image

Namna ambavyo mwili unapambana na maradhi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi

NAMNA AMBAVYO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI

Tumeona huko juu kuhusu visababishi vya maradhi na namna ambavyo maradhi yanaweza kusambaa, sasa hapa tutaona namna ambavyo miili yetu unapambana na maradhi haya kwa ajili yetu. Mwili una njia nyingi tuu na namna ya kupambana na maradhi kama utakavyoona hapo chini

 

1.KA KUTUMIA KUTA ZUIZI (PHYSICAL BARRIERS

Itambulike kuwa ili mtu aumwe ni kwamba wadudu wa maradhi wanatakiwa waingie mwilini. Sasa mwili una vizuizi yaani kuna ukuta maalum ambao unakazi ya kuzuoa wadudu hawa wasipate njia ya kuingia ndani. Vizuizi hivyo ni;-

 

A).Ngozi:ngozi yenyewe ni ukuta wa kuzuia vijidudu hivi. Ngozi hutumia chemikali kama jasho na mafuta ili kuuwa vijidudu hivi.ngozi inatabia ya kujitibu kwa haraka zaidi kama itapata jeraha ili kuzuia wadudu wasiingie.

 

B).Utando wa utelezi: huu ni utando maalumu ambao unateleza na kunata. Utando huu unapatika na sehemu nyingi za mwili kama puani kwa ajili ya kunasa mavumbi na vijidudu hawa. Utando huu pia upo machoni kwa ajili ya kunasa vijidudu hivi na kuvitoa nje.

 

C)Vinyweleo: hivi ni njia nyingine ya kunasa wadudu wowote wanaoraka kuingia ndani. Kwa mfano ndani ya pua kuwa vinyweleo hivi kwa ajili ya kunasa wadudu na mavumbi kuingia ndani.

 

D)Kemikali: kwa mfano mwili huzalisha asidi ya hydrocloric ambayo husaidia kuuwa bakteria waliopo kwenye vyakula.

 

2.INFLAMATORY RESPONSE (YAANI KUVIMBA)

Inatokea wadudu hawa wanaingia mwilini kwa mfano mtu anpojikata. Hivyo inflammatory response hali ya mwili kupambana na ma majeraha ambapo sehemu husika huvimba, huwa njeundu na kuwa na maumivu. Kitendo hiki hufanya eneo hili liwe limoto na kusababisha vimishipa vidogo vinavyoleta damu vilete damu kwa wingi na hatimaye seli kutoka kwenye damu hupambana na wadudu walofanikiwa kuingia kwenye eneo lile.

 

3.IMMUNE SYATEM (MFUMO WA KINGA)

Njia zilizotajwa hapo juu pekee haziwezi kupambana na wadudu hawa. Hivyo kuna mfumo maalumu wa kuukinga mwili dhidi ya majambazi hawa (pathojens) mfumo huu huitwa immune system ambao unatengenezwa na seli hai nyeupe za damu na aina flani ya protin ambayo kitaalamu huitwa antibodies ambazo zipo kwenye mfumo wa lymph (lymphatic system).

 

Mfumo wa lymph huu umezunguka mwili mzima na unahusika katika kubeba majimaji mwilini. Katika kufanya hivi unafanya kazi ya kuwatowa bakteria na pathogen wengine nje ya mwili. Mfumo huu una seli hai nyeupe nyingi nna hizi ndizo ambazo zinapambana na pathogen na kuwauwa.

 

Seli nyeupe za damu, kazi yao kuu seli hizi ni kuulinda mwili dhidi ya wavamizi. Kuna aina fani ya seli hizi hutowa kemikali ziitwazo antibodies ambazo huwakamata pathogens na pitowa tahadhari kwa seli nyingine ili wawaue hawa pathogens. Pindi unapoumwa hutokea tezi za lymph zinauma kama mtoki ni kwa sababu seli hizi nyeupe zipo kwa wingi eneo lile kupambana na wadudu hawa.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 689


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Aliyepaliwa na maji huduma ya kwanza itakuwaje
Vipi utamsaidia mti ambaye amepaliwa na maji? Post hii itakwenda kukifundisha jambo hili. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu protini na kazi zake mwilini
Tunahitaji kuwa na protini mwilini. Kuna baadhi ya makundi ya watu wanahitaji protini zaidi. Je unawajuwa hao ni kina nana?, na je unauwa kazi za protini mwilini na athari za upungufu wake? endelea na makala hii. Soma Zaidi...

fahamu vitamini A na kazi zake
Je na wewe i katika wale ambaowanahitaji kujuwa kuhusu Vitamini A, kazi zake na vyakula vya vitamini A. post hii inakwenda kukujuza zaidi pamoja na historia ya vitamini A. Soma Zaidi...

Upungufu wa damu mwilini
Post inaenda kuzungumzia kuhusiana na upungufu wa damu mwilini ambapo tutaona SABABU na dalili zake lakin upungufu wa damu mwilini hujulikana Kama ANEMIA. Soma Zaidi...

Hatua za kufuata baada ya kuhisi kuwa umeambukizwa na virusi vya HIV
Posti hii inahusu zaidi hatua za kufuata unapohisi umeambukizwa na virus vya ukimwi. Kwa sababu watu wengi wanakuwa na kiwewe anapohisi ameambukizwa na virus vya ukimwi kwa hiyo wanapaswa kufanya yafuatayo. Soma Zaidi...

viapo
20. Soma Zaidi...

Namna ugonjwa wa herpes simplex unavyosambaa.
Posti hii inahusu zaidi namna ya ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Soma Zaidi...

Madhara ya ulevi
Poshi hii inahusu madhara ya ulevi.Utegemezi wa pombe kwa kawaida humaanisha kuwa mtu anatumia kiasi kikubwa cha pombe na kuna masuala kuhusu kupoteza udhibiti. Soma Zaidi...

Faida za seli
Posti hii inahusu zaidi faida za seli. Seli ni chembechembe hai za mwili ambazo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

Kazi ya chanjo ya Surua
Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya Surua kwa watoto, ni Aina ya chanjo ambayo utolewa kwa watoto na kufanya kazi mbalimbali mwilini ambazo ni kumkinga mtoto asipatwe na magonjwa. Soma Zaidi...

Vipi utaepuka maumivu ya kichwa ya mara kwa mara?
maumivu ya kichwa ni moja ya dalili za kiafya ambazo huashiria hali isiyo ya kawaida. hata hivyo maumivu ya kichwa yanaweza kutokea hata kama sio mgonjwa. Hapa nitakuletea sababu zinazopelekea kuumwa na kichwa mara kwa mara.Maumivu Soma Zaidi...

Namna ya kutunza nywele za mgonjwa
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi. Soma Zaidi...