Kulipia Ramadhani
Mtu anapodaiwa siku alizo kula katika mchana wa mwezi wa Ramadhani,au siku ambazo swaumu yake ilibatilika, si lazima azilipe mara tu baada ya Ramadhani, japo ni bora mtu kumaliza deni lake haraka. Tunafahamishwa katika Hadith kuwa Bibi ‘Aysha (r.a) alikuwa akilipia Ramadhani katika mwezi wa Shaaban:
Aysha (r.a) ameeleza: “Nilikuwa na madeni ya swaumu ya Ramadhani. Sikuweza kulipa kadha ila katika mwezi wa Shaaban. (Bukhari na Muslim).
Hali kadhalika si lazima mtu kulipa mfululizo siku zote anazodaiwa, bali anaweza kuzilipa kidogo kidogo kutokana na Hadith ifuatayo:
Ibn Umar (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema juu ya kulipa Ramadhani: (Mtu) akitaka na afarikishe; na akitaka na afululize. (Daru Qu tni).
Kama mtu amechelewa kulipa siku anazodaiwa mpaka Ramadhani nyingine ikaingia, basi kwanza ataifunga hiyo Ramadhani iliyomuingilia. Baadaye ndipo alipe hiyo deni yake wala halipi fidia; iwe kuchelewa huko ni kwa udhuru ama si kwa udhuru. Lakini ni vizuri zaidi kulipa siku anazodaiwa kabla ya kuingia Ramadhani nyingine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu, kusimamisha swala za Sunnah (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hapa utajifunza taratibu za kutaja mahari katika uislamu.
Soma Zaidi...Katika kipengele hiki tutajifunza nguzo za uislamu.aina tano za nguzo za uislamu,dhana ya nguzo za uislamu,lengo na umuhimu wa nguzo za uislamu
Soma Zaidi...Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...Posti hii itakwenda kukufunza utofauti kati ya uadilifu na usawa
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "إنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِح...
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu.
Soma Zaidi...