Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake

Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake

Funga za Kafara



Funga za kafara ni funga anazolazimika Muislamu kuzileta ili ziwe kitubio baada ya kutenda kosa fulani. Yaani funga hizi zimewekwa na sheria ya Kiislamu kama fidia au faini baada ya kutenda kosa na kutaka kutubia kwa Allah (s.w). Zifuatazo ni funga za kafara kama zilivyobanishwa katika Qur-an na Hadith:



(i) Kufunga miezi miwili mfululizo kwa Muislamu aliyemuua mtu kwa bahati mbaya na akakosa mali ya kulipia fidiya kama inavyobainishwa katika Qur-an:


Na haiwi kwa Mu is lamu kumuua Muislamu (mwenziwe kusudi) ila kwa kukosea.Na mwenye kumuua Muislamu kwa kukosea basi ampe uungwana mtumwa aliye Muislamu, na pia atoe fidiya (Malipo) kuwapa warithi wake. Isipokuwa waache weny ewe kwa kufanya kuwa ni sadaqat (yao). Na aliyeuawa akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Mu is lam, basi ampe uungwana mtumwa aliye Muislamu (basi, hapana wa kupewa fidiya). Na kama (aliyeuawa) ni moja wa watu ambao kuna ahadi baina yenu na baina yao; basi warithi wake wapewe malipo na pia apewe uungwana mtumwa aliye Muislamu. Na asiyepata basi afunge miezi miwili mfululizo. Ndio kitubio kitokacho kwa Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mw eny e Hekim a. (4:92).



(ii) Kufunga miezi miwili mfululizo kwa mtu atakayemsusa mkewe kwa kumfananisha na mama yake kwa kutamka: โ€œWewe kwangu mimi nakuona kama mgongo wa mama yangu.โ€ Maneno haya yalitamkwa na Sahaba wa Mtume (s.a.w) - Aus Ibn Samit (r.a), walipogombana na mkewe. Maneno haya kwa jamii ya Waarabu wakati ule wa Mtume (s.a.w) yalikuwa mabaya sana na yalikuwa ni ya kumdhalilisha mwanamke. Hivyo baada ya kufanyika kitendo hiki, mkewe huyu Sahaba alikwenda kwa Mtume (s.a.w) kushitakia; lakini Mtume (s.a.w) hakuweza kumpatia ufumbuzi wa tatizo lake. Mama huyu alizidi kusononeka sana huku akitarajia nusra ya Allah (s.w).Ni katika hali hii ya kusononeka huyu mama Allah (s.w) alishusha kwa Mtume wake aya zifuatazo:



Mwenyezi Mungu amekwisha sikia usemi wa mwanamke yule anayejadiliana nawe sababu ya mumewe, na anashtaki mbele ya



Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu; anayasikia majibizano yenu; hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kuona. Wale miongoni mwenu wawaitao wake zao mama zao, (kwa hivyo wakajiepusha nao wasiwaingilie wala wasiw ape ruhusa kuolewa na mwanaume wengine), hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa.Wanasema neno baya na la uwongo.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye msamaha, mwenye maghfira.(58:1-2).



Baada ya kosa la huyu Sahaba kubainishwa katika aya hizi, aya zifuatazo zinatoa kitubio au adhabu ya kosa hili:


Na wale wawaitao wake zao mama zao kisha wakarudia katika yale w aliyoyasema (wakataka kuw arejea wake zao w aendelee kuishi kama kawaida), basi wampe mtumwa huru kabla ya kugusana.Mnapewa maonyo kwa haya. Na Mwenyezi Mungu anajua (yote) mnayoyatenda. Na asiye pata (mtumwa) basi afunge saumu ya miezi miwili mfululizo kabla ya kugusana; na asiyeweza basi awalishe maskini sitini.


(Mmeambiw a haya ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu,na kwa makafiri iko adhabu iumizayo. (58:3-4).



(iii) Kufunga siku tatu mfululizo kama kafara ya kuvunja kiapo kama tunavyoamrishwa katika aya ifuatayo:


โ€œMwenyezi Mungu hatakuteseni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakukamateni kwa viapo mlivyo viapa kwa nia mlioifunga bara bara. Basi kafara yake ni kuw alisha maskini kumi kwa chakula cha katikati mnacho walisha watu wa majumbani mwenu, au kuwavisha, au kumpa uungwana mtumwa. Lakini asiyeweza kupata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na vilindeni viapo vyenu (msiape kisha msitimize). Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainisheni aya zake ili mpate kushukuru โ€ (5:89).



(iv) Kufunga miezi miwili mfululizo kama kitubio cha kufanya tendo la ndoa kati ya mume na mkewe makusudi katika mchana wa mwezi wa Ramadhani.



(v)Mtu aliyehirimia Hijja au Umra haruhusiwi kuwinda na endapo atavunja amri hii ya kutowinda kitubio au kafara yake ni kufunga kama inavyobainishwa katika aya ifuatayo



โ€œEnyi mliomini! Msiue mawindo na hali (ya kuwa) mumo katika Hija au Umra. Na miongoni mwenu atakayemuua kwa kusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa (kuchinja) kilicho sawa na alichokiua,katika wanyama wanaofugwa,kama watakavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu mnyama huyo apelekwe iliko Kaโ€™aba, au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili ... (5:95). Muda wa kufunga utategemeana na thamani ya mnyama ambaye angalimchinja katika hesabu ya vibaba vya chakula.



(vi) Kama mwenye kuhiji au kufanya Umra atavunja miiko ya Ihram au iwapo atashindwa kutekeleza baadhi ya matendo ya Hijja, atalazimika kufunga kama inavyobainishwa katika aya ifuatayo:


Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na kama mkizuiwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana (nao ni mbuzi). Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjioni mwao. Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana vya kumuudhi kichwani mwake (akafanya yaliyokatazwa kama vile kunyoa), basi atoe fidia kwa kufunga au kutoa sadaqat au kuchinja wanyama (2:196).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3267

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰5 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti

Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali.

Soma Zaidi...
Taratibu za kuchaguwa mchumba katika uislamu

Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...
Je inafaha kuingizwa eda na kutolewa?

Kuingizwa au Kutolewa EdaKatika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh.

Soma Zaidi...
Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu

Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu.

Soma Zaidi...
Nadharia ya uchumi wa kiislamu

Dhana ya uchumi wa kiislamu imejegwa jui ya ukati na kati. Dhana hii imetofautiana sana na dhana nyinginezo kama ubepari na ujamaa.

Soma Zaidi...
Namna ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mambo anayofanyiwa mtu anayekaribia kufa

Haya ni maandalizi anayofanyiwa mtu aliye katika kilevi cha kifo yaani sakaratul maut

Soma Zaidi...
Kutoa kati kwa kati

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...