NAOMBA MNIELEKEZE JINSI YA MATAYARISHO YA MBEGU ZA PAPAI MPAKA NIANZE KUZITUMIA KAMA TIBA


image


Mbegu za papai ni katika baadhi ya mbegu ambazo hutumika kama dawa, na tunda lake ni katika matunda yenyevirutubisho vingi sana. Mbegu za papai zinatumka kwa matumizi mengi sana kiafya. Je ungependa kujuwa faida za papai na jinsi ya kuandaa mbegu zake kama tiba? endelea na makala hii


SWALI:

Naomba mnielekeze jinsi ya matayarisho ya Mbegu za papai mpaka nianze kuzitumia.

Papai ni katika matunda yenye vitamini C kwa wingi. Ukiachia mbali na utamu wa tunda hili lakini papai mbegu zake zina faida kubwa kiafya mwilini. Makala hii itakueleza faida za mbegu za papai na jinsi ya kuziandaa kama dawa.

 

Faida za mbegu za papai

Mbegu za papai mara nyingi huliwa baada ya kukaushwa na kusagwa unga. Pia unaweza kuzikaanga kidogo ama kuzichemsha.

  1. husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vyema
  2. Husaidia kuzuia kupata saratani
  3. Hulinda figo kufanya kazi vyema
  4. Husaidia mwili katika kupambana na vijidudu vya maradhi
  5. Husaidia kwa wenye kisukari
  6. Husaidia katika kuondosha sumu za kemikali mwilini
  7. Mbegu za papai zina virutubisho mbalimbali

 

Jinsi ya kuandaa mbegu za papai:-

1. Zitoe vyema kwenye papai

2. Zianike hadi zikauke

3. zisage unga

4. Tumia unga wake kwenye chai ama uji kijiko kimoja kila siku.

 

Faida za kiafya za kula papai

1. Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.

2. Pia papai lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper. Pia punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo. Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hawa husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kum eng’enya chakula).

4. Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchija miale hatari ya jua. Pa inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.

45. Papai huaminika kusaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu. Hupunguza hatari ya kuuguwa pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.

 

Soma zaidi hapa



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Faida za kula ndizi
Somo hiki linakwenda kukueleza faida za kiafya za kula ndizi Soma Zaidi...

image Faida za ubuyu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ubuyu Soma Zaidi...

image Tangawizi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za tangawizi Soma Zaidi...

image Limao (lemon)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula limao Soma Zaidi...

image Papai (papaya)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula papai Soma Zaidi...

image Naomba mnielekeze jinsi ya matayarisho ya Mbegu za papai mpaka nianze kuzitumia kama tiba
Mbegu za papai ni katika baadhi ya mbegu ambazo hutumika kama dawa, na tunda lake ni katika matunda yenyevirutubisho vingi sana. Mbegu za papai zinatumka kwa matumizi mengi sana kiafya. Je ungependa kujuwa faida za papai na jinsi ya kuandaa mbegu zake kama tiba? endelea na makala hii Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za stafeli/soursop
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafeli ama soursop Soma Zaidi...

image Faida za kula apple (tufaha)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha Soma Zaidi...

image Faida za mbegu za papai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za mbegu za papai Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula ukwaju
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju Soma Zaidi...