swala ya tarawehe na namna ya kuiswali, rakaa zake na suna zake.

5.

swala ya tarawehe na namna ya kuiswali, rakaa zake na suna zake.

5. Swala ya Tarawehe
Swala ya Tarawehe ni miongoni mwa Sunnah zilizokokotezwa. Swala hii huswaliwa katika mwezi wa Ramadhan tu wakati wowote kati ya kipindi baada ya swala ya Isha na kuingia kwa swala ya Alfajiri. Umuhimu wa swala hii umedhihiri katika Hadithi ifuatayo:



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akisisitiza swala ya usiku katika mwezi wa kufunga (Ramadhani), bila ya kuifaradhisha kwao. Alikuwa akisema: Atakaye swali katika usiku wa mwezi wa kufunga, akiwa na imani na akitarajia malipo (kutoka kwa Allah (s.w), dhambi zake zilizotangulia husamehewa. (Muslim)



Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali Tarawehe katika sehemu ya pili ya usiku (katika wakati ule ule wa Tahajjud). Mtume (s.a.w) aliswali Tarawehe pamoja na masahaba katika jamaa siku tatu, kisha akaacha na akawa anaswalia nyumbani kwake kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:



โ€˜Aysha (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikwenda msikitini usiku na akaswalisha Tarawehe na watu wakaswali naye. Asubuhi watu wakasimuliana habari hiyo. Mtume (s.a.w) siku ya pili alikwenda kuswalisha watu wakajaa msikitini. Alifanya hivyo hivyo siku ya tatu. Asubuhi siku ya nne watu wakapeana habari na wakajazana zaidi msikitini kwa ajili ya sw ala ya Tarawehe lakini Mtume (s.a.w) hakw enda


kuswalisha. Baadhi ya watu walisema kwa sauti โ€œswalahโ€, lakini Mtume (s.a.w) hakwenda msikitini mpaka Alfajir. Alipomaliza sw ala ya Alfajir aliwakabili watu na kuwaeleza: โ€œJambo lenu halikuwa limefichikana kwangu, lakini nilichelea kuwa kama ningaliendelea mfululizo na swala hiyo ya Tarawehe huenda ingalifanywa kuwa ni faradhi kwenu na huenda m ungalishindw a kuitekeleza โ€. (Muslim)



Pamoja na Hadithi hii, pia Mtume (s.a.w) aliwasisitiza Waislamu kuswali swala za Sunnah majumbani mwao na kuwahakikishia kuwa kufanya hivyo kuna malipo makubwa zaidi. Swala ya Tarawehe iliendelea kuswaliwa na kila mtu nyumbani kwake katika kipindi chote cha Mtume (s.a.w) na kipindi cha Khalifa wake wa kwanza (Abu Bakar). Khalifa wa pili, Umar bin Khattab, alianzisha tena kuswali swala ya Tarawehe kwa jamaa msikitini kama inavyoendelea mpaka hivi leo.



Idadi ya Rakaa za Swala ya Tarawehe



Kumekuwepo na maelezo tofauti kuhusiana na idadi ya rakaa za Swala ya tarawehe kutoka kwa wanazuoni tofauti. Lakini kutokana na Hadithi iliyosimuliwa na Mama Aysha (r.a) na kupokelewa na Maimamu wa Hadithi, Mtume (s.a.w) hakupata kuswali zaidi ya rakaa 11 katika mwezi wowote ule. Hadithi ya Jabir (r.a) iliyopokelewa na Ibnu Khuzaimah na Ib n Hibban, Mtume ameripotiwa kuswali rakaa nane za tarawehe na rakaa tatu za witri pamoja na Masahaba wake na kisha siku iliyofuatia akawa hakutoka kwenda kusalisha.



Ama kuhusiana na kuswali rakaa ishirini, ni kweli kuwa Khalifa Umar, Uthman na Ali (r.a) waliswali kwa rakaa hizo. Imamu Ibnu Hibban amesema kuwa mwanzoni ilikuwa ni rakaa kumi na moja isipokuwa kisomo (kisimamo) kilikuwa kirefu kiasi cha watu kuchoka. Hivyo baadaye ikaamuliwa kuwa idadi ya rakaa iongezwe na kisomo kipunguzwe na kuwa cha wastani ingawaje jambo hili halikuingiza Swala ya Witri, kutoka hapo kwenye rakaa 20 ilifika kwa badhi ya wengine akiwemo Imamu Malik hadi rakaa 36 ikiwa kisomo kimezidi kufupishwa. Iliyo sunnah ni kuswali tarawehe kwa rakaa 11-8 za kisimamo cha usiku cha kawaida na rakaa 3 za witri. Kwa kuwa mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur-an inahimizwa sana kuwa Waislamu wahitimishe Qur-an yote alau kwa kusoma juzuu moja kila siku. Tarawehe ni swala sawa na swala nyingine hivyo kusihi kwake kunafungamana na kupatikana khushui, masharti na nguzo zote za swala. Ama hizi tarawehe zinazoswaliwa katika misikiti mingi mbazo Imamu hupata sifa kwa kuswali mbio mbio pasipo na mazingatio wala utulivu ni kinyume kabisa na utaratibu wa swala. Watu wengi ambao huharakisha kumaliza swala ya tarawehe kwa kiasi cha kutokamilisha nguzo za swala hawapati malipo yoyote kutokana na swala zao. Bali kwa kuwa watu hawa wanaifanyia swala mchezo hapana cha kutarajia zaidi ya adhabu kali waliyoahidiwa na Allah (s.w):


โ€œBasi adhabu itawathibitikia wanao swali, ambao wanapuuza swala zaoโ€. (107:4-5)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 7064

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    ๐Ÿ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Milki ya raslimali katika uislamu

Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.

Soma Zaidi...
Sunnah za swaumu, sunnah ambazo zinaambatans ns kufungabmwezi wa Ramadhani

Yajuwe mambo ambayo yanapendeza kuyafanya wakati ukiwa umefunga Ramadhani.

Soma Zaidi...
Hizi ndio nyakati za swala tano na jinsi ya kuchunga nyakati za swala.

Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkuchunga nyakatibza swala tano.

Soma Zaidi...
Lengo la hijjah na matendo ya ibada ya hijjah na mafunzo yatokanayo

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Uzuri wa Benki za kiislamu

Kwa nini benki za kiislamu ni bora kuliko benki nyingine?

Soma Zaidi...
Ni upibutaratibu wa kuingia eda na kutoka eda

Katika uislamu hakuna sheria ya mwanamke kuingizwa eda na kutolewa eda kama ilivyozoeleka. Endelea na post hii ujifunze zaidi

Soma Zaidi...
Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini

Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha.

Soma Zaidi...
NAMNA YA KUCHINJA KATIKA UISLAMU

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ูŠูŽุนู’ู„ูŽู‰ ุดูŽุฏูŽู‘ุงุฏู ุจู’ู†ู ุฃูŽูˆู’ุณู ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ุนูŽู†ู’ ุฑูŽุณููˆู„ู ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ู‚ูŽุงู„ูŽ: "ุฅู†ูŽู‘ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ูŽ ูƒูŽุชูŽุจูŽ ุงู„ู’ุฅูุญ...

Soma Zaidi...
Madhara ya riba kwenye jamii

Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba?

Soma Zaidi...