Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu

Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu

Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu

Uchumi Katika Uislamu

Maana ya Uchumi

- Ni uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa mali, rasilimali na huduma mbalimbali katika jamii ili kujenga mahusiano kati ya binaadamu na Allah (s.w).


Sifa za Uchumi wa Kiislamu

1. Dhana ya mafanikio

Huzingatia hatima yake ambayo ni kupata radhi za Allah (s.w) pekee.


2. Dhana ya umilikaji mali

Mmiliki hakika wa pekee wa mali na rasilimali zote ni Allah (s.w).


3. Dhana ya bidhaa

Ni kitu kilicho safi, kizuri, twahara, halali, n.k.



4. Dhana ya matumizi

Haifai kufuja au kutumia mali au rasilimali kwa njia za haramu.



5. Mizani ya wakati katika kutumia

Ni kujiuliza, nini matokeo ya mali au rasilimali hiyo baada ya muda fulani?


Njia na Misingi ya Uchumi Halali Katika Uislamu

i. Pasiwe na udanganyifu wowote katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa au mali.

Rejea Qurโ€™an (17:35), (26:181-183), (83:1-4)



ii. Pasiwe na viapo katika kuuza au kununua bidha, kwani ni miongoni mwa kuuza kwa ujanja-ujanja.
Abu Qatada ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:

โ€œKuwa mwangalifu na viapo vingi katika uuzaji, kwa sababu japo

kunarahisisha uuzaji, kuna punguza barakaโ€ (Muslim).



iii. Pawe na uhuru kamili kwa mnunuzi kuikataa au kuikubali bidhaa baada ya kuiangalia.
iv. Bidhaa yenyewe iwe halali na iwe imechumwa kwa misingi ya halali pia.

v. Kuwepo na maelewano kati ya muuzaji na mnunuzi bila masharti. Dosari yeyote ya bidhaa ijulikane kabla ya manunuzi kufanyika.
vi. Muuzaji awe na uhuru wa kuuza bidhaa yake kwa bei yenye maslahi kwake na isiwe ya kumnyonya mnunuzi.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2545

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰3 web hosting    ๐Ÿ‘‰4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    ๐Ÿ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Aina za hijjah

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
TOFAUTI KATI YA MAKATOZO NA MAAMRISHO KATIKA SUNNAH

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ู‡ูุฑูŽูŠู’ุฑูŽุฉูŽ ุนูŽุจู’ุฏู ุงู„ุฑูŽู‘ุญู’ู…ูŽู†ู ุจู’ู†ู ุตูŽุฎู’ุฑู ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ู‚ูŽุงู„ูŽ: ุณูŽู…ูุนู’ุช ุฑูŽุณููˆู„ูŽ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ูŠูŽู‚ููˆู„ู: "ู…...

Soma Zaidi...
Jinsi ya kukaa itiqaf na taratibu zake

Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada.

Soma Zaidi...
Zijuwe nguzo tano za uislamu na maana zake katika sheria ya uislamu

Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.

Soma Zaidi...
Kwanini lengo la funga halifikiwi na wafungaji wengi

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu

Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume.

Soma Zaidi...