Ni zipi sifa za imamu wa swala?

Ni zipi sifa za imamu wa swala?

Sifa za Imamu Imamu ni kiongo kuongoza swala:



1. Mwenye zi. Mtu yeyote mwenye sifa zifuatazo anaweza
kuweza kuisoma Qur-an vizuri na mwenye
kuielewa vizuri.
2. Anayefahamu na kuelewa vizuri hadithi na Sunnah.
3. Mwenye tabia njema na siha nzuri.
4. Mwenye umri mkubwa (sifa hizi zizingatiwe kwa mfuatano wake).



Kama itatokea kwenye msikiti mmoja kuna watu wengi wenye sifa hizi, itabidi ipigwe kura. Pia kiongozi au mtu mwenye mamlaka katika jamii atakuwa ndiye mwenye haki ya kuwa Imamu. Hali kadhalika mtu akiwa nyumbani kwake, atakuwa ndiye mwenye haki ya kuwa Imamu. Sifa hizi zinabainishwa katika Hadithi ifuatayo:



Abu Mas ’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule aliye na uwezo mkubwa zaidi wa kusoma Kitabu cha Allah (Qur-an) atakuwa Imamu wao. Kama watakuwa sawa kwa kusoma Qur-an basi atakuwa Imamu yule aliye na ujuzi mkubwa wa Hadithi, na kama wako sawa basi yule aliyetangulia kuhajiri (kuham a kutoka Makka kw enda Madina) na kama wako sawa katika kuhajiri, basi yule aliye na umri mkubwa kuliko wote ndiye atakayekuwa Imamu. Hakuna mtu atakaye kuwa Imamu wa yule aliyemzidi madaraka (au yule aliye na mamlaka juu yake) na wala hatakaa katika nyumba yake kwa kumpa heshima mpaka apate ridhaa yake. Na hakuna mtu atakayekuwa Imamu katika nyumba au familia ya mwingine. (Muslim).



Imamu wa msikiti atakapochaguliwa hapatakuwa na mwingine kuswalisha bila ruhu sa yake. Ni vibaya mno kujipachika Uimamu mahali bila ya ridhaa ya watu unaowaongoza. Aliyejipachika Uimamu swala yake haitasihi.



Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema kuwa watu w atatu ambao sw ala zao hazitakubaliwa ni: β€œYule anayeswalisha w atu na huku hawamtaki, anayekuja kwenye swala nyuma (kuja kwenye swala baada ya wakati kupita, pia kuswali mwenyewe nyuma ya mstari), na yule anayemfanya mwanamke huru kuwa mtumwa”.(Abu Daud, Ibn Majah).



Kumfuata Imamu baada ya kuwekwa ni jambo la lazima. Hata kama Imamu huyo atafanya makosa au dhambi kubwa kiasi gani kabla Waislamu hawajamtoa na kumweka mwingine itabidi lazima wamfuate kutokana na Hadithi ifuatayo:-



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema, β€œJihadi ni wajibu chini ya Amir yeyote akiwa mcha-Mungu, au si mcha-Mungu na hata kama atakuwa amefanya madhambi makubwa, na swala ni wajibu nyuma ya kila Imamu akiwa mcha-Mungu au si mcha-Mungu na hata akiwa amefanya madhambi makubwa ”. (Abu Daudi)
Inavyotakiwa, kama Imamu ataonekana kuwa anakiuka miiko ya Kiislamu kwa kutenda yale yaliyokatazwa katika Uislamu, kama vile zinaa, ulevi, wizi, n.k. itabidi Waislamu wamtoe kwenye Uimamu na kuweka Imamu mwingine mwenye sifa zilizotajwa. Kabla ya kuchagua mwingine watawajibika kumfuata Imamu huyo huyo muovu.Hekima yake ni kuepusha ugomvi, mifarakano baina ya waislamu.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3913

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰3 web hosting    πŸ‘‰4 Dua za Mitume na Manabii    πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Nini maana ya kusimamisha swala

Post hii inakwenda kukufundisha maana ya kusimamisha swala kama inavyotumika kisheria.

Soma Zaidi...
Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga.

Soma Zaidi...
Wanaowajibika kuhijji

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango

Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi.

Soma Zaidi...
Nguzo za udhu ni sita

Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu.

Soma Zaidi...
Aina ya biashara zilizo haramu kwenye uislamu

Hapa utajifunza aina za biashara ambazo ni haramu.

Soma Zaidi...