Hadathi ya kati na kati (Janaba).
Hadathi ya kati na kati (Janaba).
Mtu hupatwa na hadathi ya kati na kati kwa kupatwa na Janaba. Janaba ni hali inayompata mtu baada ya kufanya kitendo cha jimai (kitendo cha ndoa) au kutokwa na manii kwa kuota au kwa namna nyingineyo. Mtu mwenye janaba yuko katika hali chafu kulingana na sharia ya Allah (s.w) na ameharamishiwa kufanya ibada hizi:
(i)Kuswali (rejea Qur-an 4:43, 5:6)
(ii)Kutufu.
(iii)Kukaa Msikitini.
βAysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Msielekeze milango ya nyumba hizi msikitini kwa sababu si halali msikiti kwa mwanamke mwenye hedhi au kwa mtu mwenye janaba β. (Abu Daud)
(iv) Ku is oma Qur-an hata kwa moyo.
Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: βWenye hedhi na wenye janaba hawatasoma chochote kutoka kwenye Qur-an β (Tirmidh)
Si vibaya kwa mtu mwenye janaba kula, kuongea au kugusana na watu. Pia kutokana na mafundisho ya Mtume (s.a.w) si lazima mtu kukoga mara tu baada ya kufanya kitendo cha jimai na mkewe, hasa ikiwa usiku bali anatakiwa aoshe sehemu za siri na atawadhe alale, kisha akiamka ndipo akoge kwa kujitwaharisha kwa ajili ya swala ya Alfajiri. Mafundisho haya tunayapata katika hadithi ifuatayo:
Aysha (r.a) ameeleza kuwa: Mtume (s.a.w) alipotaka kula au kulala akiwa na janaba, alikuwa kwanza akitawadha kama anavyotawadha kwa ajili ya swala. (Bukhari na Muslim).
Umeionaje Makala hii.. ?
Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.
Soma Zaidi...Uislamu haukuwekabkiwango maalumu cha mahari. Mwanamke anaweza tajabkiasi atakacho. Ila vyema kuzingatia haya wakayi wa kutamka mahari yako.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake.
Soma Zaidi...Uislamu umekataza tabia ya kuombaomba kama ndio njia ya kuendesha maisha. Pia ukaweka suluhisho la kukomesha tabia hiyo
Soma Zaidi...Hapa utajifunza nguzo kuu za swaumu. Kama hazitatimia nguzo hizi basi swaumu itakuwa ni batili.
Soma Zaidi...Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala.
Soma Zaidi...