Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?
Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?
Tumejifunza kuwa jamii yenye kudumisha nguzo ya Zakat na kutilia mkazo suala la kutoa mali na huduma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jamii yenye kuendelea kiuchumi na yenye kuishi kwa furaha na amanai ya kweli ya kibinafsi na kijamii. Jamii ya Mtume (s.a.w) na ile ya Makhalifa waongofu ni mfano wa wazi ulio mbele yetu. Jamii yetu hivi leo, pamoja na mahimizo ya utoaji wa Zakat na Sadaqat katika majukwaa mbali mbali bado hatuyapati matunda ya Zakat katika jamii. Miongoni mwa sababu zinazowafanya Waislamu wasipate matunda yanayotarajiwa kutokana na utoaji wa Zakat na Sadaqat ni:
        (i)Wengi miongoni mwa Waislamu Hawatekelezi Nguzo ya Zakat
Wengi miongoni mwa Waislamu wenye uwezo wa kutoa zakat hawaitekelezi nguzo ya zakat na hawajihimizi kutoa misaada midogo na mikubwa kwa wale wanaohitajia.
        Kwa sababu ya kutotoa Zakat na Sadaqat kwa wale wenye uwezo miongoni mwa Waislamu, kumeipelekea jamii ya Waislamu kuwa duni na dhalili mbele aya Makafiri na Washirikina.
        (ii)Wengi Watoa Zakat na Sadaqat Hawatekelezi Masharti ya Utoaji
Miongoni mwa matajiri wachache wanaojitahidi kutekeleza nguzo ya Zakat na utoaji mali kwa ajili ya kuwasaidia wanaohitajia, hawazingatii masharti ya utoaji.Baadhi ya matajiri hutoa mali zao kwa ria na hufuatilia kwa masimbulizi. Utoaji wa namna hii umefutiwa baraka na hauwezi kumnufaisha mwenye kutoa wala jamii. Ubaya wa kutoa mali au msaada wowote kwa ria na kwa masimbulizi umedhihirishwa wazi katika aya ifu atayo:
        Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia; kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonesha watu, wala hamwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho. Basi hali yake ni kama hali ya jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha ikalifikia (jabali hili) mvua kubwa (likasukuma udongo wote huo) na ikaliacha tupu. Basi haw atakuw a na uw ezo (wa kupata) chochote katika walivyovichuma; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri”. (2:264)
        Kuna baadhi ya miongoni mwa Waislamu matajiri wanaotoa Zakat bila ya kuzingatia wale wanaostahiki (Rejea Qur-an, 9:60). Badala yake huenda na kapu la fedha msikitini na kumgawia kila mtu atakayekuwa tayari kupokea. Ugawanyaji huu wa Zakat hupelekea kupewa wasiostahiki na kuwakosesha wanaostahiki na kuwabakisha katika dhiki yao. Utoaji wa namna hii huibakisha jamii ya Waislamu katika dhiki na katika uadui na uhasama. Kuna baadhi ya Waislamu pamoja na kutoa Zakat na Sadaqat, hawazingatii mipaka ya halali na haramu katika uchumi wao. Wengine huchuma kwa njia za haramu ambazo hazinufaishi jamii bali huiingiza jamii katika matatizo ya rushwa, riba, kamari, wizi, ujambazi na udhalimu wa kila namna.
        (iii) Zakat haikusanywi na Kugawanywa Kijamii
Tumejifunza kuwa utoaji na ugawaji wa Zakat, ili unufaishe jamii hauna budi kusimamiwa na jamii. Lazima jamii ya Kiislamu iwe na watu maalum wanaopita kwa kila Muislamu mwenye uwezo wa kutoa zakat, na kuipokea Zakat yake kisha kuikabidhi kwa Mtunzaji wa Baitil-Mali (Mhazini), kisha kuigawa kwa wanaostahiki.
        Sehemu kubwa ya jamii ya Waislamu hivi leo, haifuati utaratibu huu wa ukusanyaji na ugawaji wa Zakat na sadaqat bali kila mwenye kutoa Zakat huigawanya mwenyewe kwa wale wanaostahiki walio machoni mwake. Kuacha Zakat mikononi mwa watoaji binafsi, kuna hasara kubwa zifuatazo:
        Kwanza; hapitiwi na mhimizo wa makusudi juu ya utoaji wa Zaka, kiasi kwamba wenye kustahiki kutoa Zakat hujisahau na hatimaye kuacha kutoa Zakat kabisa.
        Pili; kwa kutokuwa na utaratibu wa ugawaji, sehemu kubwa ya Zakat hupewa wasiostahiki na wale wanaostahiki hubaki na dhiki yao.
Umeionaje Makala hii.. ?
*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko.
Soma Zaidi...Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.
Soma Zaidi...Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua.
Soma Zaidi...Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha taratibu za kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Dhana ya uchumi wa kiislamu imejegwa jui ya ukati na kati. Dhana hii imetofautiana sana na dhana nyinginezo kama ubepari na ujamaa.
Soma Zaidi...Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...Umuhimu wa KusimamishaSwala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.
Soma Zaidi...- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.
Soma Zaidi...