picha

Swala ya Idi al-fitir na namna ya kuiendea

Swala ya Idi al-fitir na namna ya kuiendea

Iddil -Fitri



Iddil-Fitri ni siku kuu ya Kiislamu ya kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Ramadhani. Mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imefaradhishwa funga ambayo imeambatanishwa na matendo mbali mbali ya sunnah, umekusudiwa uwe mwezi wa mafunzo na mazoezi ya kumfanya mja awe mchaji Mungu katika kiwango kinachostahiki kwa kipindi chote cha mwaka mzima.


Iddil-Fitri ndicho kilele cha mafunzo haya ambapo Waislamu wanafurahia na kumshukuru Allah (s.w) kwa kumaliza salama mafunzo haya muhimu na wakati huo huo humuomba Allah (s.w) ayafanye mafunzo hayo yawe yenye kuwafikisha kwenye lengo lililokusudiwa. Hivyo, moja kwa moja inadhihiri kuwa Iddil-Fitri haisherehekewi kwa mavazi mazuri na kwa vyakula na vinywaji vizuri tu, bali kilele cha sherehe hii kinafikiwa kwa kuswali swala ya Iddil-Fitri na kumtukuza na kumuhimidi Allah (s.w) sana kwa Takbira.



Swala ya Iddil-Fitri



Swala ya Idd mbili - Iddil-Fitri na Iddil-Hajj (kilele cha ibada ya Hija) ni sunnah zilizokokotezwa. Swala ya Idd inaswaliwa kwa rakaa mbili na kufuatiwa na Khutuba mbili kama zile zinazosomwa kabla ya swala ya Ijumaa. Swala ya idd ina Takbira 12,takbira 7 hutolewa katika rakaa ya kwanza kabla ya kusoma suratul-Faatiha na takbira 5 huletwa katika rakaa ya pili. vile vile kabla ya kusoma suratul-Faatiha.Mahali pa kuswalia Idd ni bora pawe uwanjani ili Waislamu wakusanyike pamoja kutoka sehemu mbali mbali za mji. Mtume (s.a.w) alikuwa akifanya hivyo. Ni sunnah kula chochote kabla ya kuswali Iddil-Fitri kama tunavyofahamishwa katika Hadith zifu atazo:



Anas (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah hakw enda kusw ali Iddil- Fitri mpaka alipokula Tende katika idadi ya witri. (Bukhari).
Buraydah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa hatoki kwa swala ya Iddil-Fitri mpaka awe amekula (Kitu) na hakuwa anakula katika s iku ya kuchinja (Iddil-Haj) mpaka asw ali (Dirim i).



Ni sunnah kuleta takbira mara kwa mara kuanzia pale mwezi wa Shawwal unapoandama mpaka baada ya swala ya Iddil-fitri. Takbira


Tafsiri ya Takbira:
Allah Mkubwa, Allah Mkubwa, Allah Mkubwa hapana mola ila Allah Allah Mkubwa, Allah Mkubwa na shukurani zote ni za Allah. Allah Mkubwa aliyetukuka, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi, na namtakasa asubuhi na jioni. Hapana Mola ila Allah. Wala hatumuabudu yeyote ila Yeye peke yake, tunamtakasa yeye na dini yake hata kama w atachukia makafiri.Hapana mola ila Allah peke yake. Ameisadikisha (ameitimiza) ahadi yake na akamnusuru mja (Mtume s.a.w) wake, na akalitukuza jeshi lake, akalipa ushindi kundi lake. Hapana mola ila Allah. Allah Mkubwa. Ewe Allah, teremsha rehma zako juu ya Muhammad, na Maswahaba wake Muhammad, na waliomnusuru Muhammad, na Wakeze Muhammad, na kizazi chake Muhammad, na uwape salama na amani kwa wingi.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 4575

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 ai web app     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 web hosting     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Utaratibu wa kuzika maiti ya kiislamu, hatua kwa hatua

Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa.

Soma Zaidi...
Swala ya tahiyatul masjidi yaani maamkizi ya msikitini, pamoja na swala za qabliya na baadiya

Post hii inakwenda kukujuza kuhusu swala za qabliya, baadiya na tahiyatul masjid.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kufanya suluhu kati ya mume na mke.

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kufanya suluhu katika ndoa.

Soma Zaidi...
Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa

- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.

Soma Zaidi...