Namna ya kutambuwa kibla na umuhimu wa kuelekea kibla wakati wa kuswali

4.

Namna ya kutambuwa kibla na umuhimu wa kuelekea kibla wakati wa kuswali

4. Kuelekea Qibla



Kuelekea Qibla ni sharti la nne la kusimamisha swala. Katika hali ya kawaida Muumini ni lazima aelekee 'Qibla wakati akiswali.Qibla ni neno la Kiarabu linatokana na neno 'Qabala' lenye maana ya kuelekea sehemu au upande ambao watu huelekeza nyuso zao. Kwa mtazamo wa Qur-an, Qibla ni sehemu wanapoelekea waislamu wakati wa kuswali. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Qibla ni sehemu ya katikati inayowaunganisha waumini kuwa mwili mmoja (kitu kimoja).


'Na po pote wendako geuza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu . Na hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wako. Na Mw enyezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda. (2:149)



Ummati wa Muhammad (s.a.w) Qibla chake ni Ka'aba, nyumba tukufu ya Allah iliyoko mjini Makkah, Saudi Arabia. Waislamu wote ulimwenguni huielekea Ka'aba wakati wa kuswali. Swala yoyote itakayoswaliwa bila ya kuelekea upande ilipo Ka'aba, pasipo na dharura inayokubalika kisheria kama vile kuwa mgonjwa, au kuwa safarini, ha is wih i.



Namna ya Kutafuta Qibla



Kukisia ulipo mji wa Makka, Saudi Arabia, ambao ndani yake iko Ka'aba ni jambo rahisi kwa kutumia utaalamu wa Jiografia. Chombo


kizuri cha kumuwezesha mtu kukisia ilipo Ka'aba ni ramani ya dunia. Utakapojua ulipo katika sehemu yoyote ya dunia utaweza kujua Ka'aba iko upande gani wa dira kutokea pale ulipo kwa kutumia jua au chombo cha dira (Magnetic Compass). Kwa mfano ukiwa Tanzania, utaelekea Kaskazini kamili, ukiwa Pwani kama vile Dar es Salaam na ukiwa bara kama vile Kigoma, utaelekea Kaskazini ya Kaskazini Mashariki.



Kabla ya Muislamu hajaanza kuswali, hasa anapokuwa mgeni wa mahali hana budi kufanya jitihada ya kutafuta Qibla kwanza. Ni vyema mtu asafiripo awe na dira (Magnetic Compass) na ramani ili vifaa hivi vimsaidie kutafuta Qibla, vinginevyo itabidi awaulize wenyeji wa sehemu h iyo.



Mtu akishindwa kabisa kukibaini Qibla baada ya kujitahidi mwisho wa jitihada zake, popote atakapoelekea patafaa, kwani hii sasa imekuwa ni dharura, huku tukizingatia kuwa 'Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu'.


Na Mashariki na Magharibi ni ya Mw enyezi Mungu. Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mw enyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na Mwenye kujua (kukubwa kabisa vile vile). (2:115)




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 772


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Nabii Yunus(a.s) Amuomba Allah(s.w) Msamaha
Ndani ya tumbo la samaki, Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

nguzo za uislamu
Soma Zaidi...

quran na sayansi
Soma Zaidi...

Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah
7. Soma Zaidi...

Kuangamizwa Waovu na Kuokolewa Waumini
Baada ya kuonywa wasionyeke, Allah(s. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)
Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a. Soma Zaidi...

Utaratibu wa kutekeleza hija, matendo hatua kwa hatua, pamoja na kusherehekea sikuku baada ya hija
4. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA QALQALA
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Tofauti kat ya sura za Maka na Madina
Sura za Makka na Madina Kutokana na historia ya kushuka kwake sura za Qur-an zimegawanywa katika makundi mawili - sura za Makka na sura za Madina. Soma Zaidi...

Quran si Mashairi kama wanavyodai makafiri
(i)Dai kuwa Qur-an ni Mashairi aliyotunga Muhammad (s. Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kuulingania Uislamu kwa Jamii Yake
Nabii Ibrahim(a. Soma Zaidi...