swala ya idi na nmna ya kuiswali swala ya idi

6.

swala ya idi na nmna ya kuiswali swala ya idi

6. Swala ya Idil-Fitri na Idil-Hajj



Iddil-Fitri na Iddil-Hajj ni swala za Sunnah zilizokokotezwa. Iddi hizi mbili zinazofahamika vyema kwa Waislamu kuwa ni vilele vya siku mbili baada ya kukamilisha nguzo ya Funga na Hajj. Kielelezo cha kilele cha sherehe katika Uislamu si ngoma wala tarumbeta, wala si kula na kunywa sana, bali ni kumkumbuka Allah (s.w) na kumtaja kwa wingi.



Swala ya Idd inaswaliwa baada ya jua kuchomoza na kabla ya jua kufika katikati. Ina rakaa mbili na khutuba kama swala ya Ijumaa lakini tofauti na Ijumaa, khutuba hufuatia baada ya swala. Kama ilivyo swala ya Ijumaa, swala za Idd mbili ni swala za jamaa. Ni sunnah ku swalia Idd uwanjani ili kukusanya jamaa kubwa zaidi.



Swala ya Idd ikiangukia Ijumaa



Mtume (s.a.w) ametoa ruhusa ya kutoswali swala ya Ijumaa iwapo itakuwa imeswaliwa swala ya Idd iliyoangukia siku ya Ijumaa kwa mujibu wa Hadithi zifuatazo:-
Zaid bin Arqam (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alisw alisha Idd kisha akatoa ruhusa kwa swala ya Ijumaa, akasema: 'Anayetaka kuswali na aswali'. (Vitabu Vitano vya Hadith).



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Katika siku yenu hii ya leo zimekutana Idd mbili (yaani Idd na Ijumaa)basi anayetaka asiswali Ijumaa (swala ya Idd inatosheleza) lakini sisi tutaswali Ijumaa'. (Abu Daud).



Kutokana na Hadithi hii ya mwisho, hii ni ruhusa tu na ni bora kuswali Iddi na Ijumaa kwani Mtume mwenyewe alifanya hivyo.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 255

Post zifazofanana:-

Zingatio:
Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote. Soma Zaidi...

Utaratibu kwa wajawazito na wanaonyonshesha wakiwa na virusi vya ukimwi na ukimwi
Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha Soma Zaidi...

benki za kiislamu na njia zake za kuingiza kipato
Benki za KiislamuBenki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sio ule wa riba. Soma Zaidi...

Ni yapi masharti ya Udhu na kujitwaharisha
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kabichi
Soma Zaidi...

kitabu cha matunda
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Juhudi za Waislamu Katika Kuhuisha Harakati za Kiislamu Zama za Nyerere hadi leo
i. Soma Zaidi...

NECTA FORM YWO GEOGRAPHY PAST PAPERS
Soma Zaidi...

Hukumu za Kuangalia Mwezi wa Ramadhani
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ubuyu
Soma Zaidi...

Dalili za mkojo mchafu na rangi za mkojo na mkojo mchafu
Hapautajifunza rangi kuu za mkojo na dalili zako kiafya, mkojo mchafu na dalili zake Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Dola ya Kiislamu Wakati wa Makhalifa
Soma Zaidi...