumburiwa na fanga ya mdomoni naomba ushauri
Fangasi mdomoni wanaweza kuwa tatizo endapo hawatatibiwa mapema. Wanaweza kuongeza majeraha kwenye kinywa.
Soma Zaidi...Aina ya Magonjwa ya akili
Unyogovu (Depression ) ni mojawapo ya ugonjwa wa akili ambao unahusishwa na hisia za huzuni, kukosa matumaini, na kupoteza furaha au shauku katika shughuli za kila siku. Huu si tu hisia ya huzuni iliyokatisha tamaa, bali ni hali sugu inayoweza kuathiri mabadiliko ya mwili, mawazo, na tabia ya mtu. Unyogovu unaweza kutokea kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kemikali katika ubongo, maumbile, mazingira, na matukio mbali mbali katika maisha ambayo kupelekea mgonjwa kuwa hivyo.
Soma Zaidi...