Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka

Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka

Msisitizo wa Utoaji wa Zakat na Swadaqat katika Uislamu



1.Kutoa Zakat ni faradhi na nguzo ya tatu ya Uislamu. Amri ya kutoa Zakat ya vile Allah (s.w) alivyoturuzuku iko wazi katika Qur'an. Hebu turejee aya chache zifuatazo:


Waambieni waja wangu walioamini, wasimamishe Swala na watoe katika vile tulivyowaruzuku, kwa siri na kwa dhahiri, kabla haijafika siku isiyokuwa na (msaada unaopatikana kwa) kujikomboa wala urafiki (14:31).


Enyi mlioam ini! Toeni katika vile tulivyokupeni kabla haijafika siku am bayo hapatakuwa kujikom boa wala urafiki (wa kusaidiana) wala uombezi. Na w aliokufuru ndio w aliojidhulumu (kw eli kw eli). (2:254).



2.Utoaji wa Zakat na Sadaqat ndio kitambulisho cha Uislamu na Ucha-Mungu wa mtu kama tunavyojifunza katika Qur-an:
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uwongozi
kwa wamchao Mwenyezi Mungu. Ambao huyaamini yasiyoonekana (maadam yamesemwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake) na husimamisha Sala na hutoa katika yale tuliyowapa. (2:2-3).



Sio wema (tu huo peke yake) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi (katika kusali,. Yako na mema mengine). Bali wema (hasa) ni (wa wale) wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na wanawapa mali juu ya kuwa wanayapenda - jamaa na mayatima na maskini na wasafiri (walioharibikiwa) na waombao na katika (kuwakomboa) watumwa, na wakawa wanasimamisha sala na kutoa zaka, na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na dhara na (katika) wakati wa vita; hao ndio waliosadikisha (Uislamu wao); na hao ndio wamchao Mungu. (2:177)
Tunajifunza kutokana na aya hizi kuwa utoaji mali kwa ajili ya Allah ni miongoni mwa matendo yanayompelekea mtu kuwa Mcha-Mungu. Kwa ujumla Qur-an inapotaja sifa za waumini huwa ni pamoja na watoao Zakat. Kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:



Na wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake, ni marafiki wao kwa wao. Huyaamrisha yaliyo mema na huyakataza yaliyo mabaya, na husimamisha sala na hutoa Zakat na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio ambao Mw enyezi Mungu ataw arehem u. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mw enye Hikima. (9:71).



3. Utoaji mali kwa ajili ya Allah (s.w) ni miongoni mwa mambo makubwa ya kumpelekea mja kufuzu hapa duniani na huko akhera kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


Hakika wamefuzu Waislamu. Ambao katika sala zao huwa ni wanyenyekevu. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi. Na ambao (nguzo ya) Zakat w anaitekeleza. (23:1-4).


'..Na wabashirie wanyenyekevu ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hutetemeka na wanavumilia juu ya yale yanayowasibu na wanasimamisha swala na katika vile tulivyowapa wanatoa ' (22:34-35).


'Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika'. (2:274).


4. Kutotoa mali kwa ajili ya Allah ikiwa ni pamoja na Zakat na Sadaqat ni jambo mojawapo kubwa litakalomfanya mja afeli katika maisha yake ya hapa duniani na ya huko akhera hata kama atajiita Muislamu na kutekeleza baadhi ya matendo mengine ya Kiislamu. Adhabu watakayoipata wale wenye kufanya ubakhili na kujizuilia wasitoe katika njia ya Allah (s.w) na huku wana uwezo, imewekwa bayana katika Qur'an na Hadithi. Hebu tuzingatie aya chache zifuatazo:


'Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Allah, wape habari ya adhabu iumizayo. Siku (mali yao) yatakapotiwa moto w a Jahannam na kw a hayo vikachomw a vipaji vya nyuso zao na mbavu na migongo yao(na huku wanaambiwa):'Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikizia nafsi zenu, basi onjeni yale mliyokuw a mkiyakusanya '. (9:34-35).


Na afanyae ubakhili, asiwe na haja ya viumbe wenzake. Na akakadhibisha mambo mema (asiyafanye) tutamsahilishia njia ya kwendea Motoni (92:8-10).
Hebu pia tuzingatie Hadithi inayotufahamisha juu ya adhabu itakayowafikia wale wanaoyafanyia ubakhili yale aliyowaruzuku Allah (s.w).



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Yule am baye Allah (s.w) am empa m ali lakini haitolei Zakat, m ali yake itageuzw a kuwa nyoka mkubwa (mwenye sumu kali). Ataviringwa shin goni mwake katika siku ya Hisabu na kuanza kumuuma. Baadaye nyoka huyo atasema: 'Mimi ni mali yako, mimi ni hazina yako iliyohifadhiwa '. Kisha Mtume alisoma (aya ifuatayo): 'Wala usiwaone wale ambao wamefanyaubakhili katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni bora kwao. La, ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa (madude ya kunasa shingoni) za yale waliyoyafanyia ubakhili- siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyafanya ' (3:180). (Bukhari).




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 320


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri. Soma Zaidi...

Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana
12. Soma Zaidi...

Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza
Funga za Sunnah. Soma Zaidi...

Sababu nyengine zilopelekea kushushwa kwa suratul ikhlas
Soma Zaidi...

Muhutasari wa sifa za wanafiki
Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:- (1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo. Soma Zaidi...

Mtazamo na Msimamo wa Uislamu Juu ya Kudhibiti Uzaz (uzazi wa mpango) na hukumu yake
Soma Zaidi...

'Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye'
Soma Zaidi...

Hadithi Ya 30: Allaah Amefaridhisha Mambo Ya Dini Tusiyapuuze
Soma Zaidi...

Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

kuwa mwenye kusamehe, na faida zake
27. Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)
Mtume(s. Soma Zaidi...

taratibu na namna ya kutaliki, na mambo ya kuzingatia
Taratibu za Kutaliki KiislamuKama palivyo na taratibu za kuoa Kiislamu ndivyo hivyo pia ilivyo katika kuvunja ndoa. Soma Zaidi...