Haki, wajibu na majukumu katika familia ya kiislamu na majirani zake

Haki, wajibu na majukumu katika familia ya kiislamu na majirani zake

4.2. Wajibu na Majukumu katika Familia

a) Wajibu wa Mume kwa mke

Ni wajibu wa mume kumfanyia mkewe yafuatayo ili huruma na mapenzi

yapatikane, Rejea Qur'an (30:21);



i. Kumlisha, kumvisha na kumpatia makazi mazuri kadri ya uwezo wake.

Rejea Qur'an (65:7)



ii. Kumtendea wema, kumhurumia na kumpenda mkewe au wakeze

Rejea Qur'an (4:19)



iii. Kujizuia na kumchukia, kumtukana mkewe au wakeze kwa kuyapuuza maudhi madogomadogo.


iv. Kujizuia kumpiga na kumkaripia (kuwa mkali sana) ila kwa kumpiga pigo hafifu kama kumwonya.

v. Kutunza siri za unyumba na kumfanyia uadilifu kwa kila aina ya haki zake na za ndoa kwa ujumla.

vi. Kumuamrisha mema na kumkataza mabaya na maovu ili kusimamisha maadili ya Kiislamu.

vii. Kumuelimisha elimu sahihi ya mwongozo, kumlea na kutekeleza wajibu wake wa kuumbwa.



b) Wajibu wa Mke kwa Mume

i. Kumtii mumewe katika mambo yote mema tu atakayomuamrisha.

Rejea Qur'an (4:34)



ii. Kumfurahisha na kumliwaza mumewe, hasa katika misuko suko kama Bi

Khadija (r.a) alivyofanya kwa Mtume (s.a.w).


iii. Kuhifadhi na kutunza nyumba na mali ya mumewe na kutumia bila israfu.

Rejea Qur'an (25:67)

iv. Kutosheka na kuridhika na kile anachopewa na mumewe, kiwe kidogo au kingi, kiwe kinatosha au hakitoshi.
Rejea Qur'an (65:7), (33:28-29)



v. Kuwa na subira na uvumilivu juu ya misukosuko na mitihani ya kimaisha.

Rejea Qur'an (2:153).



vi. Kumuusia na kumkumbusha mumewe kumcha Allah (s.w) na kutekeleza wajibu wake wa kuumbwa.




c) Wajibu wa Wazazi kwa watoto

i. Kuwalea watoto kimwili (kiafya) kwa kuwalisha, kuwavisha na kuwapa makazi mazuri kadri ya uwezo na wasaa wao.


ii. Kuwalea watoto kiroho na kimaadili kwa kufanya yafuatayo;

Kuomba dua ya kupatiwa mtoto mwema hata kabla ya kuzaliwa.

Kuwaadhinia sikio la kulia na kuwakimia sikio la kushoto mara tu baada ya kuzaliwa.
Kuwafanyia Haqiqah, kuwanyoa na kuwapa majina mazuri siku ya 7 au 14 au 21 baada ya kuzaliwa au siku yeyote baada ya hizo.
Haqiqah ya mbuzi 1 kwa mtoto wa kike na 2 kwa mtoto wa kiume.



- Masharti ya Mbuzi wa Haqiqah:

- Awe na umri usiopungua mwaka moja.

- Mwenye afya nzuri

- Asiwe na unaomwathiri afya au kilema chochote.

- Masharti ya kugawa nyama ya Haqiqah:

- 1/3 watakula watu wa familia ya mtoto.
- 1/3 itatolewa sadaqa kwa mafakiri na maskini.
- 1/3 itatolewa zawadi kwa majirani na marafiki wa karibu.



Kuwafundisha maadili ya Kiislamu kinadharia na kivitendo kuanzia utotoni mwao.
Kuwaelimisha na kuwalea katika vituo vya Kiislamu kuanzia shule za

awali hadi vyuo vikuu.



iii. Kuwapenda na kuwahurumia kwa kuchunga mipaka ya Allah (s.w).

Rejea Qur'an (9:23-24), (58:22)



iv. Kuwaombea watoto dua njema ya kuwa Wacha-Mungu maishani mwao.

Rejea Qur'an (25:74)



v. Kuwanasihi watoto juu ya Ucha-Mungu na kupigania na kusimamisha dini ya Allah (s.w) kama alivyofanya Nabii; Ibrahim, Yaquub (a.s) na Luqman. Rejea Qur'an (2:132-133), (31:13)




d) Wajibu wa Watoto kwa Wazazi

i. Kuwatii wazazi kwa yale tu yasiyopelekea kumuasi Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w) na si vinginevyo.
Rejea Qur'an (31:15), (29:8)



ii. Kuwaheshimu wazazi na kuongea nao kwa upole na huruma, kutobishana nao au kuwagunia hata kwa ishara.
Rejea Qur'an (17:23-24)

iii. Kuwahurumia wazazi na kuwapa msaada kwa kadri ya uwezo wanahitajia, lakini kwa kuchunga mipaka ya Allah (s.w).


iv. Kuwausia wazazi kumcha Allah (s.w) na kuwaombea dua na magh'fira.

Rejea Qur'an (14:41), (46:15)




e) Wajibu kwa Watumishi wa familia

i. Kuwatendea wema na uadilifu kama ndugu na wanafamilia wetu.

ii. Kuwahurumia na kutowapa kazi ngumu inayowaumiza bila kuwasaidia. iii. Kuwalipa amana zao tulivyokubaliana kwa muda na wakati muafaka.
iv. Kuwalisha, kuwavisha na kuwapa makazi mazuri kama ya watoto wetu. v. Tuwasamehe wanapokosea na kutowafanyia ukatili wowote ule.
vi. Kuwausia kumcha Allah (s.w)



f) Wajibu wa Watumishi wa Familia

i. Kufanya wema na kuwa waadilifu katika kazi zao. ii. Kujiepusha na kuzembea na kutega kazi.
iii. Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kadri uwezo wake.

iv. Kutunza na kuhifadhi vifaa na mazingira vya nyumbani kwa ujumla.



g) Wajibu wa Ndugu na Jamaa wa Karibu

i. Kuwafanyia ihsani jamaa na ndugu wa karibu wa kwa baba na mama.

Rejea Qur'an (4:36), (2:177)

ii. Kuanzia kuwapa sadaka pindi wanapokuwa na haki ya kupewa. iii. Kuwausia kumcha Allah (s.w).




h) Wajibu kwa Mayatima

i. Kuwalea na kuwatendea wema kama watoto wetu au zaidi. ii. Kutowanyanyasa kwa namna yeyote ile.
Rejea Qur'an (107:1-2).

iii. Kuwatunzia mali na amana zao kwa uadilifu.

iv. Kutowadhulumu na kula mali zao kwa njia ya njia ya dhulma.

Rejea Qur'an (4:10)



i) Wajibu kwa Jirani, maskini na wasiojiweza.

i. Kuwafanyia ihsani. Qur'an (4:36), (76:5-11)

ii. Kuwalisha na kuwapa msaada pale wanapohitajia. Qur'an (107:1-3).



j) Wajibu wa wadogo kwa wakubwa

- Kuwatii na kuwaheshimu kwa kila jema lisilopindukia mipaka ya Allah.



k) Wajibu wa Wakubwa kwa wadogo

i. Kutowadharau na kuwanyanyasa wadogo.

ii. Kutojitukuza na kujiona bora kuliko wengine.

Rejea Qur'an (53:32), (49:13)



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 162

Post zifazofanana:-

Vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kif cha khalifa Uthman
Soma Zaidi...

Adam(a.s) na Mkewe Katika Pepo
Adam(a. Soma Zaidi...

Hukumu na sherei zinazohusu ajira na kazi katika uislamu
Wajibu wa KufanyakaziUislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada. Soma Zaidi...

Vyakula vizuri kwa vidonda vya tumbo
Hii ni orodha ya vyakula salama na vizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

YANAYOATHIRI AFYA KATIKA VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kazi za protini mwilini ni zipi?
Virutubisho vya protini vina kazi nyingi mwilini. Zifuatazo ndio kazi protini mwilini Soma Zaidi...

Umbwaji wa mwanadamu kutoka Nutfa (tone la mbegu za uzazi), alaqah (tone la damu, mudgha (pande la nyama) na kuwa mtu kamili
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ' ' ' ' ' ' ' ' ... Soma Zaidi...

Hadithi ya mjakazi wa Mfalme
HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Soma Zaidi...

WACHA KILE ULICHO NA SHAKA NACHO NA FANYA USICHO NA SHAKA NACHO
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '... Soma Zaidi...

UTARATIBU WA KULEA MIMBA
Soma Zaidi...

Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti
2. Soma Zaidi...

DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...