Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu
Ni nini husababisha mdomo kuwa mchungu?
1.Mdomo kutokuwa msafi. Hii ni kawaida wakati umelala mdomo bakteria waliokuwa wapo mdomoni wanaendelea kufanya kazi yao, kula mabaki ya chakula na kuendelea kuzaliana. Kumbuka mate yana kazi ya kusafisha mdomo,lakini wakati umelala mate hayawezi kufanya kazi hii kwani huwezi kuyatoa. Hivyo uchafu huendelea kujizalisha bila ya kutolewa. Hali hii inaweza kusababisha mdomo kuwa mchungu unapoamka.
Vyema usile kitu muda huu, kabla ya kupiga msaki. Safisha kinywa vyema ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya muda mchache. Pia kama ulitoka kulala baada ya kutema mate kwa muda mchache yaani baada ya mdomo kujisafisha hali hii inaweza kuondoka bila ya wasi wala hakuna ulazima wa kupiga mswaki, kwani mdomo una sifa ya kujisafish awenyewe kwa kutumia mate.
2.Matumizi ya madawa ya antibiotics au antidepressants. Dawa hizi pindi mdu anapozitumia hufyonzwa ndani ya mwili na kutolewa kwa kupitia mate na kusababisha mate kuwa machungu. Mfano wa dawa hizi ni:-
A. Tetracycline
B.Gout medication kama allopurinol na lithium
C.Madawa yanayotumika kutibu maradhi ya moyo.
Baada ya kuacha kutumia dawa hizi ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya siku chache. Pia unaweza kunywa juisi ya vitu vichachu kama hali itaendelea kukusumbuwa.
3.Ujauzito, hali ya mdomo kuwa mchungu ama kuwa na ladha ya chuma kwa wajawazito ni kawaida na hali hii kutaalamu hufahamika kama dysgeusia ama metallic taste. Hutokea kwa uda wa siku kadhaa kisha huondoka. Baadhi ya wajawazito wanapata ladha ya pesa, yaani kama ulishawahi kuweka mdomon hela ya sarafu, ile ladha unayoipata ndio ambayo huwapata baadhi ya wajawazito.
4.Kama unatumia dawa za kuongeza vitamini, unaweza kupata ladha hii. Kuna baadhi ya dawa za vitamini zina madini mengi ya metali. Madini hayokama zinc, shaba, chuma na chromium. Kama dawa hiyo ina madini haya inaweza kubadili ladha ya mdomo na kuwa chungu
5.Ni dalili ya maradhi ya ini. Kama ini lako halifanyi kazi vyema ama lina matatzo, mwili utakuwa na kiasikikubwa cha ammonia ambayo ni sumu. Hatimaye kubadili ladha ya mdomo.
6.Mashambulizi ya kwenye mfumo wa upumuaji. Wakati mfumo wa upumuaji unapokuwa katika mashambulizi ya bakteria ama virusi au fangasi, inaweza kuathiri ladha ya mdomo.
7.Kama umecheuwa, hali hii inaweza kupelekea kubadilika kwa ladha ya mdomo
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1456
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 kitabu cha Simulizi
Imani potofu juu ya ugonjwa wa Ukimwi.
Posti hii inahusu zaidi imani potofu juu ya ugonjwa wa Ukimwi,ni Imani walizonazo watu wengi kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi. Soma Zaidi...
Dalili za unyanyasaji wa kimwili
Unyanyasaji wa kimwili. Unyanyasaji wa watoto kimwili hutokea wakati mtoto amejeruhiwa kimwili kimakusudi.
Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa watoto kingono ni shughuli yoyote ya kingono na mtoto, kama vile kumpapasa, kushikana mdomo na sehemu Soma Zaidi...
Namna ya kusaidia vijana wakati wa kubarehe
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia vijana wakati wa kubarehe, ni njia za kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na mwelekeo , Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA KWIKWI
Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo. Soma Zaidi...
Maana ya afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya afya Soma Zaidi...
Mkojo wa kawaida
Posti hii inahusu zaidi mkojo wa kawaida kwa kila mwanadamu na unavyopaswakuwa, mkojo wa kawaida kwa binadamu huwa na sifa zifuatazo. Soma Zaidi...
Mambo yanayoathiri Uponyaji was jeraha.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo yanayoweza kuadhiri Uponyaji wa jeraha.jeraha huleta maumivu makali sana, vilevile Uvimbe, kutoa usaha. Pia jeraha hutofautiana katika kupona kwa mtu mzima na Mtoto. Soma Zaidi...
Zijue sehemu za mwili zinazochomwa chanjo.
Posti hii inahusu zaidi sehemu ambazo zinapaswa kudungwa chanjo, hizi ni sehemu zile zilizopendekezwa kwa ajili ya kuchoma chanjo kwa kadiri ya kazi ya chanjo. Soma Zaidi...
Ijue rangi za mkojo na maana zake katika mwili kuhsu afya yako
Posti hii inahusu zaidi rangi za mkojo na maana zake, hizi ni rangi ambazo uweza kutokea kwenye mkojo wa mtu mmoja na mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa magonjwa, chakula,na mtindo wa maisha inawezekana unywaji wa maji au kutokunywa maji. Soma Zaidi...
Zijue sababu za kupoteza fahamu.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kupoteza fahamu, ni sababu ambazo umfanya mtu kupoteza fahamu kwa sababu mbalimbali kama ifuayavyo. Soma Zaidi...
Ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha
Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha hii ni chanjo wanayopewa watoto wadogo chini ya miaka mitano kwa lengo la kuzuia kuharisha chanjo hiyo kwa kitaalamu huitwa Rotarix. Soma Zaidi...
Upungufu wa damu mwilini
Post inaenda kuzungumzia kuhusiana na upungufu wa damu mwilini ambapo tutaona SABABU na dalili zake lakin upungufu wa damu mwilini hujulikana Kama ANEMIA.
Soma Zaidi...