picha

Nini maana ya kutosheka na faida za kutosheka

32.

Nini maana ya kutosheka na faida za kutosheka

32. Kuwa Mwenye Kutosheka



Kutosheka ni kuridhika na neema uliyonayo. Kutosheka ni utajiri kuliko utajiri wote uliopo ulimwenguni.
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema, utajiri si kuwa na mali nyingi lakini utajiri ni kutosheka”. (Bukhari na Muslim)
Muislamu anatakiwa awe ni mwenye kutosheka na kile alichoruzukiwa na Mola wake. Kila mtu amekadiriwa riziki yake na Allah (s.w). Hakuna mwenye uwezo wa kumpunguzia au kumzidishia mtu riziki. Hili linabainishwa katika Qur-an katika usia wa Mzee Luqman kwa mwanawe:



Ewe mwanangu! Kwa hakika jambo lolote lijapokuwa na uzito wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni au katika ardhi, Mwenyezi Mungu atalileta (amlipe mstahiki); bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo yaliyofichikana, (na) Mjuzi wa mambo yaliyo dhahiri. (31:16)
Pia Allah (s.w) anatuhakikishia:


“Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Allah...” (11:6)
Juu ya moyo wa kutosheka Mtume (s.a.w) anatuwaidhi katika Hadithi ifuatayo:
Imesimuliwa katika mamlaka ya Abdullah Bin Amr bin al-’As (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: “Yule aliyeingia Uislamu na akajaaliwa kupata riziki inayotosheleza mahitaji yake muhimu na Mwenyezi Mungu akamfanya kuwa mwenye kutosheka na kila alichotunukiwa, hakika amefuzu kikweli”. (Muslim)




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 2582

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Uandishi wa hadithi wakati wa mtume (s.a.w)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
quran na sayansi

QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Quran na sayansi

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Tanzu (makundi) za hadithi

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Zoezi la 5

Maswali mbalimbali kuhusu fiqih

Soma Zaidi...