Kusimamisha Swala za Sunnah
Baada ya Swala tano za faradhi, kuna swala nyingine za nyongeza alizozisimamisha Mtume (s.a.w) na akatuagiza nasi tumuigize. Swala hizi za ziada tunaziita Swala za Sunnah (Nawafil).
Lengo la Swala za sunnah ni lile lile la swala za faradhi la kututakasa na mambo maovu na machafu. Ni muhimu kwa kila Muislamu kudumisha hizi swala za Sunnah kwa sababu zifuatazo:
1.Kusimamisha Swala za Sunnah ni katika kumtii na kumuigiza Mtume (s.a.w), jambo ambalo ametuamrisha Allah (s.w) katika Qur-an:
2.Kusimamisha swala za sunnah kutatupelekea kufikia ucha Mungu kwa wepesi.
3.Swala za Sunnah pia zina kazi ya kujaziliza swala za faradhi ambazo kwa sababu ya udhaifu wa kibinaadamu hazikuswaliwa kwa ukamilifu unaostahiki.Kama tunavyojifunza katika Hadithi zifu atazo.
Imesimuliwa na Abu Hurairah (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: Amali ya kwanza atakayoulizwa mtu siku ya Kiyama (siku ya Hukumu) ni Swala. Swala zake zikiwa zimekamilika atafuzu. Swala zake zikiwa pungufu atafeli na kuhasirika. Kama swala zake za faradhi zitakuwa zimepungua, Allah (s.w) atasema angalia kwa mja wangu kama anaswala za ziada (Sw ala za Sunnah) ili zichukuliwe kujazia sehemu iliyopungua katika sw ala za faradhi. Kisha ndio vitendo vyake vingine vitaangaliw a kwa namna hiyo hiyoโ. (Tirmidh, Abu Daud, An-Nasai, Ibn Majah na Ahm ad).
Swala za Sunnah ni nyingi. Muislamu anatakiwa, kila atakapohisi kuhitajia msaada wa Allah (s.w) atatawadha na kuswali kwani Allah (s.w) anatuagiza:
โJisaidieni (katika mambo yenu) kwa kusubiri na kuswali, na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu. Ambao wana yakini ya kwamba watakutana na Mola wao na watarejea kwakeโ. (2:45-46)
Hata hivyo katika kitabu hiki tutajihusisha na Swala maalum za Sunnah zifuatazo:
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkuchunga nyakatibza swala tano.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika.
Soma Zaidi...Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana.
Soma Zaidi...Uislamu haukuwekabkiwango maalumu cha mahari. Mwanamke anaweza tajabkiasi atakacho. Ila vyema kuzingatia haya wakayi wa kutamka mahari yako.
Soma Zaidi...KuzuilianaTumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10.
Soma Zaidi...